Wandugu tatizo la maelezo ya Mwanasheria Mkuu liko wapi?................naomba mnielimishe............
Nilivyomuelewa AG.......amesema kulingana na utaratibu wa Bunge AG akisha draft......inarudishwa Bungeni kuridhiwa..........au?
Pia ukipitia hansard hili jambo linaeleweka.......au?
BTW: Hivi wewe Chenge pamoja na ndondo zako zote hizo.........ilikuwaje ukatuingiza mikengeni (mikataba mibovu na manunuzi ya hovyo) namna ile............yaani naendelea kuridhika kuwa wewe ni FISADI kweli kweli.............damn
Nilivyomuelewa AG.......amesema kulingana na utaratibu wa Bunge AG akisha draft......inarudishwa Bungeni kuridhiwa..........au?
TAARIFA KWA UMMA
Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya "Timu ya Kampeni" ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika "Timu ya Kampeni". Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.
Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.
Imetolewa na
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
29 Machi, 2010