Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yapangua hoja ya Dr. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yapangua hoja ya Dr. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Mar 30, 2010.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  TAARIFA KWA UMMA

  [​IMG]

  Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili. Muswada huo ulipitishwa tarehe 11 Machi 2010 katika Mkutano wa 18 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au “kinyemela”. Kifungu kidogo cha 7(3) kinaweka masharti yanayohitaji uthibitisho wa wajumbe wanaounda Timu za Kampeni za Wagombea wa Kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani. Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.

  Kwa kuzingatia madai ya Mheshimiwa Dk. Slaa, Vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa maelezo mbalimbali kuhusu suala hili. Katika mazingira haya, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

  Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na Wadau na Wabunge, Bunge liliagiza Muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.

  Marekebisho hayo ni:

  (a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.

  (b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi.

  Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni”. Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.

  Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya “Timu ya Kampeni” ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika “Timu ya Kampeni”. Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.

  Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

  Kwa kuzingatia maelezo haya kuhusu hoja za Wabunge ninaridhika kuwa kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Uchaguzi kimezingatia matakwa na maagizo ya Bunge sawa sawa. Kifungu hicho hakikuingizwa kwenye Sheria “kinyemela” au kwa hila. Aidha, mtiririko wa mamlaka za kuthibitisha Timu ya kampeni una mantiki sahihi yenye lengo zuri la kufanikisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.


  Imetolewa na
  OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
  29 Machi, 2010
   
 2. N

  Nanu JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Dr. Slaa, tunahitaji mwongozo wako hapa. Mwanasheria Mkuu anasema hakuna kifungu kilichoongezwa kinyemela! Lakini hapa hawajajibu la nani asimamie au apitishe timu ya kampeni ambayo ndiyo hoja kubwa! Nadhani hawa jamaa wanajitapatapa na inabidi aje atolee maelezo hayo bungeni!! Hii taarifa aliyoitoa wala hailezi "concerns" zilizotolewa na wabunge, it is a mere press release ionekane kuwa hawajafanya makosa! Dr. Slaa tunahitaji comments zako!
   
 3. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Serikali wametoa ufafanuzi mzuri ila pia Dr. Slaa anastahili pongezi nyingi kwa kuwa makini na hivyo siku za mbeleni ataifanye serikali pia iwe makini.
   
 4. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ufafanuzi mzuri upi? Hii bla bla ambayo hata haielweki?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mfamaji hakuna kinachoeleweka hapo zaidi ya bla bla tulizozizoea siku zote
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Nyongeza hizo zilitakiwa zifikishwe Bungeni tena kwa majadiliano na kueleweshana zaidi. Ni jambo kubwa hilo,si sawa na editorial wakuu ambazo editor anaweza kufanya ilimradi asipoteze maana ya sentensi au kifungu cha maneno. Hapa waliweka vipengele vipya kabisa ambavyo vina impact kisiasa.

  Wasitudanganye kwa Press Release ya kupaka mafuta hapa. Bravo Dr. W. Slaa. Yaamushe haya matendaji yaliyolala!!!
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160

  swala hapa si utaratibu, swala hapa ni sheria, je serikali inahaki ya kuongeza kifungu chochote kinyemela nje ya Bunge.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sheria hii imewahangaisha wabunge wetu wengi akiwemo Dr Slaa. Kifungu kinacholalamikiwa hapa kuingizwa "kinyemela" kina madhara gani? Nilidhani Dr Slaa kwa msimamo wake usioyumba angeisimamia vilivyo sheria hii lakini inaonekana inaelekea kumkwaza tangu mwanzo. Sheria hii na nyingine zote sio msahafu. Tuiache ianze kufanya kazi na kama kutahitajika marekebisho itarudi tena Bungeni. Tuna sheria nyingi mbovu ambazo akina Jaji Nyalali walipendekeza zifutwe lakini bado zipo na sisikiii zikilalamikiwa!
   
 9. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Tatizo lenu wengi hapa ni ushabiki. Ukiweka pamba machoni hata apite tembo, huwezi kuona.

  Serikali wametia maelezo yao, na najua Dr. Slaa ni makini na aliuliza kwa nia njema, basi tumsubiri yeye atuambie kama maelezo hayo ni sahihi?

  Kila siku tunasikia wabunge wametoa mapendekezo na waziri ameyakubali, hayo mapendekezo si yanachapishwa baada ya bunge kuisha?
   
 10. N

  Nanu JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba hao amboa wametajwa kuwa wakaguzi wa timu za kampeni ni watu wa CCM na ni waajiriwa wa serikali za mitaa za CCM. Hawa wote au wengi wao ni wana CCM. Sasa lazima wawe na maagizo ya kuhakikisha CCM inashinda kinyemela, wanaweza kuingiza mamluki kwenye timu kampeni ya wagombea wa upinzani, na hii kwa CCM wala si aibu na wala si dhambi, it is the order of the day!!!
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  swala si madhara makubwa ama madogo, hapa ni je sheria inaruhusu kuchomekea vifungu vya kisheria nnje ya taratibu za kisheria.
   
 12. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kusema kweli hapa serikali haijajibu hoja ....ni bla bla tu hapa. Tunahitaji watu makini kama Dr. Slaa Bungeni jamani
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye highlight zingatia. Kwa mambo ya Tz yalivyo slow kama konokono au kobe itachukua muda mrefu sana kurekebisha mapungufu ya sheria hiyo. Wewe umeona kabisa sheria mbovu alizo shauri Jaji Nyalali zifutwe au kurekebishwa bado hakuna jitihada zimefanyika.

  Sasa hii ambayo ina maslahi kisiasa zaidi kwa chama kilichoshika hatamu unafikiri ni rahisi ikubaliwe kurekebishwa baada ya kuirushusu itumike? Mimi naonelea ni vema mapungufu yaliyojitokeza mapema hii basi yafanyiwe kazi sasa ili ikianza kutumika isilete mgongano kama inavyoonekana kwa sasa.


  Sasa hivi tunashukuru kuwa angalao tuna wabunge wachache makini ambao wanasoma documents na si wachapa usingizi ambao wanasubiri kuamshwa na makofi ya kupitisha miswada ambayo wala hawakuwa wanaisoma wala kuisikiliza wakati ikiwasilishwa. Once again Bravo Dr.Slaa, I am in your shoes.
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Soma vizuri hiyo taarifa ya AG. Imejitosheleza kama "haumhurumii" sana Dr Slaa.
   
 15. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wildcard nimesoma nionacho ni taarifa yenye kuumauma maneno, kama Dr Slaa katamka hadharani kuwa kumefanyika ujanjaujanja wakuchomekea mambo kwenye sheria.
  sasa atamke bayana kuwa Kisheria inaruhusiwa kuongeza ama kupunguza mambo nje ya taratibu za bunge.
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh,mambo hayo..Iko kazi.
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  AG wa sasa tofauti na waliomtangulia ni msikivu, mchapakazi sana. Amekaa na kufanya kazi kwenye mihimili yote mitatu sasa. Tumpe muda.
   
 18. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,421
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Dr. Slaa ajitokeze aeleze kama maelezo ya ofisi ya AG yamejibu hoja yake au laah.
   
 19. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania daima, serikali bado inajikanganya kuhusu nani aliongeza kifungu cha 7(3). Wakati inasema ofisi ya Marmo ilitengeneza jedwali la marekebisho, katika marekebisho yaliyotajwa hicho kifungu cha 7(3) hakimo:


  "Hata hivyo, taarifa hiyo ilisisitiza kuwa pale bungeni viliongezwa vipengele viwili 7(1) na 7(2), si vitatu.


  Ilisema: “Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na wadau na wabunge, Bunge liliagiza muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na wabunge kuhusu makundi ya sanaa na viongozi wa vyama wanaoweza kumsaidia mgombea wakati wa kampeni za uchaguzi, serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S. Marmo, iliandaa jedwali la marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.
  “Marekebisho hayo ni: (a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7. (b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa kampeni za uchaguzi."

  Haya hata Slaa anakiri yalijadiliwa na ndiyo yalipaswa kuwekwa. Je aliyeweka kipengele cha 7(3) ni nani? Endelea na taarifa ya serikali:

  “Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge zima, mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni” kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.”

  Bado mapendekezo ya Shellukindo hayakufanyiwa kazi kwani yeye alitaka "idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu" Hakutaka mtu wa kuidhinisha idadi ya hiyo; na bado hata marekebisho ya sasa hayajatamka idadi hiyo!
   
 20. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #20
  Mar 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mmmh , kwahiyo ....?
   
Loading...