Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yapangua hoja ya Dr. Slaa

Hivi Dr. Slaa hakuna uwezekano wa kutazama kanuni zenu upya kabla ya mswaada kuwekwa sahihi na Raisi kuwa sheria kuhakikiwa na Bunge ? Hatujui sheria ngapi zimechomekewa vifungu wanadhalilisha taaluma zao na uaminifu wao sasa una mashaka makubwa Shame !!!
 
Hivi Dr. Slaa hakuna uwezekano wa kutazama kanuni zenu upya kabla ya mswaada kuwekwa sahihi na Raisi kuwa sheria kuhakikiwa na Bunge ? Hatujui sheria ngapi zimechomekewa vifungu wanadhalilisha taaluma zao na uaminifu wao sasa una mashaka makubwa Shame !!!
Nakubaliana na wewe, inaonekana kuna uwezekano wa sheria nyingi kuchimekewa vitu ambavyo havikujadiliwa bungeni hasa ukitilia maanani kuwa wabunge wetu wengi huwa hawasomi miswada na sheria zenyewe baada ya kusainiwa.
Bado maelezo ya serikali yanajikanganya sana, kwani kilichojadiliwa na kamati ya bunge zima ni kipengele kinachohusu vikundi vya sanaa na siyo mtu wa kuhakiki timu ya kampeni.
 
Hiyo ndio adha ya mazoea ya kuachia wasio na mamlaka kikatiba kuongeza wanachotaka katika sheria inayopitishwa na bunge kwenu wabunge mmejifunza nini ? Mtabadilika au kama mazoea mtaendelea kusema Ndiyo na kupiga meza ?
 
kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati "Timu ya Kampeni" iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.

Hapo ndipo penye utata. Kifungu hicho kiliongezwa na nani? Na nani aliyeamua kuwa atakayesimamia "Timu ya Kampeni" ni nani?

 
Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya "Timu ya Kampeni" ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika "Timu ya Kampeni". Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa,kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.
Maelezo haya yanaonyesha kuwa wanasheria walitunga sheria badala ya Bunge. Kazi ya wanasheria ni kutafsiri sheria na siyo kutunga sheria. Pia maelezo hayo hayaondoi malalamiko kuwa maudhui ya sheria yamebadilishwa nje ya kikao cha Bunge. Halafu kama kifungu hicho kilikuwa kimepitishwa na Bunge iweje hakipo kwenye kumbukumbu za Bunge (Hansadi)?​


Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

Maelezo haya yanaeleza utaratibu kama ulivyo, hayathibitishi kuwa utaratibu sahihi ulifuatwa katika kuingiza kifungu kipya. Kitu cha kushangaza mwanasheia hakusema chochote kuhusu masharti mapya ya mgombea wa uraisi, ubunge na udiwani yaliyoingizwa nje ya kikao cha bunge.​
 
mhhh
sheria hata haijabikiriwa imeshaanza kuwa na viraka. Mpaka ifanye kazi vizuri hii sheria itajihitaji viraka vingi.
 
TAARIFA KWA UMMA - ni umma upi ambao haujui hata taratibu za kupitisha miswaada ya sheria Bungeni na baadae kuwa Sheria??? Sasa yaonekana kana kwamba Umma ndo umafundishwa ili uamini yale ambayo Mwanasheria Mkuu (Serikali) inataka wayajue hata kama sivyo ndivyo!.

Tarehe 17 Machi, 2010, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na hivyo Muswada huo kuwa Sheria Kamili- Kama Muswaada kabla ya kutiwa saini na Rais huwa sio Sheria, ni vipi unakuwa "Sheria Kamili???"

Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au "kinyemela". - Je, vifungu vingine katika Sheria hiyo vimewekwa kwa kuzingatia utaratibu sawa na hicho kinacholalamikiwa kama sivyo, basi jibu ni kukubalina na Slaa kwani uhalali ni kuzingatia utaratibu, vinginevyo ni kama kulizunguka Bunge kwa kwa kuomba lipitishe Mswaada ambao baadae unaanza kucheza nao kwa utashi wako na si kwa kuzingatia maamuzi ya Bunge ambayo yamo pia kwenye rekodi za Bunge (Hansard).



Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge = hoja ya kubishaniwa hapa ni Je, kilikuwepo tarehe ambayo Bunge lilipitisha Muswaada?? (Muswaada uliposomwa kwa mara ya tatu kifungu kwa kifungu na wabunhge wote kuridhia??), Je, rejea kwenye Hansard inasemaje kuhusu kifungu hiki?.



Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi - Kwa nini ufafanuzi usiwe kwa vifungu vyote na iwe kwa hicho kinachobishaniwa tu kama kweli utaratibu wa kukingiza ulizingatiwa???

Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3). Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.- Marekebisho hayo ni:


(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.


(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi. - Je, marekebisho husika waliyowasilishwa na Waziri yaligusa pia kifungu kidogo cha 7(3) ??Kama jibu ni hapana, Je, tukisema Muswaada uliopitishwa na Bunge sio huo ambao umesainiwa na Rais haitakuwa sahihi kama inavyodaiwa na Dr. Slaa??



Kwa kuwa uamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno "timu ya kampeni". Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu. Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati "Timu ya Kampeni" iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.- Je, kifungu kinachohusu tafsiri ya maneno (Interpretation Provision) kinahusianaje na kubadilisha vifungu vya ndani vya Sheria tena kwa kuongeza kifungu kipya???.Je, ikitokea ubishani wa tafsiri ya Kifungu hicho kilichoongezwa (rules of interpreation)katika kupata maana halisi ya nia ya Bunge (intention of the Parliament),je hivyo kinavyosomeak asas ndivyo Bunge lilivyotaka kiandikwe, au tafsiri inatokana na nia ya Mwanasheria Mkuu (Intention of the Attorney General ) na sio ya Bunge??

Iwapo hoja toka kwa Mhe. W.H. Shellukiondo (Mb) ilihusu kutazamwa upya timu ya Kampeni ilitolewa Bungeni wakati Muswaada haujapitishwa (kwa maana ya kusomwa kwa mara ya tatu), je, kwenye jedwwali la marekebisho (schedule of Amendments) lililowasilishwa na Waziri husika kabla ya Bunge kuridhia Muswaada wa Sheria, kwa nini kifungu cha 7(3) halikutajwa kuwa kimeongezwa ili Wabunge wajue na kuridhia kwa pamoja marekebisho husika???



Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya "Timu ya Kampeni" ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika "Timu ya Kampeni". Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge -Kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu itatumia taaluma ya Sheria kurekebisha Sheria hata nje ya yale yaliyopitishwa na Bunge, kwa nini tusiamini kuwa ofisi hii nyeti imechukuwa madaraka ya Bunge ya kutunda Sheria badala ya kuandika na kuwasilisha Miswaada ya Sheria ili Bunge ipitisha kadri ambavyo Bunge limeiagiza???


Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. -Kama huu ndo utarataibu uliozoeleka, kwa nini tusiamini kuwa Miswaada yote inayopitishwa na Bunge huwa badae inafanyiwa tena nyongeza na Ofisi ya Mwansheria Mkuu kabla ya kutiwa saini na Rais kuwa Sheria jambo ambalo Bunge haliwi tena chombo cha kutunga Sheria na badala yake linaelekezwa na kuridhia yale waandishi wa Sheria wanayoyajua kwa taaluma yao. Na ikiwa Mswaada unaweza kurekebishwa kwa kuongezwa vifungu kwa jinsi hii, kuna haja gani ya miswaada kuwa inasomwa zaidi ya mara moja Bungeni kabla ya kupitishwa kuwa Sheria??? na kwa nini kama ofisi ya Mwansheria Mkuu iliona ipo haja ya kuwa na nyongeza ya kifungu katika kifungu cha 7 isingesubiri kuwasilisha tena Bungeni Mswaada wa marekebisho (Miscellenous Amendments) badala ya kujiamuliwa tu kuongeza hata yale ambayo pengine Bunge lisingeyakubali eti kwa kuwa ni uzoefu???


Hapa utata tupu!
 
TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni, Mheshimiwa Dk Wilbrod Slaa alitoa madai kwamba kuna kifungu kidogo cha (3) ambacho kimeingizwa katika kifungu cha 7 cha Sheria hiyo isivyo halali au “kinyemela”. Kifungu kidogo cha 7(3) kinaweka masharti yanayohitaji uthibitisho wa wajumbe wanaounda Timu za Kampeni za Wagombea wa Kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani. Mheshimiwa Dk. Slaa anadai kwamba kifungu cha 7(3) hakikuwepo kabisa kwenye Muswada wa Sheria uliojadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.
......hapa chini Ofisi ya Mwansheria Mkuuinatoa ufafanuzi


................... Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa Taarifa kwa Umma yenye lengo la kufafanua kile kilichotokea Bungeni hususan uandishi wa kifungu cha 7(3) katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi.

Kutokana na marekebisho yaliyopendekezwa na Wadau na Wabunge, Bunge liliagiza Muswada uchapishwe kwa mara ya pili. Baada ya Muswada huo kuchapishwa kwa mara ya pili, kifungu cha 7 hakikuwa na vifungu vya (1), (2) na (3).

....Ningependa kufahamu hivyo vifungu viwili vya kwanza vilikuwa vinasemaje......................tuendelee

Hata hivyo, kwa kuzingatia hoja zaidi zilizotolewa na Wabunge kuhusu makundi ya Sanaa na Viongozi wa Vyama wanaoweza kumsaidia Mgombea wakati wa Kampeni za Uchaguzi, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera na Uratibu wa Bunge) Mhe. Philip S.Marmo, iliandaa Jedwali la Marekebisho ambalo lilifanya marekebisho katika kifungu cha 7.
Marekebisho hayo ni:

(a) kukitaja kifungu cha 7 kilichokuwepo kuwa kifungu kidogo cha (1) katika kifungu hicho hicho cha 7.

(b) kuongeza kifungu kidogo cha (2) ili kuongeza makundi ya sanaa na kundi la watu wanaoweza kufadhiliwa na Mgombea kwa chakula, vinywaji, malazi na usafiri wakati wa Kampeni za Uchaguzi.


Kwa kuwauamuzi huu ulifanyika wakati wa Kamati ya Bunge Zima, Mwenyekiti aliagiza kwamba suala hilo la kuweka marekebisho hayo, lizingatiwe wakati wa kutoa tafsiri ya maneno “timu ya kampeni”.
Kwa kuzingatia mapendekezo ya Mhe. William H. Shellukindo kwamba idadi ya timu ya kampeni itazamwe na iwekwe wazi badala ya kuiacha wazi tu




Kidogo inachanganya....badO ningependa kufahamu vifungu viwili vya mwanzo ni vipi.................na kwa upande mwingine.................... inaonyeshwa Dr. W.Slaa alishiriki/alikuwepo hadi kufikia hapo................haya tuendelee

Katika kutekeleza hayo, kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa kwenye kifungu cha 7 cha Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ambapo tafsiri ya msamiati “Timu ya Kampeni” iliwekwa katika kifungu ambacho msamiati huo umetumika. Hii ndiyo sababu kifungu kidogo cha (3) kiliongezwa.

Kwa kuzingatia taaluma ya uandishi wa sheria ilibidi kuongeza masharti yenye amri ya kisheria (Legislative rules) katika kifungu hicho ili tafsiri ya “Timu ya Kampeni” ijitosheleze. Masharti hayo ni yale yanayohitaji uthibitisho wa watu waliomo katika “Timu ya Kampeni”. Kwa maelezo haya ni dhahiri kuwa, kifungu cha 7 kilirekebishwa na kupitishwa na Bunge.

Mpaka hapo ..................kwa mtizamo wangu naona ni sawa.....ni mamboya "drafting" hayo..............

Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima. Katika hatua hii, Wabunge wanaweza, kupitia Kanuni ya 86(II) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, kupendekeza mabadiliko katika Muswada. Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

......................agreed

Kwa kuzingatia maelezo haya kuhusu hoja za Wabunge ninaridhika kuwa kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Uchaguzi kimezingatia matakwa na maagizo ya Bunge sawa sawa. Kifungu hicho hakikuingizwa kwenye Sheria “kinyemela” au kwa hila. Aidha, mtiririko wa mamlaka za kuthibitisha Timu ya kampeni una mantiki sahihi yenye lengo zuri la kufanikisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.


Imetolewa na
OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI
29 Machi, 2010
.....................agreed


Kwa kweli ningependa kuona Dr. W Slaa akijibu/akitoa ufafanuzi wa madai yake further wa hii hoja.............Dr Slaa please.....
 
Kweli sisi tunafanywa mabwege.

Hebu Mwanasheria Mkuu atupe nukuu ya hansard ya siku hiyo kuthibitisha majibu yake.

Nadhani CA anakwepa majukumu yake ya kiuwajibikaji
 
Sheria hii imewahangaisha wabunge wetu wengi akiwemo Dr Slaa. Kifungu kinacholalamikiwa hapa kuingizwa "kinyemela" kina madhara gani? Nilidhani Dr Slaa kwa msimamo wake usioyumba angeisimamia vilivyo sheria hii lakini inaonekana inaelekea kumkwaza tangu mwanzo. Sheria hii na nyingine zote sio msahafu. Tuiache ianze kufanya kazi na kama kutahitajika marekebisho itarudi tena Bungeni. Tuna sheria nyingi mbovu ambazo akina Jaji Nyalali walipendekeza zifutwe lakini bado zipo na sisikiii zikilalamikiwa!
Kwa hiyo kwa maana hiyo hakuna sababu ya Bunge kutunga sheria kwa kuwa ofisi ya mwansheria mkuu ina uwezo wa kuweka vipengele ambayo havina madhara
 
Nimepata nukuu ya hansard ya tarehe 11 Februari ulipopitishwa mswada huu, kifungu hiki kilichukua muda mrefu kufikia concesus. Ila conclusion iliyotolewa na Press Release ya AG ndiyo uliyo uliokuwa uamuzi wa Bunge. Sourcce::http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-18-14-2010.pdf

Kifungu cha 7

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii nianze kwa kuishukuru Serikali katika kuleta marekebisho katika eneo hili ambapo kimezaliwa kifungu kidogo cha (2) ambacho kinasomekana kama tunavyoona kwenye schedule of amendment. Lakini kwenye Kamati eneo hili tulichukua muda mrefu sana na Wabunge kama wadau wakuu katika Muswada walisema haitoshi tu kuongelea vikundi vya sanaa. Mgombea anakuwa ana timu yake ya kampeni na timu yake ya kampeni inahitaji kunywa maji, kulala, vyote hivi vina gharama. Sasa tukasema hivi tusifiche fiche mambo kwa sababu katika kifungu cha 22 tutakuta yale ambayo ni makatazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa napendekeza hapa nijaribu kushawishi Kamati yako ikubali kwamba katika mstari wa pili baada ya neno voters tufikirie kuingiza maneno including the cost of providing food, drink, entertainment, accommodation or other provisions by a candidate to members of his campaign team. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiit, hizi ni gharama halali kwa wagombea na hata kama mtu atakuja kusema baadaye kwamba, hawa watu walikuwa wamekusanywa na mgombea kwa madhumuni tofauti, kwa shabaha ambayo ipo katika kifungu cha 22 utasema hapana! Hizi ni gharama halali za mgombea na upende usipende kama unajua biashara hii lazima hawa wale, wanywe, walale na yote hayo ndiyo sehemu ya mahamasisho ya siasa. Mimi nadhani tukielewana na Serikali katika hili, tutakuwa tunakwenda vizuri sana, na hizi zitakuwa disclosed,
hakuna tatizo kabisa. (Makofi) 97

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU - SERA, URATIBU NA BUNGE (MHE. PHILIP S. MARMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Serikali isingekuwa na tatizo sana na kuipanua hiyo sub clause two, lakini hofu yetu ni kuingia katika mtego ambao Mahakama Kuu iliingilia kati na ukifuatilia sana lugha ya Mheshimiwa Chenge, ni kama sasa kufanya kifungu hiki kiwe open ended.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hili ndilo eneo ambalo lilitupeleka kwenye Mahakama Kuu, likatafsiriwa kama takrima, na ndiyo maana sisi tumeona kwamba ni bora zaidi tujinyime sana kwenda huko kwa sababu ukisoma pale, all funds used for promotional art groups for purposes of presentation of candidate’s voters shall be deemed to constitute election expenses. Hii yenyewe tungeiachia Mahakama ili baadaye itafsiri kuliko twende mbali na kutaja chakula, maji, malazi na kadhalika.

MWENYEKITI: Mheshimiwa mwenye hoja nimesahau! Mheshimiwa Chenge mimi nilifikiri kwamba wazungumze halafu utakuja tena.

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapana nataka nii-guide Serikali, naomba sana.

MWENYEKITI: Haya sawa!

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namuelewa Mheshimiwa Marmo, ni Mwanasheria mzoefu kama mimi pia. Napenda tu niisaidie Serikali hapa kama concern ni hiyo, tunachoweza kusema hapa including the cost of providing … tatata, hayo niliyoyasema which has been reasonably incurred by a candidate for members of his campaign team. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno hayo ni maneno mazuri sana mdomoni, lakini kwa nia ya kutekeleza Sheria hii tunayotaka kutunga yanaipunguzia makali. Nafikiri kwa vile madhumuni yetu ni kukubaliana, na kwa vile kwa maneno matamu sana ambayo nimeyasikia humu jioni hii kuhusu dhamira ya kujenga jamii ambayo inapata viongozi bila hila na jeuri ya fedha, labda ingekuwa vyema tukaweka limit ya hiyo chini ya kampeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtaweka kama Bunge maana yake mimi situngi Sheria, mimi kazi yangu Waheshimiwa Wabunge ni kuwashauri, kuwabembeleza na kuwashawishi. Kama nia yetu ni hiyo ambayo nimeisikia Mheshimiwa Jackson Makweta anasema, zile pillars tatu za askari, mtu mwenye akili na askari kama mimi nadhani tungeweka limit kwa sababu unaweza kuwa na timu ya kufanya kampeni, wapiga kura wote wa jimbo lako la uchaguzi.

(Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa napendekeza tuweke limit.

MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amechukua vizuri hoja niliyotaka kuisema kwamba ni lazima tutenganishe vitu viwili; cha kwanza ni campaign team ambayo inazunguka na mgombea na katika mazingira ya 98 majimbo ambayo ni makubwa ni lazima wasafiri, na watafika mahali ni lazima wale, walale na wanywe kama alivyosema Mheshimiwa Chenge. Kwa maana hiyo hoja ile bado inabaki valid.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nakubaliana na Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwamba hiyo campaign team ni nani? Kwa sababu hoja inaweza kuwa kweli kwamba hawa wote kwenye kijiji ndiyo campaign team yangu na ikarudi kwenye ile dhana. Kwa hiyo, nadhani tuweke tu hata katika regulations, campaign team ziweze kutajwa, tujue campaign teams specifically ni nani! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hofu ni huko Mahakamani baadaye hata kwenye petition huwezi ku-identify ni nani ambao unataka kuwatambulisha, na dhana ya Mahakama mimi naielewa vizuri tu kwamba, takrima ni ile ambayo unafika kwenye nyumba au kwenye kijiji, halafu wewe ndiye unawanunulia chakula, lakini si kuwalisha watu uliokuwa umewabeba.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dr. Slaa, kwa hiyo umesemaje sasa? Simama basi useme maana yake sijakusikia!

MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekubaliana na hoja ya Mheshimiwa Chenge, na tumekubaliana kwamba katika regulations Serikali ikubali kuspecify ile campaign team ni nani. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU- SERA, URATIBU NA BUNGE (MHE. PHILIP S. MARMO):
Mheshimiwa Mwenyekiti, scheme ambayo inaanza kuletwa na … (Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, naomba azungumze kwanza Mheshimiwa Chenge!

MHE. ANDREW J. CHENGE:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Ni kwa kutambua tatizo hilo ambalo Mheshimiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelisema ndiyo maana nilitumia maneno reasonably incurred kwa sababu tunasema ni Mahakama ambayo itadetermine kama kweli kiwango hicho kilikuwa ni halali kwa mazingira hayo!

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani wewe ukasema kwamba, kijiji kizima ndiyo umekigeuza kuwa campaign team itakuwa ni kichekesho ambacho hakijawahi kutokea duniani hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi eneo hili naomba sana tuwe makini, na Mahakama ilifika huko kwa malengo tofauti na Bunge hili lazima liendelee kutunga Sheria na Bunge hili lazima liendelee kuweka maadili mema katika shughuli hizi za Uchaguzi. Katika eneo hili hakuna Mbunge ambaye anaweza akabisha kwamba, hoja hii haina gharama! Ina gharama na ndiyo maana tunakubali zitangazwe, iwe sehemu ya gharama za mgombea kama election expenses! (Makofi)

Mimi hoja ni hiyo tu ambayo naiomba Serikali ilielewe hili, hatupanui lakini nigependa tujikite kwenye maneno reasonably incurred na yana-flow vizuri tu. Kwa waandishi wa Sheria hii ni attempt ya mtu ambaye ana uzoefu kidogo wa masuala haya. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU - SERA, URATIBU NA BUNGE (MHE. PHILIP S. MARMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuna hoja za aina mbili; mimi nilikuwa nashawishika na ile scheme aliyotaka kuileta Mbunge wa Karatu, Mheshimiwa Dr. Slaa kwamba ili twende kwa kina zaidi kuhusu eneo hili tusije tukawa kwenye mtego.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda ili kufahamu na kutafsiri timu hii ya kampeni. Timu hii ya kampeni maana yake ni nini? Na gharama zake ni nini? Pengine tuyahamishie kwenye kanuni na kanuni hizi zitaandaliwa kabla Bunge halijavunjwa. (Makofi)

MWENYEKITI:
Sawa lakini kwenye Sheria itakaaje sasa maana yake Kanuni zitategemea tumeandika nini katika hii main. Mheshimiwa Chenge!

MHE. ANDREW J. CHENGE:
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nakushukuru sana kwa kuliona hilo haraka kwa sababu ni lazima tujenge msingi katika Sheria yenyewe ili tuweze kufika kwenye regulations. Kwa hiyo, nilikuwa nategemea, maana na mimi nimeleta formulation ambayo nilitegemea sasa kama mtu anataka hapo aboreshe kwenye hayo maneno ambayo nimependekeza kuingiza.

MWENYEKITI:
Mheshimiwa Chenge, hebu yarudie tafadhali!

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nimesema baada ya neno voters.

MWENYEKITI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia kwenye amendment, clause kifungu b(ii) maana yake nakwenda kwamba, all funds used for promotional art groups for purpose of presentation of candidates to voters ndiyo inaingia hapo, si ndiyo hapo unaingilia!

Hebu yaseme sasa!

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo langu lilikuwa kwamba including the cost of providing food, drinks, accommodations, or transportation which has been reasonably incurred by a candidate for members of his campaign team. Inaweza ikawa have lakini Sheria ya tafsiri inasimamia hayo hakuna tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo mapendekezo yangu na kama sasa Serikali inataka kuja na ka-raider ku-deal na hii lazima iwe kwenye on a stand alone basis waanzishe kifungu kingine ili tuone dhana hiyo kama inalinda marekebisho ambayo anapendekeza katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana! (Makofi)

MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naunga mkono dhana ambayo ameleta Ndugu yangu Chenge, lakini akienda kwenye details kama chakula, malazi itabidi pia katika hiyo promotional art groups tuweke mambo yote hayo.

Kwa hiyo, mimi ningeshauri kwamba, pamoja na ile aliyosema kwamba reasonable tungeishia tu kwenye including expenses za campaign team! Sasa bila kwenda katika detail kama ni chakula au malazi, ulevi, pilau, pilipili tungeishia hapo naona ingeweza for the … sasa kama unataka kuipanua zaidi yule mtu wa regulation anaweza akafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tushawishike hivyo ili tumalize hii section. (Makofi)

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu kwamba ulifundishwa na Mheshimiwa Jackson Makwetta, na kwamba unapenda sana demokrasia lakini ninatafuta Kanuni ambayo inatuwezesha kuendeleza mjadala huu, bahati mbaya sijakubuhu katika hili. Lakini nafikiri kwamba formulation ambayo Mheshimiwa Chenge, ameileta na ambayo tulifikiri kwamba ingekuwa vizuri tukaifanyia kazi ingekuwa na utaratibu wake wa kuileta, hata hivyo inategemea tu mwongozo wako. Namheshimu sana Mheshimiwa Chenge, amenilea kielimu na pia kwa kuwa king’ang’anizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafikiri kwamba kwa heshima kabisa nimuombe Mheshimiwa Chenge, akubaliane na ilivyo sasa na kwa sababu Sheria inazaliwa na inakua, tutaibadilisha kwa kadri tunavyokwenda.

Naomba kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge kwamba mimi pamoja na kuwa Mbunge, lakini ni Jaji na naomba tuheshimu nyumba hii takatifu kwamba mwenzako anapozungumza wewe unyamaze tu! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nilikuwa nafikiria kwamba maelezo ya kusema costs reasonably incurred maneno yanayosema reasonably ni sawa sawa lakini kwa kweli bila kuweka cap. kwa hiyo, idadi tunachofanya ni kuvunja uamuzi wa Mahakama na Mahakama ya Rufani, kuhusiana na takrima, tunarudisha takrima tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba kama tunaweza kufanya hivyo, kukubaliana na alichofanya Mheshimiwa Chenge, lakini hapo hapo tukaweka tena provision ingawa naona kama Kanuni haziruhusu, ya kusema kwamba Waziri ataweka cap. kwenye hii idadi ya campaigning team. Kwa sababu unaweza kuwa na Wakurya wote wanakukampenia, jimbo zima sasa itakuwa balaa. Ahsante! (Makofi/Kicheko)

MHE. DR. WILLIBROD P. SLAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kumheshimu sana Attorney General ukirejea kifungu cha 55(11) ambapo Mbunge anayetaka kufanya, inaanzia kifungu cha 10 ambapo Mbunge ambaye anataka kufanya mabadiliko au marekebisho katika hoja yake anaweza kumuomba Spika afanye marekebisho au mabadiliko katika hoja hiyo wakati anawasilisha hoja yake bila kutoa taarifa. Kwa hiyo, tunapojadili hapa ambapo hoja imewasilishwa, mimi naamini kwamba ndiyo wakati ambao tunaweza kufanya hayo mabadiliko.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hasa katika hoja ambazo tunajadili kwa muda mfupi, leo tumewasilisha hoja hii Bungeni na hatukuwa na siku moja kabla ya kubadilisha kwa sababu hata schedules, hata hotuba yenyewe imetoka leo asubuhi. Kwa hiyo, mimi nafikiri kifungu hiki kinahalalisha mabadiliko yoyote ambayo Mbunge anasimama na tumeshafanya precedents tumeshafanya kitu cha namna hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili ili nisirudi tena, narudia kwa Mheshimiwa Attorney General, sisi ambao tumekaa kwenye Bunge tunaelewa kwamba, kuna gharama za campaign team bahati mbaya katika interpretation hakuna neno lolote linalotafsiri maana ya campaign team. Kwa hiyo, Rais anapokwenda kwenye campaign team hutegemei atasafiri peke yake, Mbunge anapozunguka hutegemei kwamba yuko peke yake, sasa Mahakama ambayo haitaelewa kwamba hiki ambacho mimi na timu yangu tunakula si takrima, nina mashaka pale katika tafsiri.

Ninategemea kwamba mimi nitakapoenda ninaenda kutoa fedha za mfukoni mwangu kuwapatia wale tunaowakuta kwenye eneo, tunawapa chakula na vinywaji, pale ndiyo takrima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilichotokea nyuma ni kwamba, tulibadilisha kilichoitwa African hospitality. Sisi tulitoa kama wageni tunapofika kwenye nyumba badala ya mwenyeji kutupatia chakula, huo ndiyo utata uliotokea. Kwa hiyo, mimi nafikiri hoja inaweza kubadilika hapa kwa kutumia kifungu ambacho nimekisema. (Makofi)

MWENYEKITI: Ipo Kanuni nyingine hapa kwamba, actually ilitakiwa yule mtoa hoja katika hili ingawa alitakiwa kuwa ametoa taarifa kwamba, nitafanya mabadiliko. Lakini spirit ya Sheria hii, kwanza tushukuru kwamba kimekuja kitabu kimoja, kama ingekuwa na lile rundo la mabadiliko yaliyokuwepo hata tungekuwa hatuonani, sana sana tungekuwa tunagongana tu, ndiyo maana nimeamua kuwa very slow kama tunakubaliana tunafanya, kama hatubaliani pia hatukubaliani. Kwa hiyo, nilifikiri tungeliangalia hivyo, infact hata ile campaign team, somewhere ingeingia kwenye definition ya Sheria. Mtoa hoja, aah, Mwanasheria Mkuu wa Seikali kwanza, au mmekubaliana! (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU - SERA, URATIBU NA BUNGE (MHE. PHILIP S. MARMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli wote tuna lengo moja na mimi nilifuatilia kwa karibu sana hoja ya Mheshimiwa Chenge, na baadaye hoja ya Mheshimiwa Cheyo. Napata picha kidogo sasa ya mwelekeo. Tukiunganisha hoja ya Mheshimiwa Chenge na Mheshimiwa Cheyo, tukaweka vizuri kwa lugha ya kisheria mimi nadhani tunaweza kupiga hatua.

MWENYEKITI: Sasa meanwhile watu wenu wangekuwa wanatunga maneno gani yanaweza kuingia hapo, tutarudia. Sasa tumefika pazuri tunaagiza kwamba haya maneno tunayotaka yakae hapo watu wenu wako hapa watusaidie yanaweza kuingiaje hapo.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU - SERA, URATIBU NA BUNGE (MHE. PHILIP S. MARMO): Mheshimiwa Mwenyekiti, tungemuomba Mheshimiwa Cheyo, hebu arudie pale sikumpata vizuri, alipokuwa anaboresha.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani kama tumefikia hivyo ni suala la kuchukua yale maneno ya Mheshimiwa Chenge, nasema Mheshimiwa Chenge, siyo Cheyo, majina yanafanana. Kwenye all funds used to promotional art groups for purposes of presentation of a candidate nimekosea, to voters including the costs of providing food, drinks, accommodation or transportation which are being reasonably incurred by a candidate for members of his campaign team shall be deemed to constitute election expenses. (Makofi)

MBUNGE FULANI:
Mwenyekiti, …

MWENYEKITI:
Mwenyekiti nini? Kwani ninyi mlileta hoja? (Makofi)

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi.

MWENYEKITI: Kifungu gani sasa?

MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Hapana! Ni ufafanuzi tu kwamba hiyo idadi ya campaign team ni vizuri itazamwe na iwekwe wazi, mtu anaweza kuwa ana campaign team kwenye kila kata, nadhani tuwe conscious kidogo, nakubaliana lakini kuiacha wazi tu inaweza kutuletea matatizo.

MWENYEKITI: Si ndiyo maana tulikubaliana na definition ya campaign team iwepo na ndani ya definition inaweza ikaeleza who are these people. Kwa hiyo, tunakubaliana kwamba kwenye definition tutaongeza campaign team na katika campaign team definition ndiyo itasema haya anayosema Mheshimiwa Shellukindo lakini maneno mengine ni kama yalivyowekwa.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko yake)
 
MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi.
MWENYEKITI: Kifungu gani sasa?
MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO: Hapana! Ni ufafanuzi tu kwamba hiyo idadi
ya campaign team ni vizuri itazamwe na iwekwe wazi, mtu anaweza kuwa ana campaign team
kwenye kila kata, nadhani tuwe conscious kidogo, nakubaliana lakini kuiacha wazi tu inaweza
kutuletea matatizo.

MWENYEKITI: Si ndiyo maana tulikubaliana na definition ya campaign team iwepo na
ndani ya definition inaweza ikaeleza who are these people. Kwa hiyo, tunakubaliana kwamba
kwenye definition tutaongeza campaign team na katika campaign team definition ndiyo itasema
haya anayosema Mheshimiwa Shellukindo lakini maneno mengine ni kama yalivyowekwa.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Bunge Zima pamoja na mabadiliko
yake).

Mimi sioni ni kwa namna gani hoja za Mh Shellukindo na Mh Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge zima kama nilivyoziquote hapo juu zizae maelezo ya watu wanaotakiwa ku - approve campaign team kama nilivyoonesha (in green) hapa chini:
7. (3) For the purposes of subsection (2), "campaign team"
means a group of' persons formed by a candidate in the
nomination process or a contested election for purpose' of
presenting or assisting that candidate in the election campaigns,
who have been approved-
(a) in the case of a Presidential candidate, by the
Registrar;
(b) in the case of a Member of Parliament, by the
District Administrative Secretary; and
(c) in the case of a Councilor, by the Ward Executive
Officer.
 
Buchanan,Approval itoke wapi sasa? Ujue Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi haina maofisa wake katika ngazi yoyote ile ya chini kama mkoa, wilaya, jimbo au kata. Tumwamini AG wetu. Ni mtu makini sana ingawa sio malaika.
 
Maelezo ya AG yamejitosheleza mengine yatabaki kuwa kazi za wanasiasa.
Bravo AG!
Si lazima uwe mwanasheria ili uweze kutunga sheria, lakini ni lazima uwe mwanasheria ili uweze kuandika sheria.
 
Huu ni utaratibu uliozoeleka wa kutekeleza maelekezo ya Bunge katika Mazingira ambayo Bunge linakaa kama Kamati ya Bunge Zima................... Endapo Waziri ataafiki mapendekezo ya Mbunge yeyote,atamjulisha Mwenyekiti na Mwenyekiti akiridhia atamuelekeza Mbunge aliyetoa mapendekezo asome maelezo anayotaka yaingizwe kwenye Muswada. Ikiwa Mbunge aliyependekeza marekebisho hayo hana maelezo mahsusi, Mwenyekiti atamuagiza Katibu wa Bunge ashirikiane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuweka maneno au Kifungu kinachoweka masharti yenye maudhui aliyopendekeza Mbunge. Mwenyekiti atawahoji Wabunge kama mapendekezo yakubaliwe au la, wakikubali basi waandishi watakwenda kuandika kifungu kwa namna ambayo inatafsiri nia na uamuzi wa Bunge.

Mbona hawasemi kama baada ya kuingiza kifungu hicho mwenyekiti aliwahoji wabunge kama wanakubali?
 
Serikali ya CCM wanajua watanzania wote ni majuha kwa hiyo wanafanya watakavyo wakijua hakuna wa kuhoji na hata wale wanao hoji hawana la kuifanya serikali ya CCM ya kifisadi.

Ninacho kiona mimi tuendelee kuhimizana kuelimisha umma, pindi tukiwa na wananchi wanao elewa basi twaweza kufanya lolote lakini kwa sasa ni ngumu.

Angalia Thailand, wananchi wana maamuzi dhidi ya serikali na hakuna anayeogopa risasi. Kwa hiyo hata hapa TZ itafika wakakti wananchi (watoto na wajukuu) zetu hawata ogopa risasi na hapo ndo tutapata maendeleo ya kweli.

Vizee vya CCM vina fikiri raha ya maisha inakwisha kwa kuwa vimezeeka lakini kumbe raha hii ipo milele na wanaokwisha ni viumbe hai.

Mwangalie mtu kama chenge.....kwanza mgonjwa...je hizo pesa atafanyia nini akisha kufa??
 
Maelezo ya AG yamejitosheleza mengine yatabaki kuwa kazi za wanasiasa.
Bravo AG!
Si lazima uwe mwanasheria ili uweze kutunga sheria, lakini ni lazima uwe mwanasheria ili uweze kuandika sheria.

Kwa mawazo kama yako.....ndo maana Tanzania ni shamba la bibi
 
Mbona hawasemi kama baada ya kuingiza kifungu hicho mwenyekiti aliwahoji wabunge kama wanakubali?

Mkuu wameishasema mswada unarudishwa bungeni na aliyeongeza kifungu hicho ni Phillip kwa hiyo Dr. Slaa kama kawaida yake ameisha piga bao.
 
Hivi katika waheshimiwa wote hawa kuna anayeweza kuongea kiswahili?

Na itakuwaje mapendekezo ya wabunge binafsi yaingizwe kinyemela kwa vile tu yaliwahi kuongelewa bungeni? Mimi nilidhani baada ya majadiliano haya, hao waliokubuhu na uandishi wa sheria wangeandika halafu kurudisha bungeni ili waheshimiwa waafik kama imekidhi waliyoyataka. Hata kwenye vikao vya harusi, miniti zinasomwa na katibu kabla ya kuhalalishwa kama kumbukumbu sahihi ya yaliyozungumzwa.

Amandla......
 
Back
Top Bottom