GE2025 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetengua uteuzi Mgombea Urais wa ADC (Wilson Malumbe) kwenye kuwania Urais wa Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetengua uteuzi Mgombea Urais wa ADC (Wilson Malumbe) kwenye kuwania Urais wa Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Screenshot 2025-08-27 092911.jpg
Maktaba Media imepata taarifa kuwa Mgombea Urais kupitia Chama Cha Alliance Democratic For Change (ADC) Ndg. Wilson Malumbe huenda akaondolewa kwenye mchakato wa Urais wa Uchaguzi Mkuu 2025 baada ya Ofisi ya Msajili wa Siasa kubainisha kasoro za kupatikana kwa Mgombea huyo.

Haya yanajiri wiki kadhaa baada ya kada wa chama hicho na aliyewahi kuwa Mbunge wa Mwibara mkoani Mara, Mutamwega Mgaywa kukata rufaa kwenda Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, kupinga mchakato uliotumika kumpata Malumbe.

Mgaywa alidai alichukua uamuzi huo akitaka haki itendeke dhidi ya kitendo alichodai cha kihuni kilichofanywa na uongozi wa chama hicho kumuengua kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kugombea urais wa Tanzania, kwa kunyofoa baadhi ya taarifa zake muhimu zilizojazwa kwa ufasaha na kuwekwa nyingine asizozitambua ili kumpa nafasi Malumbe.

Haya yanajiri; Siku moja baada ya Mgombea mwingine wa Urais, Luhaga Mpina nae kuenguliwa kwa kile kilichoelezwa kukosa sifa za kugombea nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba (kanuni) za ACT Wazalendo.

CHANZO: MAKTABAMEDIATZ
==================================

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetengua uteuzi wa wagombea wawili wa urais wa Tanzania, Luhaga Mpina wa ACT-Wazalendo na Wilson Elias wa ADC, kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za kisheria katika mchakato wa uteuzi ndani ya vyama vyao.

Uamuzi huo umetolewa usiku wa jana Jumanne, Agosti 26, 2025 wakati leo Jumatano ni siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi kwa nafasi za Rais, Makamu wa Rais, wabunge na madiwani, kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni kesho, kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Agosti 26, 2025 usiku na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu ya Uraia, Abuu Kimario, imeelezwa wagombea hao wamekiuka masharti ya Kifungu cha 4(5)(a) na (b) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 baada ya kubainika kuwa uteuzi wao haukufuata misingi ya sheria, katiba na kanuni za vyama vyao.

“Mchakato wa uteuzi wa ndani ya vyama hivyo uligubikwa na utata na haukuzingatia sheria, jambo ambalo linahatarisha utawala wa sheria, amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa,” amesema Kimario.

Ofisi ya Msajili imesema uamuzi huo umetolewa baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa na pande husika na kubaini kasoro kubwa katika namna wagombea hao walivyochaguliwa ndani ya vyama vyao.

Chanzo: Mwanachi
 
Kuna tatizo hapa na hi kichezo ya kisiasa Tanzania...

Hivi huyu msajili ana mamlaka ya uteuzi au ni tume ya uchaguzi? Yeye kuwaengua anahusikaje? Bandugu nielewesheni... hayo mamlaka kayatoa wapi ndani ya katiba yetu ya mwaka 1977? Ni kipengele gani kimempa hayo mamlaka? Mtu akitaka kuyapinga kwa kumkatia rufaa anafanyaje? Huko kwa msajili kuna kitengo cha rufaa au ni mpaka mahakama kuu?
 
Ila haya mambo bwana Yan mtu ambaye alikuwa analalamikiwa kuteuliwa Kwa ujanjajanja ndo hyo anapetA 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 hii ndo bongo had kufikia oktoba atakuwa amebaki 1 tu na ndo Kaz itakuwa imekwisha
 
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetengua uteuzi wa Mgombea Urais kupitia Chama Cha Alliance Democratic For Change (ADC), Wilson Elias kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za Kisheria katika mchakato wa uteuzi ndani ya chama.

Taarifa iliyotolewa na Agosti 26, 2025 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu ya Uraia, Abuu Kimario imeelezwa Wilson amekiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 baada ya kubainika kuwa uteuzi wake haukufuata misingi ya Sheria, Katiba na Kanuni za chama.

Ikumbukwe leo Agosti 27, 2025 ni siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi kwa nafasi za Rais, Makamu wa Rais, Wabunge na Madiwani, kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni Agosti 28, 2025 kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
 
Kuna tatizo hapa na hi kichezo ya kisiasa Tanzania...

Hivi huyu msajili ana mamlaka ya uteuzi au ni tume ya uchaguzi? Yeye kuwaengua anahusikaje? Bandugu nielewesheni... hayo mamlaka kayatoa wapi ndani ya katiba yetu ya mwaka 1977? Ni kipengele gani kimempa hayo mamlaka? Mtu akitaka kuyapinga kwa kumkatia rufaa anafanyaje? Huko kwa msajili kuna kitengo cha rufaa au ni mpaka mahakama kuu?
My question, precisely!
 
Kwani tume ilinunua magari mangapi...!

Isije kuwa idadi ya magari ilikuwa ndogo wanabalance.
 
Back
Top Bottom