Ofisi ya bunge yapokea rasmi Nyumba mpya ya Spika

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
OFISI YA BUNGE YAPOKEA RASMI NYUMBA MPYA YA SPIKA MJINI DODOMA LEO
1+(1).JPG

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas Wambura kabla ya makabidhiano rasmi ya jengo la nyumba atakayokuwa anatumia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.
3+(1).JPG

Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction Company ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban Mwatawala (kulia) akitoa maelezo ya ujumla kabla ya kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya Bunge katika jengo hilo. Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha Bw. Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na Teknolojia ya Mawasiliano wa Bunge Bw. Siegfied Kuwite, na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John Joel.
6+(1).JPG

Bwana Mwatawala akimkabidhi Msanifu Majengo M. F. M Msangi (kulia) anayewakilisha Wakala wa Majengo ya Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa Mradi huu.
2+(1).JPG

Muonekano wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo litakuwa makazi ya Spika yeyote atakayeliongoza Bunge la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 na limegharimu takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika wa Bunge Dodoma.
7+(1).JPG

Mlango wa mbele wa jengo.
8+(1).JPG

Ngazi ndani ya jengo ambalo lina vyumba vinne vya kulala, sehemu ya mapumziko, sehemu ya chakula, maktaba na jiko.
9+(1).JPG

Upande wa nyuma wa jengo.

Chanzo:Michuzi

 
1.5bn Tshs???! No way, this figure must be somehow manipulated for political reasons or it was the original contract sum. Now it stand at over 2.2bn.
 
Sitta alipigania sana ujenzi wa nyumba hii sambamba na ile ofisi yake jimboni Urambo. Ushauri kwa mama Makinda, ukistaafu Uspika jiuuzie hii nyumba. Spika atakayefuata tutamjengea nyingine itakayolingana na hadhi yake kipindi hicho.
 
Sio tu nchi maskini ni nchi ya wajinga walio wengi + maskini wa kufikiri hv tangia 1961 mpaka leo spika alikuwa nakaa wapi na hii nyumba ni kwa ajili ya akiwa kikao kwa vikao vingi vya kamati vinafanyika Dar na huko ajengewe nyumba tena kidumu chama cha magamba
 
The ides of the ruling class (including those using poor tax payers money to build such a white elephant project) are the ruling ideas. Imagine wabunge wasiokatwa kodi kwenye mishahara yao wame contribute nini kwenye ujenzi wa Jumba hili?????
 
Kwa nchi ambayo rais wake anakaribia kuzungukia karibu kila nchi hapa duniani akiwa na bakuli la kuombea misaada, ni aibu na tusi kubwa kwa wananchi kujenga jengo la kuishi spika lenye thamani ya sh. 1.5 bilioni.
 
nakumbuka na ile ya gavana wa benki kuu..hii nchi majizi ndio yanathaminiwa nakutukuzwa kama wafalme,alafu madaktari wakifanya mgomo kwa ukosefu wa vitendea kazi wapumbavu hawachelewi kusema wametumwa na chadema.inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom