Spika mpya amtimua Nancy Pelosi wa Democrats kutoka ofisi za Bunge

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,821
Nancy Pelosi na naibu wake wa muda mrefu Steny Hoyer wameamriwa kuondoka katika maeneo yao ya kazi katika Bunge la Marekani na kaimu Spika wa Bunge Patrick McHenry.

Wote wawili waliambiwa kufuli kwenye milango ya ofisi zao "zitabadilishwa tena" siku ya Jumatano.

Ufurushaji huo umewadia baada ya Kevin McCarthy kufurushwa kutoka wadhifa wa spika siku ya Jumanne na Bw McHenry, mwaminifu mkuu, akateuliwa kushika wadhifa huo kwa muda.

Bi Pelosi, ambaye kwa sasa hayuko Washington, alikosoa uamuzi huo kama "kujitenga sana na utamaduni".

Ofisi yake itakabidhiwa kwa Bw McCarthy, mbunge wa chama cha Republican Garret Graves alitangaza Jumatano, akisema kwamba inapaswa kuwa ya "spika aliyetangulia".

"Kwa kuwa sasa yeye na wanademokrasia wengine wamesababisha kuwepo kwa spika aliyetangulia, amejiondoa kwenye ofisi hiyo ... huo ulikuwa uamuzi ambao Democrats na Spika Pelosi walifanya katika kumpa McCarthy ofisi hiyo," alisema, kulingana na Axios.

Bi Pelosi alitoa taarifa Jumanne akipinga uamuzi huo.

"Pamoja na maamuzi yote muhimu ambayo Uongozi mpya wa Republican lazima ushughulikie, ambayo sote tunasubiri kwa hamu, moja ya hatua za kwanza zilizochukuliwa na Spika mpya ilikuwa kuniamuru niondoke mara moja ofisi yangu huko Capitol," alisema.

"Ni jambo la kusikitisha, kwa sababu niko California kuomboleza kumpoteza rafiki yangu mpendwa Dianne Feinstein, siwezi kuondoa vitu vyangu kwa wakati huu uliowekwa."

Bi Feinstein, seneta wa California ambaye alihudumu kwa zaidi ya miongo mitatu, alifariki akiwa na umri wa miaka 90 wiki iliyopita. Mazishi yake yatafanyika Alhamisi hii.

Ingawa ni nadra kwa wanachama wa Congress ambao hawako katika majukumu ya uongozi kuwa na afisi katika jengo la Capitol, Bi Pelosi na Bw Hoyer walikuwa na kile kinachoweza kuitwa ‘maficho’ kama Spika wa zamani na Kiongozi wa Wengi.

Bi Pelosi alibainisha katika taarifa yake kwamba, kulingana na utamaduni, alimpa mtangulizi wake wa Republican afisi wakati akiwa Spika.

Wanademokrasia wote, hata hivyo, wataendelea kuwa katika nafasi zao za kazi za kawaida katika majengo ya ofisi za Bunge.

Chanzo: BBC
 
Ndiyo maana huwa mnapotezwa kwenye mikataba.

Habari fupi kama hiyo umeshindwa kuielewa jee ukipewa Mkataba wenye kurasa 500 ndiyo utaweza???

Hata Dp World waliwapoteza kwenye huo uzembe wenu!!
Wazee wa kulalamikia Wazungu 😆😆
 
Back
Top Bottom