Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Mods naomba hii msiifute wala kuichanganya na Uzi mwingine

ROMA AMEFUNGUKA ILA SIJAMUELEWA VIZURI.....

By:Mathias Raymond Nyakapala

Wakuu nawasalimu kwa jina la aliyejuu yeye jana,leo na hata milele atupaye pumzi na hapangiwi kuiondoa...........

Naandika haya nikitokea katikati ya Nchi yetu TANZANIA,nikitokea katikati ya KANDA YA KATI,nikitokea katikati ya MKOA WA DODOMA yaani DODOMA MJINI..........nimesikiliza sana nyimbo ya Msanii ambaye hata mimi nampenda na kuangalia ile Video yake yote ni vizuri sana na labda kaongea yaliyompasa kuongea ambayo wengi tulisubiri kwa muda mrefu sasa.....NIKILI BINAFSI SIJAMUELEWA KABISA LENGO LAKE NI NINI KWASASA KAMA KWELI ALIWAHI KUTEKWA?

Siogopi kuwa tofauti na wengi ili mradi ninachokisema hakivunji sheria,hakiharibu utaratibu au Maadili ya uongozi kwenye jamii yetu pia ikiwa ninachokisema ndo ukweli wangu kutoka Moyoni itakuwa nimejitendea haki na nimewatendea haki wote wanaoniamini na wale wafuasi wangu pia itakuwa nimetimiza haki yangu ya KIKATIBA(uhuru wa kutoa mawazo,na kujieleza)ninachokisema hapa sio msimamo wa Taasisi yoyote ila ni Mawazo yangu kama MwanaHip Hop na mtu ninayependa Haki,Ukweli na Uwazi.

KWANINI SIJAMUELEWA ROMA....(kwa uelewa wangu),Tofauti na kuwa amechelewa sana kusema haya ila pia kuna ziada....

1.HIP HOP-Ni utamaduni ulioenea sana duniani ambao umebeba mambo mengi na mafundisho makubwa sana kwenye jamii yetu,Roma ni MC moja ya nguzo za Hip Hop na kimsingi yeye na wengine nategemea kuwa Watakuwa mstali wa mbele KUSEMA UKWELI NA HATA KUUFIA ili mradi kinachotoka kwenye kinywa chake/chao kiwe ni KWELI TUPU mfano:-
Msanii Tupac amewahi kusema nanukuu

"When I speak I wana truth came out no matter..............................I wana change the World "

mwisho wa kunukuu

lakini pia bila kujali kitatokea nini kesho au baada ya kusema hayo ili mradi kitaleta dhana ya Mabadiliko kwenye jamii husika,siku Roma alipoachiwa nilitegemea afanye Dunia ijue kama huku Tanzania tumefikia mahala wasanii wanatekwa,wanapigwa au hata kudharirishwa lakini pia nilitegemea aseme nani alimteka kama amemjua au kama hajamjua basi atuambie watu wa Ulimwengu wa Hip Hop(wasanii na Mashabiki)ili tuendelee na Maombi mpaka ajulikane,sijasema alichoimba hakifai ila najiuliza ameimba kwaajili ya UKWELI UTOKE NJE AU KAIMBA ILI ARUDI KWENYE BIASHARA KAMA KAWAIDA(PUBLICITY)?NB:nawaza kwa sauti

2.GHARAMA ZA KUSEMA UKWELI NA MATOKEO YAKE KWENYE JAMII
-Jamii yetu kama zilivyo jamii za Kimataifa tupo kwenye WAKATI WA MABADILIKO haiepukiki hata kidogo au hatuwezi kujitenga tukasema sisi hatutaki hayo mambo.Tunashuhudia Nchi za wenzetu wakifanya Mabadiliko makubwa ya KIUCHUMI,KIJAMII NA KISIASA maana yake ukiona mwenzio ananyolewa zako tia Maji
.........for the new change sacrifice must made......
-Inawezekana wakati amepatwa na janga la kupotea Roma baada ya kupatikana angesema ukweli palepale angefanya Tanzania tuingie kwenye Mabadiliko makubwa sana kwani kuna wakati jamii inaweza kupata mabadiliko kwasababu ya Mtu mmoja(jasiri na mwenye Imani ya kweli na asiye na chembe ya uoga kuhusu kesho) tofauti na alivyosema Mambo yapo polisi akisema ataharibu upelelezi(sijui hadi leo upelelezi haujakamilika?),bad enough siku alikuwa anafanyiwa mahojiano EAT.....kipindi cha Usiku alisema kama angesema ukweli eti kuna wakati hata hizo Show za milioni TANO labda asingekuwa anapata inawezekana ndo angeishia hapo.......sasa najiuliza maswali kadhaa

a)waliomteka(kama ni kweli)ndo hao wanaompakaga Show?

b)Anawafahamu maana tulifanya maandamano mioyoni ya kumtaka aachiwe akiwa mzima/hai,kwenye mitandao tulisema sana?

c)Show na biashara zake ni muhimu kuliko anachokiimba siku zote kwenye nyimbo zake,anasemaga akafungwe au akatupwe kwenye daraja la...............ni sehemu ya biashara tu au anamaanishaga kitu kweli huyu?

KRS ONE anasema nanukuu
"think about children we bring up........"

Wapo wanahip hop wanaokuwa na kujifunza kwetu kama sisi tulivyojifunza kwa Kaka na Baba zetu sasa kama tutakuwa wakwanza kuwaza watoto wetu,familia zetu na Material things hatutafanya mabadiliko yoyote kwenye jamii zetu hata siku moja............

3.ROMA TEMBEA JUU YA MANENO YAKO
-Nikiwa ni mtu ambaye naamini kwenye Hip Hop ndo chanzo cha Ukombozi kwenye jamii nyingi duniani,natamani watu wote mtembee juu ya maneno yenu kama Ukiimba kitu uwe unamaanisha kweli mfano mzuri ni Bob Marley alikuwa anasema mambo ambayo anaweka msimamo kwa gharama ya Uhai wake ndo maana mpaka leo Tunamkumbuka na Kumheshimu sana,Waliofia ukweli na wanaheshimika wapo wengi kama wanaharakati Malcom X,Martin Luther.......n.k(dunia inawakumbuka na kuwaenzi kwa heshima)

Roma na Wasanii wengine lazima mjue Watawala wanaweza kubadilika kila msimu na watakumbukwa kwa Mabaya yao na Mazuri yao lakini kwenye HIP HOP HAUTAKUMBUKWA KWA KUWA MWOGA NA MJINGA KISA BIASHARA,unaweza kuwa tajiri sana lakini utajiri wako/biashara yako ina maana gani kama hautendi yale ya KWELI/HAKI,haufanyi yaliyo kwenye moyo wako?

-sikiliza nyimbo za Ant-Vitus,CO2,KRS ONE,FUGEE,SUGU,MAR-P na wengine wengi wanasema yanayowajaza na kuisaidia Jamii kwa ujumla.

-Mwisho nyimbo ni nzuri sana but Speak louder than you do I know you can!

KIJANA FIA UNACHOKIAMINI USIWE MTUMWA WA BIASHARA NA KUTENGENEZA PUBLICITY

Sent using Jamii Forums mobile app
Kauliza ivi je akifa kishujaa leo ....utaenda kusaidia familia yake na mama yake????
 
"Mungu wa Paulo ndio Mungu wa Daudi na ndio Mungu ya John wayahaudi wanaemuita Yohana."...
 
"Kutekana tekana ni mambo ya kishamba weka silaha chini tubishane kwa hoja" Nakwenda Zimbabwe
 
Wimbo ni mbaya, yaani hauwezi kumuingizia hela. Kwa sababu 2015 kila mwananchi alihitaji mabadiliko, sasa yeye kaibuka ni li nyimbo la kinafiki. Maisha kwake naamni yatazidi kuwa magumu maana anachezea system ya wateja wake. Ki ukweli sasa namchukia sana huyu kijana mnafiki
Naona umejitaidi kujitokeza sijawaona kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"....weka silaha chini tubishane kwa hoja...."
Sio kwa hizi undeveloping countries.
Hii situation labda kwenye nchi ambazo ni highly civilized ambapo watakuwa ni First World Countries
 
Lakini bado swali ni lile lile,kwa nini ROMA MKATOLIKI Atekwe???ili iwe nini? Yes ni maharufu lakini kwa umaarufu gani sana??? Kwa siasa au upinzani au kutaka chama cha CCM au chama cha CHADEMA au kichukua Wake za Watu???,sipati jibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Roma inasadikika ile ishu ya vyet na ile kuvamia clous jamaa alikuwa anataka kuachia bonge la nyimbo wakamuwahi mapema ila naamini kama ameweza kupata ujasiri wa hii ana weza akaunganisha na ile aliyotaka kutoa au akapotezea maana ililenga sana kipindi kile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rudia tena kusikiliza, kuna sehemu kasema hakuona nyota kwenye shoulder japo anajua ni solider... Ulikuja mwenyewe au ulipewa order

Mungu wa Paulo ama John mnayemuita Yohana hahahahaha katisha sana Roma.. Kuna sehemu pia kasema alipokuwa hakujua kama ni saa nne ama Saanane.... Wapi Ben wa Saanane
Ukisoma huo mstari Wa mwisho
Kwa mawazo yangu
Inawezekana Roma alikuwa anasifiwa sana na mkuru mbele ya mtoto,hvyo mtoto akaona wivu na kuamua kutaka kumpoteza kabisa ila mkuru akaweka ngumu.

We kakupa ambulence,mi kanijengea.....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaelewa mkuu! Zimbabwe ametumia kama kiitikio lkn hakija beba maana yeyote,nilipokuwa jkt miaka kadhaa iliyopita tuliimba sana kwenye mchakamchaka hiko kiitikio cha Zimbabwe.
Zimbabwe hutumika kama
Dr au mwalimu ndo maana ikiona katika video utawaona.
Kama siyo mtunzi au mwanafasihi ningumu kuelewa.
Wale Wa jkt wanajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom