Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Kama umeshasikiliza nyimbo mpya ya Roma inayoitwa Zimbabwe hebu tuchambulie japo mstari mmoja uliouelewa.

Karibuni wanafasihi
 
Hujaelewa mkuu! Zimbabwe ametumia kama kiitikio lkn hakija beba maana yeyote,nilipokuwa jkt miaka kadhaa iliyopita tuliimba sana kwenye mchakamchaka hiko kiitikio cha Zimbabwe.

Wewe ndiyo hujaelewa tafsida iliyofichwa humo.
Na yeye alitaka uelewe hivyo sababu imewekwa kwa wanaona mbali.
Tazama picha na matendo huku ukisikiliza maneno utapata jibu
 
kitu pekee ambacho nimekuwa nikimuombea uyu dogo ni kwamba, awe alitekwa lakini walimhurumia kumtatua rinda. kama atakuwa amepoteza rinda hapo sasa, sijui atafanyeje. ila kwa trauma ile aliyokuwa nayo wiki lile, aisee kuna siku Mungu atawalipa watesi wake tu.
Mkuu,kwani hata kama alitatuliwa rinda ndio anajiunga na timu moja kwa moja..? Jibu ni hapana.


Hiki kitu cha kusema kwamba jamaa katatuliwa rinda hakiniingii kichwani na siamini kamwe.
 
Exactly mkuu. Kuna maana kubwa sana kwenye hili neno "Nakwenda Zimbabwe"
Hivi huko si ndo kwa yule jamaa mbabe ambaye anazeekea Madarakani. Kwenye video naona anaenda Zimbabwe na raia kutoka kila sekta wanamfuata. Hili dongo la kisomi sana.
Zimbabwe kwenye umasikini wa kutisha.
 
Wewe ndiyo hujaelewa tafsida iliyofichwa humo.
Na yeye alitaka uelewe hivyo sababu imewekwa kwa wanaona mbali.
Tazama picha na matendo huku ukisikiliza maneno utapata jibu
Sawa mkuu! Kila mtu ana upeo wake wa kutafsiri jambo
 
Hujaelewa mkuu! Zimbabwe ametumia kama kiitikio lkn hakija beba maana yeyote,nilipokuwa jkt miaka kadhaa iliyopita tuliimba sana kwenye mchakamchaka hiko kiitikio cha Zimbabwe.
Mkuu kwa video inavyoongea inasapoti kabsa kwenda Zimbabwe. watu wote wanaacha shughuli zao wanamfuata nyuma mchizi, haijalishi umuhimu wa shughuli yenyewe
 
Ukiusikiliza wimbo kwa umakini utapata angalau kapicha ya kisanga alichopitia Roma mkatoliki.

Ni mkasa uliomtisha sana,nafikiri huenda alijua ndio mwisho wake wamaisha kufungwa mikoni na kufumbwa macho kwa siku kdhaa huku ukiteswa bila kujua hatma yako ni jambo lakuogofya na kutisha

Familia ambayo anaamini angeiacha wapweke ndicho kitu pekee kilichafanya asiseme ukweli.
 
Kiitikio kina maanisha nchi inaelekea Zimbabwe sasa zimbombo (maana yake kazi ipo) kwa maoni yangu lkn.

So kiuchumi tunaelekea Zimbabwe, kisiasa Zimbabwe, kijamii Zimbabwe. Hapa tunaunganisha na ile Mungu wa Daudi ndio Mungu wa Paulo na John tunaemuhta Yohana. Hawa lao moja maana Mungu wao mmoja.

Akili pia bila shaka ni moja u cant separate those three people
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom