Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Mimi sioni cha AJABU alichoimba hapo!!
Binafsi sikupenda kabisa kitu alichofanyiwa siku zilizopita.

Lakini tujiulize kweli yale yamepita na MWENYEZI akamsaidia karudi MZIMA.

Sasa nyimbo hii ni NINI,wote tunajua aliteswa hiyo nyimbo haina maudhui anaruka mara huku mara huko,

Utasikia hapa watu wataleta hadithi nyinbo hii INA UJUMBE MZITO MPAKA UTULIZE KICHWA SANA KUIELEWA.
Huu wimbo wenye upeo mdogo wa kufikiri hawawezi kumwelewa Roma.
Nimefurahi kuona Roma amepata nguvu tena ya kurudi katika fani Mungu akulinde and keep strong .. [HASHTAG]#SikaiKimya[/HASHTAG]
✈️
 
View attachment 563143View attachment 563144 huyu dada kapodolewa vizuri,,wengine sijui mnapakwa mpaka mnakuwa kama masanamu na mnapoteza sura zenu halisi,,mfano hamisa mobeto na mama yake huwa hawapendezei kabisa make up zao,kuna gigy money huyu anajipodoaga anakuwa sanamu sanamu,,hebu igeni kwa mrs roma kapendeza kajipodoa kidogo tu na sio kukandikwa makeup kama nyumba ya udongo bwana ,
Nimemaliza

ha we jamaa kweli bado ipo hata siuliziii
 
Mimi sioni cha AJABU alichoimba hapo!!
Binafsi sikupenda kabisa kitu alichofanyiwa siku zilizopita.

Lakini tujiulize kweli yale yamepita na MWENYEZI akamsaidia karudi MZIMA.

Sasa nyimbo hii ni NINI,wote tunajua aliteswa hiyo nyimbo haina maudhui anaruka mara huku mara huko,

Utasikia hapa watu wataleta hadithi nyinbo hii INA UJUMBE MZITO MPAKA UTULIZE KICHWA SANA KUIELEWA.
Unaijua kazi ya muziki?
Au unadhani kazi ya muziki ni kujaza kumbi za disko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MISUKOSUKO IMEMPA UJASIRI WA KUINGIA FRONT!
nimependa idea yao!
safiiii!
MUME AKIWA AINA YA ROMA MKE UKIBAKI NYUMA NYUMA UNASUBIRI KUKANDA VISHETI LAZIMA ABOREKE!
hapa sasa wanaenda sawa!
 
bado naendelea kuisikiliza labda nitaelewa alichokizungumzia kwenye wimbo wake
 
Mimi sioni cha AJABU alichoimba hapo!!
Binafsi sikupenda kabisa kitu alichofanyiwa siku zilizopita.

Lakini tujiulize kweli yale yamepita na MWENYEZI akamsaidia karudi MZIMA.

Sasa nyimbo hii ni NINI,wote tunajua aliteswa hiyo nyimbo haina maudhui anaruka mara huku mara huko,

Utasikia hapa watu wataleta hadithi nyinbo hii INA UJUMBE MZITO MPAKA UTULIZE KICHWA SANA KUIELEWA.


Tena wewe ni mmoja wa wanaliingizia hasara TAIFA hili kwa kutotumia akili kama mwenzako BASHITE lakini Mungu mwacheni aitwe Mungu
 
Mods naomba hii msiifute wala kuichanganya na Uzi mwingine

ROMA AMEFUNGUKA ILA SIJAMUELEWA VIZURI.....

By:Mathias Raymond Nyakapala

Wakuu nawasalimu kwa jina la aliyejuu yeye jana,leo na hata milele atupaye pumzi na hapangiwi kuiondoa...........

Naandika haya nikitokea katikati ya Nchi yetu TANZANIA,nikitokea katikati ya KANDA YA KATI,nikitokea katikati ya MKOA WA DODOMA yaani DODOMA MJINI..........nimesikiliza sana nyimbo ya Msanii ambaye hata mimi nampenda na kuangalia ile Video yake yote ni vizuri sana na labda kaongea yaliyompasa kuongea ambayo wengi tulisubiri kwa muda mrefu sasa.....NIKILI BINAFSI SIJAMUELEWA KABISA LENGO LAKE NI NINI KWASASA KAMA KWELI ALIWAHI KUTEKWA?

Siogopi kuwa tofauti na wengi ili mradi ninachokisema hakivunji sheria,hakiharibu utaratibu au Maadili ya uongozi kwenye jamii yetu pia ikiwa ninachokisema ndo ukweli wangu kutoka Moyoni itakuwa nimejitendea haki na nimewatendea haki wote wanaoniamini na wale wafuasi wangu pia itakuwa nimetimiza haki yangu ya KIKATIBA(uhuru wa kutoa mawazo,na kujieleza)ninachokisema hapa sio msimamo wa Taasisi yoyote ila ni Mawazo yangu kama MwanaHip Hop na mtu ninayependa Haki,Ukweli na Uwazi.

KWANINI SIJAMUELEWA ROMA....(kwa uelewa wangu),Tofauti na kuwa amechelewa sana kusema haya ila pia kuna ziada....

1.HIP HOP-Ni utamaduni ulioenea sana duniani ambao umebeba mambo mengi na mafundisho makubwa sana kwenye jamii yetu,Roma ni MC moja ya nguzo za Hip Hop na kimsingi yeye na wengine nategemea kuwa Watakuwa mstali wa mbele KUSEMA UKWELI NA HATA KUUFIA ili mradi kinachotoka kwenye kinywa chake/chao kiwe ni KWELI TUPU mfano:-
Msanii Tupac amewahi kusema nanukuu

"When I speak I wana truth came out no matter..............................I wana change the World "

mwisho wa kunukuu

lakini pia bila kujali kitatokea nini kesho au baada ya kusema hayo ili mradi kitaleta dhana ya Mabadiliko kwenye jamii husika,siku Roma alipoachiwa nilitegemea afanye Dunia ijue kama huku Tanzania tumefikia mahala wasanii wanatekwa,wanapigwa au hata kudharirishwa lakini pia nilitegemea aseme nani alimteka kama amemjua au kama hajamjua basi atuambie watu wa Ulimwengu wa Hip Hop(wasanii na Mashabiki)ili tuendelee na Maombi mpaka ajulikane,sijasema alichoimba hakifai ila najiuliza ameimba kwaajili ya UKWELI UTOKE NJE AU KAIMBA ILI ARUDI KWENYE BIASHARA KAMA KAWAIDA(PUBLICITY)?NB:nawaza kwa sauti

2.GHARAMA ZA KUSEMA UKWELI NA MATOKEO YAKE KWENYE JAMII
-Jamii yetu kama zilivyo jamii za Kimataifa tupo kwenye WAKATI WA MABADILIKO haiepukiki hata kidogo au hatuwezi kujitenga tukasema sisi hatutaki hayo mambo.Tunashuhudia Nchi za wenzetu wakifanya Mabadiliko makubwa ya KIUCHUMI,KIJAMII NA KISIASA maana yake ukiona mwenzio ananyolewa zako tia Maji
.........for the new change sacrifice must made......
-Inawezekana wakati amepatwa na janga la kupotea Roma baada ya kupatikana angesema ukweli palepale angefanya Tanzania tuingie kwenye Mabadiliko makubwa sana kwani kuna wakati jamii inaweza kupata mabadiliko kwasababu ya Mtu mmoja(jasiri na mwenye Imani ya kweli na asiye na chembe ya uoga kuhusu kesho) tofauti na alivyosema Mambo yapo polisi akisema ataharibu upelelezi(sijui hadi leo upelelezi haujakamilika?),bad enough siku alikuwa anafanyiwa mahojiano EAT.....kipindi cha Usiku alisema kama angesema ukweli eti kuna wakati hata hizo Show za milioni TANO labda asingekuwa anapata inawezekana ndo angeishia hapo.......sasa najiuliza maswali kadhaa

a)waliomteka(kama ni kweli)ndo hao wanaompakaga Show?

b)Anawafahamu maana tulifanya maandamano mioyoni ya kumtaka aachiwe akiwa mzima/hai,kwenye mitandao tulisema sana?

c)Show na biashara zake ni muhimu kuliko anachokiimba siku zote kwenye nyimbo zake,anasemaga akafungwe au akatupwe kwenye daraja la...............ni sehemu ya biashara tu au anamaanishaga kitu kweli huyu?

KRS ONE anasema nanukuu
"think about children we bring up........"

Wapo wanahip hop wanaokuwa na kujifunza kwetu kama sisi tulivyojifunza kwa Kaka na Baba zetu sasa kama tutakuwa wakwanza kuwaza watoto wetu,familia zetu na Material things hatutafanya mabadiliko yoyote kwenye jamii zetu hata siku moja............

3.ROMA TEMBEA JUU YA MANENO YAKO
-Nikiwa ni mtu ambaye naamini kwenye Hip Hop ndo chanzo cha Ukombozi kwenye jamii nyingi duniani,natamani watu wote mtembee juu ya maneno yenu kama Ukiimba kitu uwe unamaanisha kweli mfano mzuri ni Bob Marley alikuwa anasema mambo ambayo anaweka msimamo kwa gharama ya Uhai wake ndo maana mpaka leo Tunamkumbuka na Kumheshimu sana,Waliofia ukweli na wanaheshimika wapo wengi kama wanaharakati Malcom X,Martin Luther.......n.k(dunia inawakumbuka na kuwaenzi kwa heshima)

Roma na Wasanii wengine lazima mjue Watawala wanaweza kubadilika kila msimu na watakumbukwa kwa Mabaya yao na Mazuri yao lakini kwenye HIP HOP HAUTAKUMBUKWA KWA KUWA MWOGA NA MJINGA KISA BIASHARA,unaweza kuwa tajiri sana lakini utajiri wako/biashara yako ina maana gani kama hautendi yale ya KWELI/HAKI,haufanyi yaliyo kwenye moyo wako?

-sikiliza nyimbo za Ant-Vitus,CO2,KRS ONE,FUGEE,SUGU,MAR-P na wengine wengi wanasema yanayowajaza na kuisaidia Jamii kwa ujumla.

-Mwisho nyimbo ni nzuri sana but Speak louder than you do I know you can!

KIJANA FIA UNACHOKIAMINI USIWE MTUMWA WA BIASHARA NA KUTENGENEZA PUBLICITY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom