under_score
Senior Member
- Nov 2, 2011
- 190
- 45
The interesting part of it. Hivi watu walipelekwa mahakamani hata kabla ya uchunguzi kufanyika, hii si kuiongezea idara ya mahakama mzigo kwa kesi zisizo na ulazima?
Wakuu,
hata mimi siko mbali sana na maoni kama hayo yaliyotolewa hapo juu, japo sioni ajabu kwa kesi dhidi ya Mh. Lema mbunge wangu kufunguliwa mahakamani kabla hata ya uchunguzi kwani si mara ya kwanza kusikia hayo yakifanyika, japo sifahamu kama huo ndio utaratibu sahihi wa sheria, kwani mimi si mwanasheria.
Ila, kinachonipa wasiwasi mimi ni hili la Mh. Lema na OCD Zuberi kufunguliwa 'jalada moja' la uchunguzi! Ina maana nature ya makosa wanayotuhumiwa nayo yanafanana kiasi cha kufunguliwa 'jalada moja' la uchunguzi ??
Ok, Mh. Lema kishafunguliwa kesi tayari, je ina mana OCD Zuberi akipatikana na hiyo hatia anayodaiwa kuchunguzwa nayo naye pia ataunganishwa kama mtuhumiwa kwenye Kesi hii ya Mh. Lema na Wenzake 18??
Na kama hivyo ndivyo, je ni vipi sasa OCD Zuberi yeye anakuwa uraiani bado, wakati Mh. Lema na wenzake 18 washafunguliwa kesi tayari mahakamani??
Learned brothers, hivi hii imekaaje jamani, em naomba msaada wa hekima zenu kidogo!