OCD, Zuberi Mwombeji afunguliwa jalada kwa kuwaita panya wana A TOWN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OCD, Zuberi Mwombeji afunguliwa jalada kwa kuwaita panya wana A TOWN

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Nov 3, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri,” alisema OCD Mwombeji.

  chanzo: mwananchi
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Huu utetezi wa malezi mema kutoka kwa familia naona sasa umekuwa wimbo wa kawaida wa wakurupukaji serikalini na kwingineko.
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  polisi wanamchunguza polisi mwenzao hapo kuna haki itatendeka kweli kwanini wasitafute independent entity kuchunguza issue nzima. we need an independent eye to look into it and not someone who has a dog in the fight.
   
 4. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Panya niyeye na mabwana zake wanao mtumia kuwachanganya watu. Nyambaf nguvu ya umma itawaangusha tu
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Filing a case is one thing but observation of justice is another important yet difficult thing to happen given bad record of our legal authorities. They probably have to launch an independent committee to investigate into the allegations but not relying on same corrupt organs to expect fairness and justice.
   
 6. Z

  Zhu Senior Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapanya ni wale wahuni. Lugha.Jf hapa kuna matusi yakutisha, mbona hakuna kesi.
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hiyo lugha unayotumia ndiyo Zuberi aliitumia na wewe kesho ikiambiwa umewaita binadamu panya utakataa kama anavyokataa OCD, anajifanya eti amelelewa vizuri familia gani inafundisha kuwaita binadamu wenzake panya kumbe hata tanzania tuna kina Gaddafi shame on him ngoja nitafute wanasheria niinunue hiyo kesi.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ufunguaji wa jadala kumchunguza mkuu wa kituo cha polisi Arusha ni kutokana na tishio la wananchi wa Arusha kuweka mgomo wa vyombo vya usafiri, na kama hatua hazichukuliwi maana yake kizaazaa kikubwa kitafumuka, hii ni ishara wazi ya nguvu ya umma isivyoshindikana.
   
 9. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Walifikishwaje mahakamani kama uchunguzi ulikuwa haujafanyika sawa sawa na kupata ushahidi ili haki itendeke? Je, ina maana watafuta mashitaka yaliyoko mahakamani sasa? Na kama mahakama itandelea na kesi, polisi watatoa ushahidi upi ikiwa uchunguzi ndiyo kwanza unafanyika?

  Na je, kama uchunguzi ukifanyika na kukosa ushahidi dhidi ya hiyo kesi ambayo tayari iko mahakamani, je POLISI watachukua hatua gani dhidi ya POLISI ambao wamefungua kesi ya uongo, ya kubambikiza?

  Hili sakata la Lema na Mwombeji aidha litampa Mwombeji u-RPC mahali fulani au litamrudisha kijijini kama Zombe. Time will tell.

  Simfahamu vizuri sana RPC Mpwapwa, ila wanaomfahamu vizuri wanasema ni mtu makini na anaijua kazi yake, japo wakati mwingine anayumba kidogo kuchukua hatua.
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Arusha inaweza kuanzisha kama Bengazi kisha wengine wanaitikia hadi ukweli uenee nchi nzima.
   
 11. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  kesi ya panya ,hakimu paka! Kuna haki hapo kweli?
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  asimsingizie mama.... Kwani mama ndie aliemfundisha ukatili na dharau?
   
 13. u

  ureni JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi ningependa kutoa maoni yangu kama ifuatavyo,huyu OCD aliyewaita wananchi panya ni kuwa tayari ameshatuhumiwa kama alivyotuhumiwa Lema,hivyo basi kua huyu ni boss wa polisi ili aachie uchunguzi ulio huru anatakiwa ajiuzulu apishe nafasi ya uchunguzi huru,akishajiuzulu akamatwe awekwe ndani apelekwe mahakamani na apewe nafasi ya kupata dhamana vilele kama alivyopewa lema manake ni haki yake ya kimsingi na kesi iendelee mpaka hukumu itakapotoka.
  Zaidi ya hapo kama ataendelea kuwa madarakani uwezekano mkubwa wa kuvuruga ushaidi upo.
  Inatakiwa ieleweke kwamba raia yoyote akitenda kosa lazima sheria ichukue mkondo wake hata akiwa hakimu.
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  wewe nawe ovyo!
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Inauwaje mtu anafunguliwa jalada wakati akiendelea kushika wadhifa ambao kwa namna moja ana nyingine utazuia uchunguzi huru?. Ilitakiwa ajizulu kwanza wadhifa huo ili kupisha uchunguzi huru. Anything short of that is tactic to calm the public anger on one man who thinks his authority can be used to punish those who are opposing him. He abuses the power.

  Historia inaonesha kuwa chunguzi kama hizi huwa hazina effect kwa mchunguzwaji. Hapo ni IGP kuangalia chini na kumuhamisha kituo cha kazi huyu mbabe ambaye uwepo wake Arusha una negative effect kwenye mahusiano kati ya polisi na wananchi. Polisi wanatakiwa kuwa rafiki wa raia wema na si adui. Maamuzi hayo yatakuwa ni ya busara zaidi kuliko polisi kuanzisha uchunguza wa kisanii kama huu.
   
 16. m

  mataka JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 287
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  mtaongea sana zaidi ya kasuku! Mbona akina Lowassa, Chenge na wengineo wengi waliochota mabilion na kuhifikisha nchi hapa ilipo kwa madeni ya mabilion ya kesi mbona wanapeta barabaran na mavogo lakn hawakuwekwa ndani sembuse mtu ku2humiwa kusema neno panya! Mie sio tatizo kwa jinsi 2lpofikia na kaneno hako. Hayo mambo ya siasa mwisho wake ni vurugu tu.
   
 17. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo tuhuma ya OCD imebaki moja tu sasa ya kuwaita wananchi panya ambayo ikikosa vielelezo ocd hatapatikana na hatia yoyote, na kauli yake ya malezi mema ya familia yake itakuwa kweli.
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160


  Nilitegemea huyo ocd angesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi lakini hawajazungumzia jambn hilo. Na hapo ndio uchunguzi unapotiliwa shaka!
   
 20. k

  king kong Senior Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asimamishwe kenge na mdomo wake wa siasa za maji taka
   
Loading...