OCD, Zuberi Mwombeji afunguliwa jalada kwa kuwaita panya wana A TOWN

Its real terrible,, inadhihirisha polisi walivo wa kukurupuka. huwezi kusema umeanzisha uchunguzi kwa inshu/case ambayo tayari iko mahakamani, ina maana umeipeleka kwa ushahidi upi? nani anamchunguza OCD zuberi,,maofisa toka Makao Makuu ya Polisi? Rpc mwenyewe na Staff Officer wake? Kuna watu wengine independent nje ya JESHI LA POLISI KATIKA UCHUNGUZI HUO? Rpc ahojiwe upya juu ya components za kamati hiyo otherwise tusitegemee chochote tofauti
 
Kumbe kuna kipindi mwita uwa unapata nafuu ya matatizo yako ya akili!!
filing a case is one thing but observation of justice is another important yet difficult thing to happen given bad record of our legal authorities. They probably have to launch an independent committee to investigate into the allegations but not relying on same corrupt organs to expect fairness and justice.
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita."Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote," alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya.
The interesting part of it. Hivi watu walipelekwa mahakamani hata kabla ya uchunguzi kufanyika, hii si kuiongezea idara ya mahakama mzigo kwa kesi zisizo na ulazima?
 
Mim binafsi nlikuwa mahakamani na nikamsikia akitamka manene hayo, kwa bahati nzuri kuna bwana alimrekodi akitamka hayo maneno.
 
OCD, OCD, Kwa maana halisi. Kwamba anachunguzwa wakati yuko kazini???????????? Taarifa zote za willaya kuhusiana na jeshi la polisi zinapata idhini yake kwanza wakuu! Kwa ufupi ni ngumu sana KUMPIGA PANYA ALIYETUMBUKIA KWENYE MTUNGI KUKIWA NA MAJI YA KUNYWA. Hii kitu sielewi kabisa.
 
Kesi ya ngedere kula hindi kwa shamba nyani kuwa hakimu..sasa wapi haki patikana banaa...Tazama sana taona kesi kwisha mara moja bila jibu patikana....Mtu taka badiliko kwa nchi na dola piga piga mitaani...Haki ya mtu hapana potea banaa....
 
Maneno mbofumbofu kama ya huyo OCD ndio ilifanya wale vijana wale vijana wa Libya kumfanyia 'kitu mbaya' Gadaffi kabla ya kumuua!
 
Tanzania ni nchi moja ya ajabu sana ambapo CEO anateua wafanyakazi walio chini yake wamchunguze, polisi watamchunguzaje OCD wakati baadhi wanapangiwa majukumu na huyo huyo wanayemchunguza? Kweli ukistaajabu ya Musa njoo Tanzania utaona ya filauni, anatakiwa akae pembeni wakati uchunguzi ukiendelea huo ndio utawala wa sheria vinginevyo sheria tunaziimba tu mdomoni.
 
Huu utetezi wa malezi mema kutoka kwa familia naona sasa umekuwa wimbo wa kawaida wa wakurupukaji serikalini na kwingineko.

Inabidi familia ziwe ziantoa certificate, ili tuthibitishe kama kweli alipata hayo malezi, maana matoto mengine yanakulia kwenye vijiwe vya bangi, then yakija kuita watu mapanya yanadanganya yalipewa hayo malezi. Show us at least certificate of attendance of family 'malezi mema program'...
 
huyu OCD AMEAGIZWA KUFANYA HII kazi yeye ni mbwa tu anabweka tudili na system mbovu ya wale wezi waliomuweka mamlakani pasipo maaadili
 
Mim binafsi nlikuwa mahakamani na nikamsikia akitamka manene hayo, kwa bahati nzuri kuna bwana alimrekodi akitamka hayo maneno.

Wakuu, mwenye original clip ya hiyo incident em tungeomba atuwekee hapa jamvini kabla hatujaja letewa 'fake' yake iliyochakachuliwa na hawa wabakaji wa haki za msingi za binadamu, maana washazoea kufikiriaga kila mtu ni mpumbavu sana huku ulimwenguni kasoro wao !
 
Police na siasa wapi na wapi, nafikri ungesema..uonevu coz OCD hafanyi siasa.
Unaweza kufikiri hafanyi siasa lakini OCD anafanya siasa kwa maelekezi ya CCM, tatizo analeta maneno wanayotumia jeshini kwenye siasa, jeshini kuitwa panya ni jambo la kawaida wakati nikiwa JKT tuliitwa majina tena mengine mabaya zaidi ya hayo. Namshauri achague moja kazi yake au siasa kama anataka siasa apande majukwaani apambane na kina Mtikila kwa maneno si kufanya siasa akizidiwa anajikinga kwa krauni ya polisi.
 
Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita
Jamani hebu tujiulize kesi inayochunguzwa si iko mahakamani? kwanini waanziche kesi nyingine huku si kuingilia mahakama? majalada mawili kwa kesi moja au mimi sijui mambo ya mahakama. Lets say, uchunguzi wao huu mpya uwakute wote wana hatia baadae ile kesi ya mahakama waliyofunguliwa wakutwe hawana hatia and vice versa itakuwaje? najiuliza tu.
 
Back
Top Bottom