OCD, Zuberi Mwombeji afunguliwa jalada kwa kuwaita panya wana A TOWN

wewe mwombeji ni pakashume na subiria uliwe na mapanya kama gadafi
 
Asimamishwe au la Nguvu ya umma itamwondoa,Nanyaro ambaye ni mwenyekiti wa BAVICHA mkoa amenukuliwa akimtaka IGP achukue hatua haraka sana kuhusiana na hili sakata vinginevyo wataingia barabarani hadi OCDangoke,kamwe haturudi nyuma
 
Filing a case is one thing but observation of justice is another important yet difficult thing to happen given bad record of our legal authorities. They probably have to launch an independent committee to investigate into the allegations but not relying on same corrupt organs to expect fairness and justice.
Mwita25 usibadili ID maana rula unazonyoosha siku hizi siyo za kichina bali from German!!!! Upo sahihi kabisa, ni njia ya kutaka kumuosha kamanda Zuberi.
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri,” alisema OCD Mwombeji.

chanzo: mwananchi

Hakuna haki yoyote itakayotendeka kwa polisi wao kwa wao kuchunguzana sana hii ni danganya toto ili kuwapunguza watu hasira.Wanachosema na watakachokitenda vitakuwa ni vitu viwili tofauti.Pili wanasema watafanya uchunguzi kwa maswala yote mawili kwa Lema na OCD kwa sbb ilitokea kwa wakati mmoja,sasa kama hawakuwa walishafanya uchunguzi ni kesi gani walimfungulia Lema wkt uchunguzi ulikuwa bado?Tukisema polisi mnatumika kuvunja sheria badala ya kuzisimamia mnasema uongo sasa ukweli ni UPI Kama sio mifano mbayoionyesha waziwazi?.Jana polisi pia walikuwa wakiwakamata watu kwa kuangalia mavazi(combati)sasa hii ni halali?Mnatujengea chuki wananchi kwa kuwachukua nyie kbs,ulinzi shirikishi mtafanya na nani?.
 
Polisi Mkoa wa Arusha imefungua jalada ya uchunguzi dhidi ya kauli ya kuwaita panya wananchi na wanachama wa Chadema inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Zuberi Mwombeji. Kamanda Mpwapwa amesema sambamba na uchunguzi huo, jalada hilo pia litahusika na uchunguzi wa makosa yanayodaiwa kutendwa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na watu wengine 18 waliofikishwa mahakamani Jumatatu iliyopita.“Kwa sababu mambo yote mawili ya uhalifu unaodaiwa kutendwa na Lema na wenzake pamoja na madai ya OCD kuwaita wananchi mapanya yalitokea sehemu moja na siku hiyohiyo, tutayachunguza kwa pamoja kubaini ukweli na kupata ushahidi ili haki itendeke kwa wote,” alisema Kamanda Mpwapwa.Oktoba 28, mwaka huu akiwa eneo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alikokuwa akikiliza kesi ya kupinga ubunge wa Lema iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, OCD Mwombeji anadaiwa kuwaita wananchi wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema mapanya. Akizungumzia madai hayo jana kwa njia ya simu, OCD Mwombeji alikana kutoa kauli hiyo na kusema hizo ni propaganda zinazoenezwa kuhalalisha uhalifu au kutafuta huruma ya umma kwa makosa yaliyotendeka. “Sijawahi wala siwezi kumwita mwanadamu mwenzangu panya. Ukiachilia mbali maadili na malezi mema niliyopata kutoka kwa familia yangu, hata wadhifa na cheo changu hakinipi uhalali wa kutoa kauli kama hiyo, ninaomba umma wa Arusha usubiri uchunguzi unaoendelea kwani ukweli utadhihiri,” alisema OCD Mwombeji.

chanzo: mwananchi
Uchunguzi unafanywa na nani? ameteuliwa na nani? Natabiri ushindi kwa OCD mwombeji.
 
Anachunguzwa na askari wa chini yake au wakubwa zake? Ameshasimamishwa kazi ili kupisha huo uchunguzi? Hapa ni kudanganyana tuu hakuna kitu.
 
Nahusisha uhusiano wa Lema na Mwombeki na ule wa Mrema na IGP. Jamaa anafanya kila liwezekanalo akifikiria u IGP. Aibu yake.
 
We live in times where the world has no mercy for people who dont want to use and apply their brains. Police in Tanzania, the long term view of its success lies on the professionalism. Short of it, the force would become part of the big political problem. It is important of them to choose the side to work with very careful!
 
Huu utetezi wa malezi mema kutoka kwa familia naona sasa umekuwa wimbo wa kawaida wa wakurupukaji serikalini na kwingineko.
Kwa hiyo anataka tuamini kuwa Wazazi wa RA walimlea mtoto wao katika mazingira ambayo yangemuandaa aje kuwa fisadi? Au Wazazi wa Zombe walimlea mtoto wao katika mazingira kwamba akikua aje kuwa uwa uwa! Aache upupu wake hapa. Yeye ameshalikoroga angoje sasa kulinywa tu.
Na kama walifanya uhalifu sehemu moja sambamba na Lema, kama inavyodaiwa hapa, mbona yeye hajakamatwa bado wakati uchunguzi unaendelea! Au wengine huwa wanahukumiwa kabla kabla hakimu hajatoa hukumu wanawekwa ndani na wengine lazima kwanza uchunguzi ufanyike ndio wakamatwe!
 
Huyu mzee ni mnafiki sana,hastahili na hafai hapa Arusha!!!ajue kuwa sheria ni msomeno,hukata huku na kule!!!Kama yeye yuko juu ya sheria sawa!!!
 
polisi wanamchunguza polisi mwenzao hapo kuna haki itatendeka kweli kwanini wasitafute independent entity kuchunguza issue nzima. we need an independent eye to look into it and not someone who has a dog in the fight.

Haki iko mikononi mwa wananchi wenyewe maana sisi ndio ametutukana panya. Kila anayemtukana mwenzake panya hujikuta amekuwa panya wa kikwelii kama Gaddafi
 
Sasa nani anamchunguza nani? Lakini wakati mwingine polisi wako fair (baadhi). Hata hivyo ingekuwepo kamati ya polisi, asasi za kijamii na raia kuchunguza ukweli huu, au la sivyo OCD apewe likizo ya lazima ili kupisha uchunguzi.
 
Kubambikizia watu kesi ni maadili mema? au familia yake ilisahau na hilo?
 
Back
Top Bottom