Nyumba yenye chumba kimoja self sebule na jiko inaweza tumia tofali ngapi wadau

Nyumba yenye chumba kimoja self sebule na jiko inaweza tumia tofali ngapi wadau
Chumba kina ukubwa gani? Jiko lina ukubwa gani? Sebule ina ukubwa gani? Unapaua kawaida au hidden roof?

Kuna kamoja nataka nijenge kwenye kieneo kidogo nategemea kutumia tofali 1,200 ila chumba 3m*3m na sebule 3m*4m.
 
we mzee baba nyumba inategemea na vitu kama:-
1. ukubwa wa nyumba- experience yangu mwaka fulani nilianza kujenga chumba na sebule nikanunua tofali elfu moja ila ninavyokumbuka chumba niliweka kumi na mbili 12*12 alafu choo nikaweka tano , sebule nikaweka kumi na na tano hivyo upana ukasomeka kumi na saba(17) alafu urefu ikawa ishirini na saba 27 (sina uhakika na vipimo kama ni mita au futi) hizo tofali sikutoboa zikaisha kati kati ya ujenzi.
2. Eneo husika- eneo lenye muniko utatumia tofali kidogo tofauti na eneo lilopo tambarare
3. ukubwa/urefu wa msingi- kadri msingi unapokuja juu ndipo idadi ya tofali zinalika.
4. ramani ya nyumba- ramani yenye umbo la mraba aitachukua tofali nyingi tofauti na ramani yenye mbwembwe kona kona nyingi, hapa ndio utasikia mbona wote wamejenga nyumba yenye idadi sawa ya vyumba n.k lakini mmoja tofali nyingi mwengine katumia tofali kidogo.
5. wengine wanasema idadi ya uwazi na ukubwa wake- uwazi kama wa madirisha milango N.k wanasema inapunguza matumizi ya tofali (sina imani nalo sana binafsi)
wakati naanza niliambiwa chumba kimoja kinakula tofali 400 kwahiyo unaweza ukaanza na idadi hiyo ukapiga mara partion unayoitaka japo aiwezi kuwa hesabu halisi lakini utapata mwanga fulani hivi, hivyo ndio ninavyovikumbuka kutokana na uzoefu wangu wa ujenzi naamini umepata ABC katika hilo.
Ziada.
Mfuko mmoja wa cement niliambia unajenga tofali 40-50 za msingi alafu zile za baada ya msingi unajenga 60-70 (nikitaka kuthibitisha mambo yanaingiliana najikuta napoteza hesabu)
 
Back
Top Bottom