Nyumba ya Sanaa inabomolewa!

Insurgent, why win situation, when the title belongs to you. I tend to think that it is a loose situation. And by the way mijamaa haina hela itachukua loan kujenga hizo ghorofa kwa nini menejment ya nyumba ya sanaa wasijenge wao?

Isijekuwe management ya nyumba ya sanaa walifanya kama siganature yako inavyosema!!!!!

Title pekee haitoshi kujenga jumba la sivyo wengi tungekuwa na majumba :)
 
Una uhakika gani haitakuwa quality? Bado unadhania...

Historia inatufundisha. Hakuna aliyeingia katika mikataba kama hii alipata quality space, kuanzia TLS na kuendelea. Sasa wewe usiyedhania basi tupe facts, hao Nyumba ya Sanaa wamepewa ukubwa gani na kwenye ghorofa zipi?

Amandla....
 
i AM SAD KWAMBA ILE KITU IMEBOMOLEWA...

LAKINI NDIO COST YA MAENDELEO NA NASKIA VIGOGO WAMO NDANI HUMO WAKILAMBA LIPS TU KUSUBIRI RETURNS ON INVESTIMENT
 
Yaani hapo umetema kama mimi ninavyotema. Straight up....no sugar coating.
na mimi niliyezaliwa ocean road hospitali nielekee kijiji gani??
acha kuongea kama umekosa dira.
Ukiingia kiundani sana utakuta Nyumba Ya Sanaa haikuwa idea ya mzungu bali yeye aliendeleza wazo. ni kama kusema Reggae imeanzishwa na Bob Marley na Peter Tosh ilihali wao walikuwa Renaissances artists tu.
Manufaa ya Nyumba ya Sanaa ni makubwa kuliko hizo valuer unazoenda kunywa pale jioni
 
Gazeti la Dira la leo, kuna taarifa kutoka ubalozi wa Norway kuhusu Nyumba ya Sanaa. wamekiri kupokea copy ya waraka wa wasanii walioupeleka Ikulu kwa rais. Balozi ametoa comments zake. Nipo mbali kikazi ila nimepigiwa simu na mdau anayefuatilia ishu za Nyumba ya Sanaa.
Seems serikali ya Tanzania haiwezi kufanya kitu mpaka ipigwe pressure.
Je hatuna right thinking????
 
Jamani mbona jumba hilo liliisha achana na biashara ya wasanii na usanii?
Mara ya mwisho nilipitia pale palikuwa ni mahali pa mvinyo wa bei mbaya, makutano ya sister-do waendeshao mb na wanabees wa mtaani. Kumuenzi JKN kulifutika tangu awamu ya pili, sema tu wengi wetu inakuwa ni vigumu kulikubali hilo na mpango wa kulipinga hatuna.
Maandalizi ya kubadilisha matumizi yalianza muda mrefu kabla haijafutwa rasmi hapo february 24 2005. Kilichoendelea ni kuwekana sawa na kufukuzana ktk bodi ya wadhamini ili wabaki wale wanaoongea lugha moja. Baada ya hapo wakaanzisha kampuni iitwayo Nyumba ya Sanaa Ltd ambayo ikadaka mali zoote za taasisi ya awali na wakaendelea kuingia mikataba na madudu mengine mpaka walipompata huyo mwekezaji aliyejificha nyuma ya NBM.

Dawa ya tatizo la Nyumba ya sanaa ni kumwomba Mdhamini mkuu wa serikali aliyeko HAZINA kuichukua (hakuna atakayempinga kisheria) kisha utaratibu wa kuunda chombo huru au bodi huru kuiendesha au kuunganisha vyama vya sanaa kuiendesha kwa manufaa ya wasanii na watanzania kwa ujumla.

Lawama za awali zimwendee Sr. Jean ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa taasisi hiyo kwani ndiye aliyewakaribisha matapeli kwenye bodi na ndugu Josephat Rweyemamu ambaye alihusika kuwashawishi hao matapeli kufanya mapinduzi ya kumtoa Sr. Jean na kubadili mfumo wa Nyumba ya Sanaa. Ila kiboko ya yote ni ndugu Aliko Atunkolepo ambaye ni mwenyekiti wa NYS since miaka ya tisini ambapo hakuruhusu kufanyika uchaguzi na uteuzi wa wajumbe wapya na ndiye aliyeinjinia kuifuta bodi ya Nyumba ya Sanaa kwa kabidhi wasii mkuu ili atimize lengo lake analolitimiza sasa. Mjue ana mashtaka bandia aliyofunguliwa na wanabodi wenzake (wawili) kisutu kuhusu masuala ya ufisadi wa fedha za mwekezaji. Kuna mengi yametendeka pale ila serikali inayajua na inahusika big time.
 
tumeuza urithi wetu wa ardhini sasa tunashindwa hata kutetea urithi wetu wa vizazi vijavyo. Huyo Sr. kutokana na vyanzo vyangu vya ndani sana amejaribu kuona wenye nchi wanabadili uamuzi. Kitu ambacho sijui ni nini kimetokea. Ningependa tupate nafasi ya kumhoji huyu sista.. what happened. Wakati wengine wana tatizo kwa sababu jina la Lowassa limetokea mimi tatizo langu ni dhana nzima ya hicho kilichotokea. Kati ya maeneo yote jiji la Dar.. la Nyumba ya Sanaa ndilo lililokuwa bora.. yawezekana sista alipewa "offer she couldn't refuse"?
 
Kuna wakati Ocean Road hospital ilikuwa karibu ipigwe bei kuruhusu ujenzi wa hoteli mahala pake. Mkurugenzi wa Mambo ya Kale wa wakati ule angelegea tu, saa hizi tusingekuwa na hospitali hiyo! Sitashangaa kusikia tena kuwa pale mahali pamepigwa bei na mfadhili amewapa ghorofa tatu kwa ajili ya matumizi ya hospitali. Bila shaka wengi humu na nje ya humu wataona hayo ni maendeleo!

Amandla.....
 
Nimeongea na ARCHIVE wamesema suala la nyumba ya sanaa ni mfupa mgumu kwao kuukabili kwa sasa. kwani wana majengo yaliyopo chini ya uangalizi wao lakini yanabomolewa kibabe kupisha ujenzi wa ghorofa za vioo kwa ajili ya uwekezaji.

Ndugu Aliko/ Alipo maarufu Babu A! tangu achukue madaraka ya uenyekiti wa bodi alihakikisha anaajiri mameneja wakuu wa NYS ambao ni std 7 leaver. nina ushahidi kwa hilo. na sasa baada ya kumtimua meneja Saria Mauky aliyekuwa kilaza wa kutupwa (darasa la saba) amemwajiri ndugu Jamal ambaye hata hakumaliza hilo darasa la saba na hana elimu wala ujuzi wa masuala ya menejiment sembuse ukuu wa idara. Anafanya hivi ili anapowatumia kuendorse masuala yake wasiweze kuhoji kwani wanajua wamepewa ulaji wa kudra. Kuna mjumbe mwingine wa bodi anaitwa Lyimo ambaye yupo viwanda na biashara (mchumi) pia na ndugu Ntomola ambaye mara ya mwisho nafahamu alikuwa TIC. hawa ndo wahusika wakuu wa mikataba yote na utapeli wooote. Babu A. ni mwanasheria ambaye alikuwa kanjanja miaka mingi hadi alipograduate OUT miaka sita iliyopita ila kabla ya hapo alikuwa na certificate in law lakinia aliendesha law firm kiujanja-ujanja mpaka alipopata uwakili majuzi. Huyu m-baba ni mwongeaji na diblo mzuri sana. hata waziri seif Khatib alipopewa tipp na wasanii kuhusu Nyumba ya sanaa alikwenda na kupigwa ganzi na kukaa kimya. Anatumia kigezo cha kuwalilia wasanii ili atimize malengo yake.

Nina maswali mengi sana najiuliza kuhusu hii kadhia. na ninapata tashwishwi kwamba kuna wakulu wapo kwenye system wanachekelea hii saga. Kuna mwandishi aliandika makala in daily news miaka minne iliyopita alitishiwa maisha na kutaka kushtakiwa.... najua aliyefanya hivyo ni Babu A.

Hawa wanaoshadidia uwekezaji wa kujenga ghorofa pale NYS wanajua maana ya ARTIFACT?? ina umuhimu gani kwa jamiii??? au wapo wapo kama mbu anayesubiri kufa baada ya kunyonya damu ya mtu?

Hivi hawa akina LOWASA hawawezi kusomewa dua mbaya wakashuka six feet under by tomorrow?? at least nchi itapumua.
 
valluer.jpg
Yaani hapo umetema kama mimi ninavyotema. Straight up....no sugar coating.
na mimi niliyezaliwa ocean road hospitali nielekee kijiji gani??
acha kuongea kama umekosa dira.
Ukiingia kiundani sana utakuta Nyumba Ya Sanaa haikuwa idea ya mzungu bali yeye aliendeleza wazo. ni kama kusema Reggae imeanzishwa na Bob Marley na Peter Tosh ilihali wao walikuwa Renaissances artists tu.
Manufaa ya Nyumba ya Sanaa ni makubwa kuliko hizo valuer unazoenda kunywa pale jioni
 
Nyumba ya Sanaa (in Swahili, "House of Art"), also known as the Mwalimu Nyerere Cultural Centre or Julius Nyerere Cultural Centre is a cultural centre in Dar es Salaam, Tanzania, established to promote local art and craftmanship.

The Centre was founded by Maryknoll Sister from Los Angeles in the United States of America, Sr. Jean Pruitt in 1972. Sr. Jean founded Nyumba ya Sanaa (House of Art) a special shop for Tanzanian youth artist to display their creative handicraft works and sell them. It supports local artists, stages dance and music exhibitions, and sells local art such as tingatinga paintings. It is one of the main tourist attractions in Dar es Salaam.

George Lilanga, one of the most famous Tanzanian artists, began his career at the Centre. Part of the buildings of the Centre, as well as its main entrance gates, have been decorated by Lilanga.
 
Msanii

Hili suala seems limekugusa sana - But, kuweka masuala katika perspective - Hii nchi inatawaliwa na "genge la wahuni". Kwa wao what matters is today and tomorrow will take care of itself! Kikwete yupo pale Magogoni "symbolically", watawala wako O'bay, Masaka, na Mikocheni.

Ipo siku"Salender Bridge" Polisi Station itauzwa, Ocean Road hospital ipo karibu sana kuuzwa, na nadhani yule Mama wa EOTF - Former First Lady aliikosa kosa by Inches! - Naona wameshaweka na "road block" usipite nyuma yake between 18hrs - 06hrs. Mabadiliko ya "matumizi ya ardhi" yanayofanyaka Tanzania ni ya kutisha sana - Pale Palm beach hotel vipi? Etienne je? Nasubiri uwanja wa Gymkana utauzwa lini?
 
Niliwahi kuona barua iliyotumwa kwa rais kwa dispach ambayo wasanii walisign kumwomba aingilie kati kuzuia uvunjwaji wake. lakini kama kawaida Kikwete msikivu hakuwa na muda wa kilio cha wasanii.
ndo maana hajawapangia wizara itakayoshughulikia ishu zao.

Barua ilipelekwa last month naambiwa ikapokelewa. na wasanii walituma nakala kwenye balozi za nchi zilizojenga nyumba ya sanaa.

Inaonesha kuna watu Ikulu wanafaidika na kuuzwa kwa nyumba ya Sanaa
kwa hiyo kila kitu kiundiwe wizara mpaka na hawa wanavaa nusu uchi nao waundiwe wizara!
 
kuna vitu vinanikeraga sana, eti preserve nyumba ya sanaa for heritage, usiweke mradi wa umeme kihansi, utaua vyura, usipitishe barabara kandokando ya serengeti, utabughudhi wanyama......usipofikiria sana utagundua wazungu wanatuona sisi waafrika kama makumbusho flani hata mahitaji yetu ya kibinadamu yanapimwa katika mtazamo huo.. vunja weka vitu vya maana hao vyura wa kihansi waite wazungu wakaweke huko kwao sisi tunao wakutosha, na hiyo nyumba ya sanaa inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida?vitu vyote vinapatikana slipway,makumbusho,bagamoyo hakuna sababu ya kuwa nazo kama uyoga kila sehemu.

Rafiki yangu mmoja aliwahi kunikumbusha msemo mmoja "Ukiwa uchi wa mnyama wa tutakuvika hata ukoka ujisetiri lakini ukiwa uchi wa akili tutakuvika nini"

Sisi kama Taifa,kama nchi ya ulimwengu wa tatu tuna nyuchi zote mbili uchi wa nyama na uchi wa akili.

Wenzetu nchi zilizo endelea wamejenga miji yao na kuisakafia vyema lakini utashangaa katikati ya mji wana kiunga kikubwa cha manyasi ambacho ni public. Kuna miji mingi sana katikati ya jiji kuna msitu wa ekari 50.
Sisi kwetu kuna watu wanatamani kujenga katikati ya barabara kwenye Fukwe viwanja vya wazi makaburini hata sehemu nyeti kama wet land ambako bahari inapumulia.

Kujenga kila mahali mpaka kupokonya maeneo ya wazi au yale yaliyotengwa kwa kazi maarum si utajiri. Kwa sababu hata hao wenye fedha nyingi wabebao jina halisi la matajiri kamwe hawatamani kabisa wazo hilo kujenga ovyo^2.

Tuna nyuchi zote mbili na pengine hata uchi wa tatu, uchi wa mnyama, uchi wa akili na uchi wa Roho
 
Nimeongea na ARCHIVE wamesema suala la nyumba ya sanaa ni mfupa mgumu kwao kuukabili kwa sasa. kwani wana majengo yaliyopo chini ya uangalizi wao lakini yanabomolewa kibabe kupisha ujenzi wa ghorofa za vioo kwa ajili ya uwekezaji.

Ndugu Aliko/ Alipo maarufu Babu A! tangu achukue madaraka ya uenyekiti wa bodi alihakikisha anaajiri mameneja wakuu wa NYS ambao ni std 7 leaver. nina ushahidi kwa hilo. na sasa baada ya kumtimua meneja Saria Mauky aliyekuwa kilaza wa kutupwa (darasa la saba) amemwajiri ndugu Jamal ambaye hata hakumaliza hilo darasa la saba na hana elimu wala ujuzi wa masuala ya menejiment sembuse ukuu wa idara. Anafanya hivi ili anapowatumia kuendorse masuala yake wasiweze kuhoji kwani wanajua wamepewa ulaji wa kudra. Kuna mjumbe mwingine wa bodi anaitwa Lyimo ambaye yupo viwanda na biashara (mchumi) pia na ndugu Ntomola ambaye mara ya mwisho nafahamu alikuwa TIC. hawa ndo wahusika wakuu wa mikataba yote na utapeli wooote. Babu A. ni mwanasheria ambaye alikuwa kanjanja miaka mingi hadi alipograduate OUT miaka sita iliyopita ila kabla ya hapo alikuwa na certificate in law lakinia aliendesha law firm kiujanja-ujanja mpaka alipopata uwakili majuzi. Huyu m-baba ni mwongeaji na diblo mzuri sana. hata waziri seif Khatib alipopewa tipp na wasanii kuhusu Nyumba ya sanaa alikwenda na kupigwa ganzi na kukaa kimya. Anatumia kigezo cha kuwalilia wasanii ili atimize malengo yake.

Nina maswali mengi sana najiuliza kuhusu hii kadhia. na ninapata tashwishwi kwamba kuna wakulu wapo kwenye system wanachekelea hii saga. Kuna mwandishi aliandika makala in daily news miaka minne iliyopita alitishiwa maisha na kutaka kushtakiwa.... najua aliyefanya hivyo ni Babu A.

Hawa wanaoshadidia uwekezaji wa kujenga ghorofa pale NYS wanajua maana ya ARTIFACT?? ina umuhimu gani kwa jamiii??? au wapo wapo kama mbu anayesubiri kufa baada ya kunyonya damu ya mtu?

Hivi hawa akina LOWASA hawawezi kusomewa dua mbaya wakashuka six feet under by tomorrow?? at least nchi itapumua.

Nalipata Simanzi lako.
Akina Lowassa wataishi muda mrefu kdiogo mpaka uovu waliouanzisha ujae nakufurika.

Wao wanapesa kuliko Dikteta Mobuto ambaye nchi nzima ya kongo ilikuwa yake lakini masikini baada ya kurudisha alikosa kuambulia hata kitalu chs '2x6' ili mwili wake ulale salama?

Akina Lowassa watendelea na Fujo zao mpaka muda wao utakapo kwisha.
Si lazima uwe mwisho wa maisha yao.

Tunahitaji hekima kumaliza ujinga uliojisokotea ndani ya jamii yetu kuliko dua.

Muumba alisha tupa kila kitu kwa ujinga tumeweka lehani kwa bei ya mlo manati.

Akina Lowassa wamefika hapo kupitia kwenye mabega yetu, wanapata kiburi kupitia mabegani mwetu, wanazidi kuwa na ujasiri wa kuiba kutapanya na kututazama usoni kwa kejeri kwa sababu ni sisi wenyewe tumewabeba na hatuna mpango wa kuwabwaga.

Dua haliwezi kusaidia kwa sababu kuna dua la kuwaombea maisha marefu ambalo linasomwa kila siku.
 
kwa hiyo kila kitu kiundiwe wizara mpaka na hawa wanavaa nusu uchi nao waundiwe wizara!
Kwa nini ujenzi imeundiwa wizara? kwa nini nishati nayo ina wizara. au niambie kwamba sanaa na utamaduni siyo vipaumbele vyetu.
Watoto wanapata elimu duni kwa sababu hatujali vya kwetu na wala hatuvithamini.
moja mbili tatu
 
tumeuza urithi wetu wa ardhini sasa tunashindwa hata kutetea urithi wetu wa vizazi vijavyo. Huyo Sr. kutokana na vyanzo vyangu vya ndani sana amejaribu kuona wenye nchi wanabadili uamuzi. Kitu ambacho sijui ni nini kimetokea. Ningependa tupate nafasi ya kumhoji huyu sista.. what happened. Wakati wengine wana tatizo kwa sababu jina la Lowassa limetokea mimi tatizo langu ni dhana nzima ya hicho kilichotokea. Kati ya maeneo yote jiji la Dar.. la Nyumba ya Sanaa ndilo lililokuwa bora.. yawezekana sista alipewa "offer she couldn't refuse"?
MM hii ishu kwa kweli inachanganya kumkichwa, nilikutana na sister miaka mitatu iliyopita, na akanigusia suala hili, sikufichi wakati anaongea machozi yalikuwa yanamtoka na kusema hana la kufanya , anamuachia mungu, nilijisikia uchungu pia, kulingana na maongezi yake, aliitaja serikali, hakutaja mtu, nahisi atakuwa ni mtu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa serikalini ndiye aliyetoa maamuzi hayo. hivyo sijui kama sister alikuwa akiigiza kuhuzunika au la!!!! na nadhani yeye ndiye anayeyajua yote haya, kama vp mnaweza kumtafuta na kuongea naye kuona ana maoni yapi, nadhani msanii atakuwa anajua jinsi ya kumpata.
 
Back
Top Bottom