Shomari
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,112
- 241
- Thread starter
- #21
Unajua jamani tusiongee kama walevi humu ndani, ndio maana hapa pakaitwa Home of Great Thinkers!kuna vitu vinanikeraga sana, eti preserve nyumba ya sanaa for heritage, usiweke mradi wa umeme kihansi, utaua vyura, usipitishe barabara kandokando ya serengeti, utabughudhi wanyama......usipofikiria sana utagundua wazungu wanatuona sisi waafrika kama makumbusho flani hata mahitaji yetu ya kibinadamu yanapimwa katika mtazamo huo.. vunja weka vitu vya maana hao vyura wa kihansi waite wazungu wakaweke huko kwao sisi tunao wakutosha, na hiyo nyumba ya sanaa inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida?vitu vyote vinapatikana slipway,makumbusho,bagamoyo hakuna sababu ya kuwa nazo kama uyoga kila sehemu.
Ukiongelea Msanii wa Kuchonga vinyago, Tingatinga na wengine wanaofanana hao ni watanzania nia wa Kawaida kabisa, au sijui ulikuwa una maana ipi? Nyumba ya Sanaa ilikuwa ya muhimu sana kwao kwa ajili ya kutangaza sanaa zao, taifa kwa ujumla, vilevile kuvumbua na kukuza wasanii wachanga, Watanzania wengi wanachukulia sanaa hasa za mikono ni jambo lisilo na umuhimu, lakini nakwambia sanaa kama ya uchoraji ina thamani yake kubwa sana katika jamii.
Katika kampeni za kikwete mwaka huu alipata kuzungumzia suala la kukuza sanaa akisema kwamba katika nchi zilizoendelea maendeleo yake huletwa na wasanii sababu ndio walipa kodi wakuu, na kwama nasi tunapaswa kuiga mfano huo kwa kuwathamini wasanii: na hivi ndivyo alivyoanza!!