Nyumba ya chumba, sebule, jiko, choo inaingia bati mita ngapi?

Nyumba ya chumba, sebule, jiko, choo inaingia bati mita ngapi?

Hao wanaokwambia MITA ni elfu 27, watakua madalali

Hiyo elfu 27 ni Bei ya Bati zima lililokamilika la MITA 3 Kwa makampuni Kama kiboko,sunshare,kinglion n.k
Hao ni alaf mkuu nimewapigia kupitia namba Yao iliyopo kwenye website Yao ndio wakaniambia hivyo mkuu
 
KWA UPAUAJI WAKISASA WA MAPAA MANNE.

Ukitaka kupata tahmini nzuri ya bati,

Pima eneo lote la nyumba Yako linalohitajika kupauliwa, including makorido na vibaraza

Katika VIPIMO vya square futi au square MITA.

Kisha gawanya Kwa square futi 144 au square MITA 16 (Kama ulipimia skwea MITA)

Ujibu utakalopata, Zidisha Kwa 12

HIZO NDIO BATI ZITAKAZOHITAJIKA KWENYE NYUMBA YAKO YOTE.

Mfano:
nyumba ya jumla square MITA 100
Itakua (100÷16)× 12= 75
Maana ake Hii nyumba itahitaji jumla ya bati 75
 
Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1

👉Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi

👉Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi

👉Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi

👉Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi

👉Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi

👉Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi

Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi

Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.

Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144

YAANI, 809÷144= 5.62

Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.

Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.
 
Anaeweza kumtag mtoa mada anisaidie,

ule Uzi WA "Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa"

Kuna vitu vingi niliandika mle, anaweza kusoma vikamsaidia kwenye ujenzi wake.

Kutype upya ni kipengele sana🙏
 
Anaeweza kumtag mtoa mada anisaidie,

ule Uzi WA "Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa"

Kuna vitu vingi niliandika mle, anaweza kusoma vikamsaidia kwenye ujenzi wake.

Kutype upya ni kipengele sana🙏
Sawa mkuu ngoja niutafute
 
Back
Top Bottom