Nyumba Mpya Zinazozwa Chanika Zinausalama Kweli?

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,123
1,921
Wakulungwa kumekuwa na matangazo ya nyumba mpya zinazouzwa Chanika, Chamazi na kwingineko kila kona sasa watu wengi sana wamekuwa na hofu wakitaka kufahamu usalama wa hizi nyumba isijekuwa kuna janja janja

JF wapo watu hapa ni wajanja wa kufahamu mambo katika jiji hili la Dar es Salaam ingekuwa vizuri mkazungumzia jambo hili kwa weledi mkubwa ili Watanzania wakajifunza jambo

Mfano wa nyumba hizo unaweza kuwa kama huu
Mara nyingi bei inaweka kuwa ndani ya ml 40
 
Attachments

  • images (2).jpeg
    images (2).jpeg
    9.1 KB · Views: 12
jenga uza izo

1. choo shimo urefu futi 4
2. mbao za kenchi za minazi isiyokomaa
3. wiring wanatumia nyaya za spika
4. mfuko mmoja wa dangote tofali mia

ingia kichwa kichwa upigwe
Ili kutaka kuthibitisha ikiwa shimo siyo futi 4, tofali ni imara na ishu kama hizo potential mteja anatakiwa kufanya nini kujiridhisha ubora?
 
Ili kutaka kuthibitisha ikiwa shimo siyo futi 4, tofali ni imara na ishu kama hizo potential mteja anatakiwa kufanya nini kujiridhisha ubora?
Bomoa sehemu ya nyumba hiyo mpya then pekecha hilo tofali.

Chukua nondo yako ya urefu wa futi sita zamisha kwenye shimo la choo jiridhishe, panda juu ya dari kagua mbao mnazi then waambie mnisamehe kwa uharibifu wowote nilioufanya lakini siwezi kununua uchafu huu.

Utakua umemaliza..
 
Wakulungwa kumekuwa na matangazo ya nyumba mpya zinazouzwa Chanika, Chamazi na kwingineko kila kona sasa watu wengi sana wamekuwa na hofu wakitaka kufahamu usalama wa hizi nyumba isijekuwa kuna janja janja

JF wapo watu hapa ni wajanja wa kufahamu mambo katika jiji hili la Dar es Salaam ingekuwa vizuri mkazungumzia jambo hili kwa weledi mkubwa ili Watanzania wakajifunza jambo

Mfano wa nyumba hizo unaweza kuwa kama huu
Bora uende ukatembelee.....ujionee na kukagua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom