Nyota wa mchezo wa MO29 na D9

Nyota wa mchezo wa MO29 na D9

Wangapi wanauponda na hawaitwi Magaidi ila Hawa ? Tuliza akili uelewe nilicho kiandika.

Shida yoyote anaye kuwa dhidi yenu mnamuita chawa, maana yake vijana hampo kwa ajili ya ukweli zaidi ya kufurahisha nafasi zenu.
sio wote mnawaita magaidi nakubari, ila, mna njia nyingi za kuwashughurikia mfano kuwapoteza, kuwatisha n.k
Mnatakiwa muandaliwe menu yenu sambamba na mtoacho.
Tunaelekea D9 nchi yetu sote tutaelewana tu,
 
IMG-20251128-WA0000.jpg
 
Maji ni kitu chenye nguvu sana!
Kamwe usijaribu kuyazuia yanapochagua njia yake, maana hutayaweza. Ukijaribu, yatakusababishia madhara makubwa!

Ni wakati wa mabadiliko… Hayazuiliki! Na kujaribu kufanya hivyo ni kujitafutia shida za kujitakia.

Nyota waliohamasisha na kufanikisha maandamano ya kudai haki ya October 29, kwa sehemu kubwa, walikuwa ni watu wa jinsia pinzani ya kiume.
Ninaposema nyota, namaanisha kwamba wapo wengi waliohusika, lakini ninaowataja hapa ni wale waliotamba zaidi.

Kutoka upande wa wanawake:
  • Mange Kimambi
  • Maria Sarungi
  • Rachel Danga
Kutoka upande wa wanaume:
  • Sativa
  • Pastor Dickson
  • Nuru Vazi
  • Pole Pole
  • Gwajima, n.k.
Kazi waliyoifanya ilionekana, na ndiyo imezaa maandamano ya awamu ya pili ya D9.

Kabla ya MO29, Pole Pole alijizolea umaarufu kutokana na kutoa data ambazo chanzo chake kilikuwa yeye mwenyewe. Watanganyika wengi waliona anawachana kisawasawa.
Mange naye akawa anapewa taarifa za ndani, na akawa anazipenyeza bila woga.

Lakini pamoja na nguvu yote hiyo, maandamano yale yakatawaliwa na kiwango kikubwa cha ukatili ulioteketeza maelfu ya roho zisizo na hatia — pamoja na majeruhi, makovu na ulemavu wa kila aina.

Hata hivyo, matakwa ya MO29 hayakutekelezwa.
Hii ikapelekea maandalizi ya maandamano ya D9, siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Maandalizi ya D9, pamoja na wale nyota wa MO29, yamemuibua mtu mpya kabisa mahiri, mwenye nguvu, na hatari zaidi.

Huyu mtu ni kama jeshi la mtu mmoja, aliye full loaded kwa kila aina ya silaha kubwa na ndogo, za masafa marefu na mafupi.
Na huyu si mwingine bali ni:

Habil Kabil
  • Bingwa wa mipango na mifumo
  • Mtu mwenye ushawishi wa ajabu
  • Mdukuzi hatari
  • Anayedukua kila kitu, kidogo au kikubwa — na kila alichonacho ni silaha kuelekea D9
  • Kwa sasa, ndiye mtu anayesikilizwa zaidi Tanganyika kwenye live talks mitandaoni
Ana ufahamu wa kila jambo na huwasilisha mikakati yake kwa lugha nyepesi.
Ana mbinu za kipekee za kuwasiliana na wale wanaowekwa kwenye rada yake:
  1. Email
  2. Barua/Fax
  3. Simu
  4. Live talks mitandaoni
Kwa kila njia, anahakikisha hakuna nafasi ya visingizio.
Na mara zote anakupa chaguzi mbili tu: A au B.

Kila analoibuka nalo linatisha kuliko lililotangulia. Kwa sasa, watu hawalali hawajui nani ndiye anayefuata na atawekewa ultimatum gani.

Wengi wangetamani wasahauliwe mpaka D9 ifike… lakini kwa hali ilivyo sasa, inaonekana hakuna atakayebaki. Kila mmoja ataandikiwa wakati wake.

Jana, mbali na taasisi iliyoguswa kwa sehemu, ni Bwana Subwoofer aliyeibuliwa na kashfa ya kughushi na amepewa ultimatum ya siku 7 ajitafakari na kujibu.
Tundu Lissu japo hajaonekana front lakini movement yake ya NRNE imechangia kwa zaid ya 50% ndugu mchambuzi hujamtendea haki kabisa
 
Kwanini watu sio waadilifu katika uandishi ? Hivi kwa maana ipi au kwa sababu ipi mnayaita yale ya October 29 ni maandamano ?

Kingine, kwa sababu ipi na kwa maana ipi watu wahamasishaji juu ya vurugu na uasi mnawaita nyota ya mchezo au watu mahiri, na kuacha kuwaita kwa majina yao stahiki kama vile Mafatani, Wazandiki, Magaidi, Wahaini na mfano wa hayo ?

Kwanini hamjipambi na sifa ya ukweli pamoja na uadilifu ?

Kwetu sisi kiimani, tunasema lazima mtaulizwa, na lazima mtalipwa stahiki zenu mbele ya Mola mlezi.
Wewe na serikali Yako ya CCM yaite mtakavyo,ila wanachi na nchi za nje yakiwemo mabeberu hayo yalikuwa maandamano
 
Hiki nini umeweka ? Nataka hoja za wazi na ubainifu.

Kanuni kutoka mbinguni ni kuwa mkiona viongozi wenu ni mafisadi, waovu basi na raia mna tabia hizo hizo.

Swali la msingi ni kuwa, viongozi wanalo kosea na nyinyi raia ndio mkosee na kufanya uharibifu ?

Mna tabia za kinafiki sana, mnakemea uovu kwa upande mmoja na kusahau maovu yaliyo fanywa na raia. Uadilifu uko wapi ? Huu uozo ndio wanao ishi nao TEC.
Hoja za wazi na ubainifu anazo Samia the butcher aliyeua vijana na wazazi wetu,anayo kazi this time
 
Issue ya Habil inatoa funzo kubwa sana kama taifa.

Ila kwakuwa CCM na TISS wamejaa mapunguani hawajaona tatizo.

Vijana watanzania wako Tayari kumsikiliza mtu yoyote atakaye wapa matumaini na kuwaelezea mabaya ya Serikali, kama TAIFA hili jambo ni hatari sana ..
Sasa misukule imejificha huko ikihondomola mali za watanzania ikiongozwa na chura Gen Z ndo wameamka hivyo hakuna kupoa
 
Wewe na serikali Yako ya CCM yaite mtakavyo,ila wanachi na nchi za nje yakiwemo mabeberu hayo yalikuwa maandamano
Hii haibadilishi ya kuwa zile zilikuwa ni vurugu, uasi, ugaidi na uzandiki.
 
Hoja za wazi na ubainifu anazo Samia the butcher aliyeua vijana na wazazi wetu,anayo kazi this time
Ajabu nyinyi nyote mlio kwenye mrengo huo, hamna hoja wala kuteteanachokidai.

Hii ni ajabu sana.
 
Back
Top Bottom