Nyota wa mchezo wa MO29 na D9

Nyota wa mchezo wa MO29 na D9

Maji ni kitu chenye nguvu sana!
Kamwe usijaribu kuyazuia yanapochagua njia yake, maana hutayaweza. Ukijaribu, yatakusababishia madhara makubwa!

Ni wakati wa mabadiliko… Hayazuiliki! Na kujaribu kufanya hivyo ni kujitafutia shida za kujitakia.

Nyota waliohamasisha na kufanikisha maandamano ya kudai haki ya October 29, kwa sehemu kubwa, walikuwa ni watu wa jinsia pinzani ya kiume.
Ninaposema nyota, namaanisha kwamba wapo wengi waliohusika, lakini ninaowataja hapa ni wale waliotamba zaidi.

Kutoka upande wa wanawake:
  • Mange Kimambi
  • Maria Sarungi
  • Rachel Danga
Kutoka upande wa wanaume:
  • Sativa
  • Pastor Dickson
  • Nuru Vazi
  • Pole Pole
  • Gwajima, n.k.
Kazi waliyoifanya ilionekana, na ndiyo imezaa maandamano ya awamu ya pili ya D9.

Kabla ya MO29, Pole Pole alijizolea umaarufu kutokana na kutoa data ambazo chanzo chake kilikuwa yeye mwenyewe. Watanganyika wengi waliona anawachana kisawasawa.
Mange naye akawa anapewa taarifa za ndani, na akawa anazipenyeza bila woga.

Lakini pamoja na nguvu yote hiyo, maandamano yale yakatawaliwa na kiwango kikubwa cha ukatili ulioteketeza maelfu ya roho zisizo na hatia — pamoja na majeruhi, makovu na ulemavu wa kila aina.

Hata hivyo, matakwa ya MO29 hayakutekelezwa.
Hii ikapelekea maandalizi ya maandamano ya D9, siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Maandalizi ya D9, pamoja na wale nyota wa MO29, yamemuibua mtu mpya kabisa mahiri, mwenye nguvu, na hatari zaidi.

Huyu mtu ni kama jeshi la mtu mmoja, aliye full loaded kwa kila aina ya silaha kubwa na ndogo, za masafa marefu na mafupi.
Na huyu si mwingine bali ni:

Habil Kabil
  • Bingwa wa mipango na mifumo
  • Mtu mwenye ushawishi wa ajabu
  • Mdukuzi hatari
  • Anayedukua kila kitu, kidogo au kikubwa — na kila alichonacho ni silaha kuelekea D9
  • Kwa sasa, ndiye mtu anayesikilizwa zaidi Tanganyika kwenye live talks mitandaoni
Ana ufahamu wa kila jambo na huwasilisha mikakati yake kwa lugha nyepesi.
Ana mbinu za kipekee za kuwasiliana na wale wanaowekwa kwenye rada yake:
  1. Email
  2. Barua/Fax
  3. Simu
  4. Live talks mitandaoni
Kwa kila njia, anahakikisha hakuna nafasi ya visingizio.
Na mara zote anakupa chaguzi mbili tu: A au B.

Kila analoibuka nalo linatisha kuliko lililotangulia. Kwa sasa, watu hawalali hawajui nani ndiye anayefuata na atawekewa ultimatum gani.

Wengi wangetamani wasahauliwe mpaka D9 ifike… lakini kwa hali ilivyo sasa, inaonekana hakuna atakayebaki. Kila mmoja ataandikiwa wakati wake.

Jana, mbali na taasisi iliyoguswa kwa sehemu, ni Bwana Subwoofer aliyeibuliwa na kashfa ya kughushi na amepewa ultimatum ya siku 7 ajitafakari na kujibu.
Kwanini watu sio waadilifu katika uandishi ? Hivi kwa maana ipi au kwa sababu ipi mnayaita yale ya October 29 ni maandamano ?

Kingine, kwa sababu ipi na kwa maana ipi watu wahamasishaji juu ya vurugu na uasi mnawaita nyota ya mchezo au watu mahiri, na kuacha kuwaita kwa majina yao stahiki kama vile Mafatani, Wazandiki, Magaidi, Wahaini na mfano wa hayo ?

Kwanini hamjipambi na sifa ya ukweli pamoja na uadilifu ?

Kwetu sisi kiimani, tunasema lazima mtaulizwa, na lazima mtalipwa stahiki zenu mbele ya Mola mlezi.
 
Hivi mnajua mnachezewa saikolojia na hamtaki kuamini
Je Yale yote anayowaeleza hyo pungasese wenu lipi lililoleta impact chanya katika jamii kuachana na huo umbea wa vijiweni
Siku Moja mwambieni a test hyo mifumo yake ili muhakikishe kile anachowaeleza
Anawalisha matangopoli na nyie mnaamimin et mmepata mtu wa kuwatetea
Tumien vizuri akili vinginevyo ataendelea kuwaona mazwazwa
 
Njoo na account yako tunayoijua, unaogopa nn?
 
Kwanini watu sio waadilifu katika uandishi ? Hivi kwa maana ipi au kwa sababu ipi mnayaita yale ya October 29 ni maandamano ?

Kingine, kwa sababu ipi na kwa maana ipi watu wahamasishaji juu ya vurugu na uasi mnawaita nyota ya mchezo au watu mahiri, na kuacha kuwaita kwa majina yao stahiki kama vile Mafatani, Wazandiki, Magaidi, Wahaini na mfano wa hayo ?

Kwanini hamjipambi na sifa ya ukweli pamoja na uadilifu ?

Kwetu sisi kiimani, tunasema lazima mtaulizwa, na lazima mtalipwa stahiki zenu mbele ya Mola mlezi.
Kwahiyo hawa wanaoteka watu na kuua, wanaotumia mali za umma vibaya, wanaoharibu uchaguzi kwa kuwafunga wapinzani na kuiba kura wapo sahihi?
 
Kwanza kubali ya kuwa kilichofanywa na raia ni uasi, ugaidi, uzandiki, ufisadi na uharibifu.

Kwahiyo unataka kuniambia watawala wanapokosea suluhu ni kufanya uasi ? Uvunjifu wa amani ?
 
Maji ni kitu chenye nguvu sana!
Kamwe usijaribu kuyazuia yanapochagua njia yake, maana hutayaweza. Ukijaribu, yatakusababishia madhara makubwa!

Ni wakati wa mabadiliko… Hayazuiliki! Na kujaribu kufanya hivyo ni kujitafutia shida za kujitakia.

Nyota waliohamasisha na kufanikisha maandamano ya kudai haki ya October 29, kwa sehemu kubwa, walikuwa ni watu wa jinsia pinzani ya kiume.
Ninaposema nyota, namaanisha kwamba wapo wengi waliohusika, lakini ninaowataja hapa ni wale waliotamba zaidi.

Kutoka upande wa wanawake:
  • Mange Kimambi
  • Maria Sarungi
  • Rachel Danga
Kutoka upande wa wanaume:
  • Sativa
  • Pastor Dickson
  • Nuru Vazi
  • Pole Pole
  • Gwajima, n.k.
Kazi waliyoifanya ilionekana, na ndiyo imezaa maandamano ya awamu ya pili ya D9.

Kabla ya MO29, Pole Pole alijizolea umaarufu kutokana na kutoa data ambazo chanzo chake kilikuwa yeye mwenyewe. Watanganyika wengi waliona anawachana kisawasawa.
Mange naye akawa anapewa taarifa za ndani, na akawa anazipenyeza bila woga.

Lakini pamoja na nguvu yote hiyo, maandamano yale yakatawaliwa na kiwango kikubwa cha ukatili ulioteketeza maelfu ya roho zisizo na hatia — pamoja na majeruhi, makovu na ulemavu wa kila aina.

Hata hivyo, matakwa ya MO29 hayakutekelezwa.
Hii ikapelekea maandalizi ya maandamano ya D9, siku ya Uhuru wa Tanganyika.

Maandalizi ya D9, pamoja na wale nyota wa MO29, yamemuibua mtu mpya kabisa mahiri, mwenye nguvu, na hatari zaidi.

Huyu mtu ni kama jeshi la mtu mmoja, aliye full loaded kwa kila aina ya silaha kubwa na ndogo, za masafa marefu na mafupi.
Na huyu si mwingine bali ni:

Habil Kabil
  • Bingwa wa mipango na mifumo
  • Mtu mwenye ushawishi wa ajabu
  • Mdukuzi hatari
  • Anayedukua kila kitu, kidogo au kikubwa — na kila alichonacho ni silaha kuelekea D9
  • Kwa sasa, ndiye mtu anayesikilizwa zaidi Tanganyika kwenye live talks mitandaoni
Ana ufahamu wa kila jambo na huwasilisha mikakati yake kwa lugha nyepesi.
Ana mbinu za kipekee za kuwasiliana na wale wanaowekwa kwenye rada yake:
  1. Email
  2. Barua/Fax
  3. Simu
  4. Live talks mitandaoni
Kwa kila njia, anahakikisha hakuna nafasi ya visingizio.
Na mara zote anakupa chaguzi mbili tu: A au B.

Kila analoibuka nalo linatisha kuliko lililotangulia. Kwa sasa, watu hawalali hawajui nani ndiye anayefuata na atawekewa ultimatum gani.

Wengi wangetamani wasahauliwe mpaka D9 ifike… lakini kwa hali ilivyo sasa, inaonekana hakuna atakayebaki. Kila mmoja ataandikiwa wakati wake.

Jana, mbali na taasisi iliyoguswa kwa sehemu, ni Bwana Subwoofer aliyeibuliwa na kashfa ya kughushi na amepewa ultimatum ya siku 7 ajitafakari na kujibu.
Umemsahau mtambo wa matusi Rachel Dangwa😊
 
Wabongo bwana kwa kuchotwa akili.. nimemsikiliza shujaa wao Habili akizungumzia NATO na pengine uwezekano wa wao kuingilia hali hii. Nikagundua mshikaji ameamua kuwachota mburula. Ajabu ni kwamba mburula wa kiTZ wanamkubali Ile mbaya!
Nb. Ukitoka hiyo siku aga vizuri kwenu.
 
Issue ya Habil inatoa funzo kubwa sana kama taifa.

Ila kwakuwa CCM na TISS wamejaa mapunguani hawajaona tatizo.

Vijana watanzania wako Tayari kumsikiliza mtu yoyote atakaye wapa matumaini na kuwaelezea mabaya ya Serikali, kama TAIFA hili jambo ni hatari sana ..
Hao wamevimbewa rushwa na maposho haramu, hawawezi ona chochote chenye tija Kwa taifa
 
Hiki nini umeweka ? Nataka hoja za wazi na ubainifu.

Kanuni kutoka mbinguni ni kuwa mkiona viongozi wenu ni mafisadi, waovu basi na raia mna tabia hizo hizo.

Swali la msingi ni kuwa, viongozi wanalo kosea na nyinyi raia ndio mkosee na kufanya uharibifu ?

Mna tabia za kinafiki sana, mnakemea uovu kwa upande mmoja na kusahau maovu yaliyo fanywa na raia. Uadilifu uko wapi ? Huu uozo ndio wanao ishi nao TEC.
 
Shida Wabongo ni vichwa mchunga sana.
Wabongo bwana kwa kuchotwa akili.. nimemsikiliza shujaa wao Habili akizungumzia NATO na pengine uwezekano wa wao kuingilia hali hii. Nikagundua mshikaji ameamua kuwachota mburula. Ajabu ni kwamba mburula wa kiTZ wanamkubali Ile mbaya!
Nb. Ukitoka hiyo siku aga vizuri kwenu.
 
policcm kwa upeo wao wanampakazia sio mtu ni mashine ya AI.
Katoa picha yake mtandaoni kukanusha hilo. Ni kijana GenZ wa bongo aliekulia nje na kukoza rafuzi ya kibongo, ila ni Mtanzania wa kuzaliwa bongo. Sasa nasikia mbwa mteule anaanza kuamisha magori, eti kuna mataifa wananyemelea utajiri wetu. Wahuni hawawaoni? najiuliza
Utajiri gani tena maana aliponyimwa misaada alisema Nchi ina rasilimali chache!!!

Halafu maji anaagiza USA
 
s-l1200 (2).webp
s-l1200 (1).webp
s-l1200.webp
 
Back
Top Bottom