Nyomi hii - Mubarak bye bye!!!!!!!!!!!!!!!!!

kwanini na sisi tusijipange kwani matatizo yao na Tanzania hayatofautiani,kusekana ajira,gharama za maisha kupanda,kutokuwa na demokrasia ya kweli.....
tuna kila sababu ya kufanya mabadiliko

mbona sisi yamezidi; ilitakiwa tuwe tumetangulia wao wanafuata, ile ya Arusha ilikuwa sababu tosha kumaliza udhia
 
Apo ingekuwa Tz askali wangekuwa washaua watu kama elfu ivi.
Polisi na wanajeshi wetu inabidi muwe mnakodolea macho Tv kuna vya kujifunza apo.
Sio kazi yenu kupiga tuu
 
Hawa marais wetu sijui vichwa maji au nini, we raia hawakutaki umekazana tu kuwatawala? Its a matter of tym jamaa atanyanyuka tu!
 
Eee bwana ee!! hii inanikumbusha enzi za Mtikila na sera za UZAWA. Lakini ilikuwa tukiona polisi kila mtu anapotelea njia yake!
 
Mungu aepushie mbali huu mwamko usije Tanzania maana utaweza kuiondoa hii amani tuliyo irithi, Tumuache Kikwete atulie ale nchi na akina Rostam tartiiiibu huku wananchi tukihangaika na ya fuatayo.

1.Vifo mahosptalini vinavyoweza kuzuilika
2.Foleni mabarabarani
3.Mfumuko wa bei
4.Kukosa kazi hivyo kuzalisha vibaka
5.Wizi wa kodi zetu
6.Ukosefu wa maji safi na ya uhakika
Mkuu hayo uloyasema hapo ndo chanzo cha kufanikisha mwamuko wa mageuzi ambao unaomba mungu auepushe.
 
..waandamanaji wanaonekana wamevaa vizuri kuliko mwananchi wa kawaida wa Tanzania.

..pia nawaona kama wana afya na lishe nzuri kushinda wa-Tanzania wengi ninaowaona mijini na vijijini.

..maeneo wanayoandamana yanaonekana kuwa ni masafi na yenye mpangilio kuliko miji mikubwa ya Tanzania.

..tofauti ni kwamba wa-Tanzania tumeridhika, wakati wa-Misri hawajaridhika!!!
 
Mungu aepushie mbali huu mwamko usije Tanzania maana utaweza kuiondoa hii amani tuliyo irithi, Tumuache Kikwete atulie ale nchi na akina Rostam tartiiiibu huku wananchi tukihangaika na ya fuatayo.

1.Vifo mahosptalini vinavyoweza kuzuilika
2.Foleni mabarabarani
3.Mfumuko wa bei
4.Kukosa kazi hivyo kuzalisha vibaka
5.Wizi wa kodi zetu
6.Ukosefu wa maji safi na ya uhakika

Tusubiri tu Mubaraak aking'oka tu tulianzishe na sisi hapa bongo au mnasemaje wadau!
 
To preserve piece people like to be feeling that they have been uleashed and not coerced under the tyranny governments. Kinachotokea Egypt ni kati ya Army na Raia ni uwepo wa international media ambazo zinaangalia kwa karibu movement zote hasa ukizingatia kuwa jeshi hilo linapata $1.2billion of aid from USA ambao wametamka wazi kuwa hawataki kuona matumizi ya nguvu dhidi ya raia. Sisi misaada yetu inatoka China ambako kila siku wananyongwa watu si chini ya 50 kwa makosa mbalimbali, unatarajia nini hapo?.

Watu wanaandamana kutoka Mount meru hotel kuelekea NMC mnawaua je kama wote wakiwa tayari kufa mtaua wangapi?. Serikali dhalimu kila siku huhofia watu wake. Kitendo cha jeshi la misri ni cha kuigwa duniani kote kuwa kazi ya vyombo vya ulinzi ni kulinda raia si kuwaadhibu na kuwaua kama ambavyo akili za viongozi wetu wa bongo zinavyowaza. "Utasikia andamane mtaona cha mtema kuni" - Haya ni maneno ya kumwambia mkeo na familia yako siyo watu wanaokulipa mshahara kwa kodi zao.

Ifikie wakati sasa watawala wajue kuwa kuongoza si tu kuwa na escot na kuzuia wengine kutumia barabara masaa mawili kabla yako, bali ni kazi ngumu inayotaka commitment from the heart na ujasili mkubwa wa kutoogopa kupoteza marafiki mafisadi wachache kwa ajili ya utawi wa walio wengi.
 
Dah, ukifikiria kuiachia ikulu kwa staili hii ya Mubarak unafeelaje? Ikulu tam banaaa, huhangaiki na visa wala nn we unakuta kila ki2 kishaandaliwa ah acha 2.
 
Mubarak kisha lainika. Ataitisha uchaguzi mwezi wa 9 na yeye hatagombea!! Source CNN
 
Bongo haiwezi tokea sababu ASKARI WETU WAKO BRAIN WASHED!:msela:
Wao kila kitu NDIO AFANDE

USITEGEMEE HATA SIKU MOJA BONDO KUWA HIVI.

PIA WATU NI WAOGA KUPITA KUNGURU SASA UNATEGEMEA WATAJITOKEZA NA KUKAA MTAANI WIKI NZIMA?

WACHACHE SANA WENYE UJASIRI KM HUO NA HII NDIO INADHOOFISHA NGUVU YA UMMA HAPA TZ.
mimi naamini iko siku watu wataweka uoga pembeni amini usi amini na si mda mrefu.....kama CCM itaindelea na us**** huu..............
 
Back
Top Bottom