Nyoka wa ajabu

Nyoka wa ajabu

Mambo yote ambayo yanamchukiza muumba kwa mfano wewe unaenda msikitini au kanisani kwa ajili tu umeambiwa na mshirikina uende kwenye nyumba za ibada ili mambo yako yanyooke hapo umeenda si kwa ajili ya mungu ila kwa ajili unashida fulani hapo utakuwa mshirikina Ingawa unaingia kwenye nyumba ya ibada
kumbe mshirikina anaweza kukupa ushauri wa kwenda msikitini au kanisani?... ni upendo ulioje wa namna hii?, sasa kwanini mashehe na wachungaji wanabania waumini kwenda kwa washirikina?
 
Mambo yote ambayo yanamchukiza muumba kwa mfano wewe unaenda msikitini au kanisani kwa ajili tu umeambiwa na mshirikina uende kwenye nyumba za ibada ili mambo yako yanyooke hapo umeenda si kwa ajili ya mungu ila kwa ajili unashida fulani hapo utakuwa mshirikina Ingawa unaingia kwenye nyumba ya ibada
Kwahiyo ukifanya hayo ndio unaota umegeuka kuwa nyoka?
 
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?

Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
We utakuwa ulikuwa una 'Ota' sio bore!!!
 
Nafikiri mshana jr alikupitia kukusalimu au mwenziwe MziziMkavu, si unajuwa wale wanapenda sana kuhamsha watanzania wavivu wanaopenda kulala muda wa kazi. Usihofu, walikuwa wanakukumbushia tu wajibu wako kwa taifa letu. In short, wanakupenda maana kama si hivyo, wangekukaba pumzi na umauti ungekukuta hapo kwenye hiko kiti.
Sawa lakini jana ulikuwa siku ya mapumziko
 
Mkuu kutubu dhambi ni kama kupewa dhamana tu ama kuachiwa kwa utaratibu wa Parole wa kifungo cha nje ila suala la kwamba umeshahukumiwa liko pale pale!
Sasa una maanisha nini hapo?
 
Sasa nimekupata je wewe unaamini katika ndoto au maono
Huwa sifatishi ndoto kabisa, na huwa naota vitu vingi tu lakini napuuzia, hiyo ilinishangaza kwavile ilikuwa mchana halafu tofauti na ndoto zingine hiyo nimeota kama ninmebadilika na kuwa nyoka, na pia niliweka bayana kuwa lengo la huu uzi sio tu kuambiwa ndoto hiyo ina maana gani tu, bali pia nilipenda kwenda deep zaidi ili nipate kufahamu kama mimi ni binadamu mwenye mawazo ya nyoka au Nyoka mwenye mawazo ya kuwa binadamu au ni vipi?
 
Ebu tuone picha yako ulivyokuwa nyoka na ukiwa binadamu then tujaji unafananaje zaidi.
 
Ebu tuone picha yako ulivyokuwa nyoka na ukiwa binadamu then tujaji unafananaje zaidi.
Lengo la uzi huu haikuwa kujua nafananaje vinginevyo ningetumia kioo tu
Hebu jaribu kusoma tena kisha ndo urudi kuchangia mada
 
Back
Top Bottom