Nyoka wa ajabu

Nyoka wa ajabu

nilivyo elewa mimi ni kwamba akiwa juu ya mti anaona ni kunguru lakini akiwa chini anaona ni njiwa... na ni kama mara mbili hivi alihakiki hivyo...

Lakini swali la msingi anataka kujua je yeye ni nyoka anayeota/kuwaza kuwa binadamu? au ni binadamu anayewaza/kuota kuwa nyoka?....
na pia sidhani kama shida yake ni kujua hii ndoto inamaanisha nini, yawezekana sio mtilia maanani wa tafsiri za ndoto!...

Samahani nataka kujua victim wa hii kesi ambaye ni mlalamikaji wa kwanza ndugu Jimena athibitishe kwamba yeye wakati wa tukio tajwa alikuwa ni nyoka aliyebadilika kuwa binadamu ama ni binadamu aliyebadilika kuwa nyoka na ikiwezekana alete ushahidi tawi moja la mti aalioutaja sambamba na njiwa mmoja na kunguru mmoja wanaotajwa kwenye kesi yake kama vielelezo!
 
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?

Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili
du, mkuu hii ndoto yako ni kali sana...naomba uwahi maombi kwa askofu gwajima akuondolee mapepo mwilini mwako....hilo litakuwa pepo linakusumbua.
 
Tukifuata maandiko ya vitabu vitukufu vya Mwenezi Mungu tunaambiwa kuanzia siku unazaliwa ratiba yako imeshaandaliwa hadi mwisho baada ya kumaliza maisha haya kwenda kupangiwa kazi nyingine...kwa muktadha huu ukipadilika ni bure tu maana mwenyewe mkuu Mbinguni keshakuweka reserve!
ina maana mkuu,hakuna dhambi wa kutubu kwa Mungu
 
nilivyo elewa mimi ni kwamba akiwa juu ya mti anaona ni kunguru lakini akiwa chini anaona ni njiwa... na ni kama mara mbili hivi alihakiki hivyo...

Lakini swali la msingi anataka kujua je yeye ni nyoka anayeota/kuwaza kuwa binadamu? au ni binadamu anayewaza/kuota kuwa nyoka?....
na pia sidhani kama shida yake ni kujua hii ndoto inamaanisha nini, yawezekana sio mtilia maanani wa tafsiri za ndoto!...
Uko sahihi kabisa mkuu
 
uwiii unaamini ndoto
wewe ndoto inakupa MAWAZO !!
hivi ni kweli wanasayansi mpk leo wameshindwa king'amua ndoto ni nini hasa

sasa nitaanzaje kukushauri wewe mungu humjui na hukubari uwepo majini kwako ni story za kutunga
7BU ndoto kama hizo hushabiiana na maswara ya kiroho yenye kumuhusisha mungu na viumbe vyake visivyoonekana kawaida
eti ?
 
Anyway labda itakua ina maana fulani, kutafsiri ndoto kunahitaji elimu yake. Ukiota nyoka maana yake ni ADUI au UBAYA me naweza kusema labda wewe upo katika namna fulani ambayo sio NZURI au SAHIHI na pengine unatarajia kupata kitu fulani au matokeo fulani huyatakayo lakini kumbe ni tofauti na hali halisi
Asante.

Kwahiyo we uonavyo maswala ya mimi kuwa nyoka au nyoka kuwa mimi sio ya ukweli bali tu kuna mipango yangu ambayo itafeli?
 
Habari za mda huu wana JF

Siku ya leo mapema tuu mchana kwenye saa saba wakati napitia posts mbali mbali hapa jamvini nilijikuta nimepitiwa na usingizi wa ghafla.

Na kujikuta nipo mazingira ambayo sijawahi kuyaona, na nilikuwa katika umbo la nyoka kimwili na mawazo pia, hilo halikunishangaza sana kwa sababu nilijiona kuwa mimi ni nyoka na niliona hayo ndio maisha yangu ya siku zote kama nyoka wengine,

Lakini ghafla kulitokea na njiwa wawili waliotua mbele yangu juu ya mti ulio mfano wa miti ile ya Crismass, nami nikaanza kuupanda ule mti kwa taratibu na busara kwa lengo la kuwakamata wale njiwa ili niwale...

Cha ajabu nilipofika juu na kuwakaribia nikagundua kuwa wale sio njiwa ila ni kunguru, na mimi kama nyoka nilikuwa sina tabia ya kula kunguru hivyo niliamua kushuka chini bila kuwabugudhi niendelee na mambo mengine lakini nilipofika chini na kutazama tena juu ya ule mti niliwaona kuwa ni njiwa na wala si kunguru kama nilivyofikiri hapo mwanzo, kwa mara ya pili niliamua kurudi tena juu ya mti ili niwakamate, ila nilipofika juu niliwaona ni kunguru na wala sio njiwa, hichi kitu kilinishangaza sana, maana nikiwa chini nawaona kama njiwa lakini nikiwa juu nawaona kama kunguru...

Wakati nipo katika dimbi la mawazo nisijue nini cha kufanya mara ghafla chini ya ule mti alipita sungura...

Hapo sasa nikaachana na habari ya wale njiwa/kunguru na kuanza kumfukuza yule sungura,

Ghafla nikashituka maana nilikuwa naamshwa ili nile chakula cha mchana na nilipongalia saa ilikuwa ni saa saba na dakika ishirini na tano mchana

Shida yangu hapa sio tu kutaka kujua hii ndoto inamaanisha nini Ila nikukutaka kujua mimi ni nani?

Je mimi ni binadamu ambaye nawaza/kuota kuwa nyoka au ni nyoka ambaye anawaza/kuota kuwa binadamu???

Na je maisha yangu na ufahamu wangu kwa sasa upo wapi?
Ni kwa nyoka au binadamu?
Na ni yapi ni maisha yangu ya kweli ninayoishi sasa kati ya nyoka au binadamu?

Cc Appolo Annael Bennie 369 Mkuu wa chuo aretasludovick pamoja na wengine wote ambao mna ufahamu kuhusu haya maswala naomba ufafanuzi wenu maana naona muda unapita bila mimi kupata ufumbuzi kwenye hili

Nafikiri mshana jr alikupitia kukusalimu au mwenziwe MziziMkavu, si unajuwa wale wanapenda sana kuhamsha watanzania wavivu wanaopenda kulala muda wa kazi. Usihofu, walikuwa wanakukumbushia tu wajibu wako kwa taifa letu. In short, wanakupenda maana kama si hivyo, wangekukaba pumzi na umauti ungekukuta hapo kwenye hiko kiti.
 
Nimejikuta nacheka peke yangu. Mkuu angalia isije ikawa unataka kupata malaria kweli, unajua ungeuliza ndoto ina maana gani ningekuelewa, ila unapouliza wewe ni nani ndio hapo umeniacha hoi. Wewe si binadamu au? ungekuwa nyoka ungeweza kweli hata kuja humu JF?
NIMECHOKA UJUE HATA MIE
 
Binafsi huwa siamin hizo mambo za ndoto.. Nishaota sana cjui nipo vitani,cjui nipo marekani,cjui nakimbizwa na mbwa mara nakimbizwa na nyoka, mara hiki cjui nakula mijusi..kiujumla we fanya kupotezea tu hizo mambo.. Kama unaamin kwenye masuala ya kidini fanya maombi/dua kama unaamin kwenye uganga nenda kapige ndumba kidogo na kama ni huamin uwepo wa Mungu endelea kula bata..
Wewe ni wewe na utabaki kua ww, forget about nyoka dreams...

Asante sana acha nile bata tu maana hamna namna sasa
 
Samahani nataka kujua victim wa hii kesi ambaye ni mlalamikaji wa kwanza ndugu Jimena athibitishe kwamba yeye wakati wa tukio tajwa alikuwa ni nyoka aliyebadilika kuwa binadamu ama ni binadamu aliyebadilika kuwa nyoka na ikiwezekana alete ushahidi tawi moja la mti aalioutaja sambamba na njiwa mmoja na kunguru mmoja wanaotajwa kwenye kesi yake kama vielelezo!
Avilete akiwa kama Jimena, au avilete akiwa kama nyoka?
 
Lazima itakuwa alihusisha, ndoto ya nyoka ni uadui, ila sasa kunguru wakawa wanamsaidia, kwa sababu angejua tangu chini wale ni kunguru asingepanda juu,lakini walikuwa wanaonekana njiwa, akipanda wanakuwa kunguru, ndio ikawa heri kwake
Kama naanza kukuelewa vile
Cc Bennie 369 hebu pitia hapa
 
Asante.

Kwahiyo we uonavyo maswala ya mimi kuwa nyoka au nyoka kuwa mimi sio ya ukweli bali tu kuna mipango yangu ambayo itafeli?
Bila shaka wewe ni binadam kamili labda ungekua na uwezo wakimiujiza zaidi ningekutilia shaka. Hiyo ni ndoto tu inamaana fulani, ondoa imani ya wewe si mtu
 
Samahani nataka kujua victim wa hii kesi ambaye ni mlalamikaji wa kwanza ndugu Jimena athibitishe kwamba yeye wakati wa tukio tajwa alikuwa ni nyoka aliyebadilika kuwa binadamu ama ni binadamu aliyebadilika kuwa nyoka na ikiwezekana alete ushahidi tawi moja la mti aalioutaja sambamba na njiwa mmoja na kunguru mmoja wanaotajwa kwenye kesi yake kama vielelezo!
Sio tu kwamba sina tawi la mti bali hata eneo ambalo ndoto imetokea silifahamu zaidi ya kushtuka tu nilipoamshwa nile
 
Back
Top Bottom