Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

Nyerere: Salaam zenu mnaomkejeli!

FF
Unajuwa hawa jamaa hata Halloween wameshaanza kusherehekea hapa TZ. Baadaye watasema iwe sikukuu ya kitaifa!! Halafu wakiulizwa kwa nini mnashereheka? watesema mbona nchi nyengine duniani za ... zinasherehekea!!
Nimeishasema mimi sio madhehebu ya kikiristo. Chunga sana, dogo!
 
Lugha zako si njema, mara "dogo", mara "bi mdogo", mara mwanamke. Hivi unanini wewe? hicho katika Uislaam kinaitwa "Kibri" au (kujitukuza) na kuona wengine mradi tu wapowapo na hawana hadhi kama yako. Wewe unasema si madhehebu ya Kikiristo lakini kama ni Muislaam inabidi ujirekebishe sana kwa faida yako.
Usitake kunifundisha. Kutokuwa Mkristo hakuna maana ni lazima uwe Mwislamu. Vipi wewe, mbona mwangalio wako finyu sana? Bado ninakungoja unijibu hoja. Mbona unazidi kuzunguka mbuyu, bi mdogo, yamekushinda sio?
 
Wengi tu hatutamuita nyerere baba, watoto wetu hawatamuita, wala ukoo wetu kwasababu ni mafundisho nje kabisa ya kidini..

We have to agree to differ BIG TIME
 
Looh hata link hujaiona? na hapo si kukuambia Muislaam soma vizuri. "kama" hujaiona; kama link hujaiona basi unamatatizo ya kuona rudi tena hapo juu kidogo, na sasa pokea hii article itakusaidia ufaham wako, vipi Kiingereza kinapanda kidogo au Kiarabu?: Saudi Female Bloggers Meeting in Riyadh « American Bedu
Duhu, mwa'netu huna hata haya? Nakuambia hata Lisa Miedah Valentine (huyo uliyemuibia sura kwenye avatar yako) sidhani kama ana mawazo potofu pia na uongo kama wako!
 
Kwaaaaakwkakwkaaaaakwa, umenifanya nicheke sana, pole sana naomba soma kuhusu "The kunyah (الكني&#1577😉" au "nick name". Usikurupuke. Sikisii.QUOTE]


Soma Quran Surat : Al-Hujurat ayat 12

[/49:12] O ye who believe! let not one people deride another people, who may be better than they, nor let women deride other women, who may be better than they. And defame not your own people, nor call one another by nicknames. Bad indeed is evil reputation after the profession of belief; and those who repent not are the wrongdoers.

Turudi kwenye Maana ya hiyo nick name ya Foxy
1.Sexually appealing/attractive
2.one hot spunky piece of ass, who is just perfect for *******ng
Kwa ujumla Mama Faiza hilo Foxy si sahihi kwa binti wa Kiislamu kulitumia ndio maana niliwahi kukwambia tafuta ustaadh wako ajaribu kukupa darsa, na hapa siongelei utamaduni wa kiarabu, naongelea kanuni na taratibu za Kiislam; umeweka link Arab google weka ya Kiislamu ndiyo ninayoitaka.

Chama
Gongo la Mboto DSM


 
Kwa ujumla Mama Faiza hilo Foxy si sahihi kwa binti wa Kiislamu kulitumia ndio maana niliwahi kukwambia tafuta ustaadh wako ajaribu kukupa darsa, na hapa siongelei utamaduni wa kiarabu, naongelea kanuni na taratibu za Kiislam; umeweka link Arab google weka ya Kiislamu ndiyo ninayoitaka.
Asante chama kwa kuliona hilo. Ndo maana namwambia FaizaFoxy amezidi uongo. Kwanza hiyo search ya arab forums kwenye Google haithibitishi chochote na kile nilichomuuliza. Pia hiyo makala nyingine aliyoiweka ndo kabisa inaonyesha jinsi gani akili yake ilivyo. Halafu utaona vilaza kama ritz nao wanajidai kumpa FF sapoti bila aibu, duh!

Na kuhusu hilo jina la Foxy sio hapo tu, inaonyesha jinsi gani huyu demu alivyo ndumilakuwili. Hata huko kwenye jukwaa la wakubwa ambako maadili ya Kiislamu hayazingatiwi kabisaa mtafute utampata. Ndio maana nimemuuliza, je angepata fursa hiyo kama angekuwa kwenye jukwaa la Kiislamu? Hadi sasa hajanijibu kikamilifu, anakwepa kwepa tu na kujichekesha kwa kebehi!
 
1. Namshukuru Mchambuzi kwa kuleta mada hii, inasaidia kujuwa tofauti ya mawazo yetu na kujuwa upepo unakwendaje ktk nchi yetu...
2. Nawashukuru wachangiaji wote, proposing and opposing, bila ubaguzi... ni haki yetu ya kikatiba..
3. Kutokana na mjadala huu nimejifunza kuwa:
  • Nyerere tumemtambua kuwa baba wa taifa letu kwa sababu ya mchango wake kwa watu wake wote na dini zao, na si kwa imani yake
  • heshima hiyo, japokuwa imefanana na matumizi ya heshima inayotumiwa na makasisi wa RC, lakini Nyerere hakupewa kwa misingi hiyo, yaani u-katoliki wake. Na kama inaonekana hivyo basi ni hisia na shida ya kutamani kuchukiana zaidi kuliko imani.
  • Kuna matumizi ya maneno au heshima yanayoingiliana kati ya dini na siasa nayo ni pamoja na Rais, Mwenyekiti, Katibu, nk. Isipokuwa Al~Hajj, Mtakatifu, Mwenyeheri, Mwadhama nk hayo ni maneno au majina ya heshima za kidini zaidi na hizo hutolewa na dini husika. Vilevile kuna heshima zinazotumika katika nyanja za elimu, siasa na dini kama vile Prof, Dr nk nk...
  • wanaopinga heshima hiyo ya baba wa taifa wanafanya hivyo kwa kutumia zaidi mafundisho ya dini yao kama msingi mkuu wa hoja pingamizi zao
  • Lakini Tanzania, na Tanganyika yake si nchi ya kidini. Hivyo tuepuke kufanya maamuzi yetu ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa, kwa misingi ya dini zetu. Tukifanya hivyo hatutaweza kubaki wamoja...tutafarakana, kutawanyika na kuishia kuwa kama taifa la Somalia (limegawanyika katika Punti land, Somalia na ya tatu inakaribia) ...
Vilevile katika mjadala huu nimegunduwa kuwa
(1) Wana dini wengi hatuna ufahamu unaofanaa katika kufafanuwa aya za misaafu
(2) Hatuna nchi moja inayosimama kama mfano standard wa misingi ya dini zetu. Tanzania itabaki Tanzania, na u-Islam wa Tz usihangaike kuiga kutoka Pakstan, Saudia, Iran na kwingineko... Hata sisi Mungu ni wetu na anapokea sala zetu kama viumbe wake, au siyo? Waarabu au wazungu siyo standards ya dini na lugha zao pia...
(3) misimamo mingine inaonesha chuki zaidi kuliko dini na imani...
(4) Wakati mwingine tunasumbuliwa zaidi na lugha kuliko mantiki ya imani zetu, na uzalendo wetu, na umoja wetu katika nchi yetu.. hilo halina tija ktk yote mawili au matatu...ni kuongeza pengo na umbali wa mtengano uliopo..
(5) heshima ya baba wa taifa haina madhara yoyote katika imani zetu na haituzuii kumwabudu Mungu na uwezekano wa kwenda peponi...
 
Kwanza pole sana kwa sad story yako. Pili, sina tatizo na US wakiwa na Father au Fathers. Hilo sipo kabisa huko.

Mimi nipo na imani yangu ya Kiislaam, siruhusiwi kumuita mtu yeyote baba zaidi ya aliyenizaa. Na pia hapa Tanzania Waislaam wenye msimamo kama wangu ni wengi sana, kwanini basi hawa wasio Waislaam walazimishe tumuite Nyerere "baba" wa Taifa wakati imani yetu hairuhusu? na hicho ni cheo kinachpatikana katika Ukristo na Kikatoliki ndio kabisa, nadhani nimeainisha mara nyingi na Ritz hapo juu kaweka list kamili ya u "baba".

Hili Waislaam hatukubaliani nalo, labda wale wasiojuwa maana.

Acha hizo...
Nani kakulazimisha kumuita Nyerere Baba wa Taifa?

Heshima ni kitu cha bure. Kama wewe hutaki kumheshimu hiyo ni hiari yako. Hakuna mtu wa kukufunga.
Tupo wengi sana tunaomuenzi Nyerere kwa mazuri mengi aliyoifanyia nchi hii ikiwa ni pamoja na kuwa muasisi wa Taifa hili. Tupo wengi tunaomheshimu, na tunatumia haki yetu na heshima yetu kumheshimu Nyerere na kumtambua kama baba wa Taifa.
Suala lilopo kwenu ni kuwa mnatumia chuki dhidi ya Nyerere kujaribu kujiweka pamoja. Na kwa juhudi hiyo basi hamtaki aheshimiwe kwasababu mnaona kuwa akiwa anaheshimiwa na jamii hoja zenu za chuki zitakosa mashiko na umoja wenu wenye asili ya AMNUT utaparaganyika. Ndio maana mnashupalia kum-demonize. Kila kibaya mna-associate na Nyerere, ili aonekane mbaya na kwamba ndiye aliyesababisha matatizo yenu. Na baadhi yenu mna chuki binafsi zilizopitishwa kwenu na wazazi wenu walioadhibiwa na mkono wa sheria enzi za Nyerere. Hayo ndiyo yanayowasumbua mpaka mmefikia hatua ya kusingizia uislam kuwa eti sababu ya hiyo dini basi hamwezi kumwita baba wa Taifa. Sisi wenye akili zetu (wapo na waislam pia), tunamwita baba wa Taifa, sio kama baba wa kutuzaa, na wala neno hilo halina uhusiano na dini yoyote. Ni heshima tu. Wewe na wenzako kaeni hivyo hivyo na machuki yenu.
 
JK analitamkaga kwa shidashida, Mzee AHM ndio amelitumia mara nyingi tu. Hii ni hadhi ya KISIASA haina hata chembe ya UDINI. Vinginevyo hata Dar hapakufai kuishi kabisa. Mabucha ya nguruwe kila kona, ushoga kila mahala tena mwingine ukiratibiwa na Waislaam wenzako, kumbi zingine za starehe zimepakana na misikiti, mahoteli ya nguruwe na pombe kila kona,...
Wewe unahangaika na U-Baba wa Taifa wa Mwalimu. Unalo jingine. Uislaam umeurithi tu. Unaonekana kuwa Muislaam zaidi ya waliokurithisha. Tuambie jina lako halisi. Uislaam hauruhusu kujipachika majina au jinsia bandia.

husipende kumfananisha Mzee Ally H.M na Kikwete.A.H.M alibebwa na J.k.N lakini kikwete kajibeba,kwahyo hana haja ya kumlamba miguu Nyerere.
 
Mi nashauri mkubaliane kutokukubaliana. Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.
and this piece?
 
Kwanza kabisa inabidi utuombe msamaha...
Wewe na nani? Sijaona unaungwa mkono na Waislamu walio wengi humu jamvini zaidi ya vilaza wachache ninaoweza kuwahesabu kwa vidole vya kiganja kimoja. Kwa hiyo usitake kujifanya wewe ndie muwakilishi wa Waislamu wote humu jamvini!
 
Baba wa Taifa Mwalimu J. k. Nyerere katika utawala wake aliishi kwa kufanya kazi kupita kiasi na hakufaidi matunda ya urais wake. Hata familia yake hakutaka waishi maisha ya anasa. Tulipanda nao MABASI YA Uda.

Nyerere aliinua sana kilimo kwa kumfikia kila mkulima kupitia mashirika yake. Aliyaendesha mashirika haya kwa hasara akilenga kuinua kilimo. Tungeenda na kasi ya Mwalimu sasa tungekuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kilimo Inchi za nje.
Mwalimu alisomesha watu bure ndiyo maana watanzania waliokuwa wanaenda kusoma nje walionekana kuwa na akili sana kwani kulikuwa na ufundishwaji unaofanana inchi nzima. Wale waliofaulu walikuwa na akili kweli. Sasa hivi bila pesa huwezi kusonga mbele pamoja na kuwa na akili nyingi. Inchi yetu baadaye itakuwa na viongozi wajinga wajinga tu.

Mwalimu alipigana vita kuikomboa Africa sehemu kubwa.

Mwalimu alimchakaza Iddi Amini akingia Uganda na kuwaandaa Waganda ili wajitawale wenyewe.
Hakuna Inchi ya Kiafrica maskini imewahi kufanya hivyo.

Tutachukua muda mrefu kumpata Nyerere mwingine.
 
Mchambuzi, ninasubiri utuletee hapa jamvini, sheria iliyompa mwalimu "ubaba" wa taifa kwa maana ni wewe uliyesema haya yafuatayo:

tofauti na heshima ya baba wa taifa ambayoe inatambulika kisheria, heshima rais bora huwa ni maoni ya wananchi walio wengi ambayo hupitia mchakato wa tafiti/vipima joto mbali mbali zinazolenga kukusanya maoni ya wananchi
 
FaizaFoxy said:
Kipo kwenye 17%

Ha ha ha...! Wewe mama ukiishiwa unakuwa huna hata aibu. Hiyo ndiyo miongozo ya dini yako inayokufanya ubuni vitu na kuvisema kama ukweli?
Kwenye uzi mwingine Historian scholar Mohamed said alisema vita ya maji maji ilikuwa ni vita ya waislam na wakristu. Nikamuuliza zile "Mahoka" zilizochomwa moto na wajerumani ndio ilikuwa misikiti? lol
 
Wanamchukia coz sio muislamu!!! teh teh!!! Wanataka tuwape ubaba wa taifa kina mzee Sykes!!!!
hakika wewe ni great thinker!
sasa ngoja tusubiri mitazamo ya kina FF,RITZ,MS,REJAO ili tujue nao wana maoni gani
 
Back
Top Bottom