Mi nashauri mkubaliane kutokukubaliana. Mwandishi ameelezea utofauti kati ya Baba na Rais bora wa Taifa,kila mtu ameelewa,labda kama mtu hakubali. Halafu ameonyesha kuwa asili ya ubaba wa taifa ama jina hilo haikutokea kanisa katoliki wala si Roma wanaotoa jina hilo kwa viongozi wa nchi hapa duniani,iwe za kiislamu au kikristo. Hata hatukuwahi kusikia aliyetoa jina hilo alikuwa kardinali Rugambwa au Pengo! Mi nadhani imechukuliwa kifamilia zaidi kwamba...kiongozi wa familia huwa ni mwanamume. Na kwa bahati ni kwamba wanaharakati wengi katika ukombozi na mapinduzi ya nchi zao,walikuwa wanaume... Kifamilia kuna mambo ambayo hayakamiliki hadi baba aje.. Heshima ya ubaba,ni kuonesha uongozi,msimamo,ujasiri,vision,na maamuzi ambayo hata kama yatapingwa na watoto au wake zake,ya baba yanakuwa ya mwisho.. Someone can correct me ila huo ndiyo ufahamu wangu.