Nyerere ndiye aliyeshauri umri wa kuanza shule uwe miaka 7

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,243
12,767
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea Mwalimu Nyerere alitoa hoja nyingi juu ya mustakabali wa elimu yetu. Moja ya hoja yake ulihusu umri wa mwanafunzi kuanza shule.

Alisema kuwa kuanza shule na miaka 5 au 6 haifai sababu mtoto anamaliza na miaka 12-13. Umri ambao hawezi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii. Kwanza nchi ya kijamaa inahitaji wafanyakazi(wakulima).

Mtoto wa 12 hawezi kuwa na manufaa yoyote. Pili asilimia kubwa sana ya watoto waliomaliza shule ya msingi enzi hizo, asilimia 87 walikuwa hawaendelei na sekondari, hivyo ni bora wanapomaliza shule ya msingi wawe na uwezo wa kufanya kazi.

Huo ndiyo mwanzo wa kuanza shule na miaka 7. Unaweza soma kitabu chake hicho na vingine vingi bure ndani ya maktaba app. Ipakue playstore.

IMG_20220308_141326_220.jpg
 
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea Mwalimu Nyerere alitoa hoja nyingi juu ya mustakabali wa elimu yetu. Moja ya hoja yake ulihusu umri wa mwanafunzi kuanza shule.

Alisema kuwa kuanza shule na miaka 5 au 6 haifai sababu mtoto anamaliza na miaka 12-13. Umri ambao hawezi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii. Kwanza nchi ya kijamaa inahitaji wafanyakazi(wakulima). Mtoto wa 12 hawezi kuwa na manufaa yoyote. Pili asilimia kubwa sana ya watoto waliomaliza shule ya msingi enzi hizo, asilimia 87 walikuwa hawaendelei na sekondari, hivyo ni bora wabapomaliza shule ya msingi wawe na uwezo wa kufanya kazi. Huo ndiyo mwanzo wa kuanza shule na miaka 7. Unaweza soma kitabu chake hicho na vingine vingi bure ndani ya maktaba app. Ipakue playstore.View attachment 2163089
Nitumie softcopy mkuu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nyerere alikuwa sahihi, hata hivyo zama zimebadilika. Hatuna budi kujitafakari kama kweli ni lazima kusubiri miaka 7 ndipo mtoto aanze elimu ya msingi. Nadhani tunaweza kubadili bila athari zozote kubwa, na tutachochea ari ya vijana kujitegemea mapema zaidi kwa kuchangia pato la taifa badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Tangu kuanza kwa Sekondari za Kata, asilimia kubwa ya watanzania wanafanikiwa kupata Elimu ya sekondari. Hii inaongeza miaka mingine 4 vijana wakingali chini ya mfumo rasmi wa elimu wenye usimamizi wa karibu.

Mimi naona sio vibaya tukirudisha miaka 2 nyuma, watoto waruhusiwe kuanza shule na miaka 5 ili wamalize sekondari wakiwa na umri wa miaka 16.

Kwa jinsi elimu yetu ya sasa ilivyo, watu wanazeekea shuleni. Fikiria mtu anamaliza digrii na miaka 23-25!
 
Kwa sasa hivi maisha yamebadilika japo wataalamu wanasema ubongo unakuwa umekomaa kuanzia miaka 7.
Lakini sahivi mtoto wa miaka 4 ana uelewa kuliko enzi zetu tukiwa na miaka 7
Kabla Nyerere alilazimika kusema hayo sababu watu walikuwa wanaanza shule na miaka 5. Maana enzi za wakoloni na mapema baada ya uhuru. Si kweli kwamba zamani walikuwa wanachelewa kukomaa akili.
 
Nyerere alikuwa sahihi, hata hivyo zama zimebadilika. Hatuna budi kujitafakari kama kweli ni lazima kusubiri miaka 7 ndipo mtoto aanze elimu ya msingi. Nadhani tunaweza kubadili bila athari zozote kubwa, na tutachochea ari ya vijana kujitegemea mapema zaidi kwa kuchangia pato la taifa badala ya kuendelea kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Tangu kuanza kwa Sekondari za Kata, asilimia kubwa ya watanzania wanafanikiwa kupata Elimu ya sekondari. Hii inaongeza miaka mingine 4 vijana wakingali chini ya mfumo rasmi wa elimu wenye usimamizi wa karibu.

Mimi naona sio vibaya tukirudisha miaka 2 nyuma, watoto waruhusiwe kuanza shule na miaka 5 ili wamalize sekondari wakiwa na umri wa miaka 16.

Kwa jinsi elimu yetu ya sasa ilivyo, watu wanazeekea shuleni. Fikiria mtu anamaliza digrii na miaka 23-25!
yah, ni bora kushusha. japo ukishusha kwa miaka miwili, ujiandae vyumba vya kuchukua intake ya miaka mitatu kwa mpigo. Na mtu akianza mapema ni rahisi kwake kusoma master na Phd bila kuona umri umemtupa.
 
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea Mwalimu Nyerere alitoa hoja nyingi juu ya mustakabali wa elimu yetu. Moja ya hoja yake ulihusu umri wa mwanafunzi kuanza shule.

Alisema kuwa kuanza shule na miaka 5 au 6 haifai sababu mtoto anamaliza na miaka 12-13. Umri ambao hawezi kuwa na manufaa yoyote kwa jamii. Kwanza nchi ya kijamaa inahitaji wafanyakazi(wakulima). Mtoto wa 12 hawezi kuwa na manufaa yoyote. Pili asilimia kubwa sana ya watoto waliomaliza shule ya msingi enzi hizo, asilimia 87 walikuwa hawaendelei na sekondari, hivyo ni bora wabapomaliza shule ya msingi wawe na uwezo wa kufanya kazi. Huo ndiyo mwanzo wa kuanza shule na miaka 7. Unaweza soma kitabu chake hicho na vingine vingi bure ndani ya maktaba app. Ipakue playstore.View attachment 2163089
Aliwajaza watu ujinga kuwa eti miaka 12 au 13 ndio mwisho wa kusoma mtoto akianza kusoma mapema. Dah, huyu Mzee hapo alibugi sana tena sana.
 
Kwa wakati huo alikuwa sahihi kwa kiasi fulani. Alisema kuwa ni asilimia 13 tu ya wanafunzi ndiyo wanaweza kwenda sekondari. Hivyo ni bora elimu yetu iiangalie jinsi ya kuwatumia hawa 87%
 
Back
Top Bottom