lakini tukubaliane kuwa nyerere hajatufikisha popote na kweli hakuwa na maono. ni kweli alijenga mshikamano wa kitaifa lakini kungine kote alikuwa anaendeshwa na emotions zaidi kul.iko kuangalia ahalisia wa mambo na dunia inakokwenda.
Mshikamano kivipi?
Hapo hua sipaelewi vizuri!
Kwani alipewa nchi hii ikiwa na vita au vurugu ?
Nijuavyo mimi Mwalimu amepewa nchi na Mwingereza ikiwa inatawalika vizuri na watu wakiwa na nidhamu ya hali ya juu ya kutii shera katika kila sekta.
Wajerumani ndio waliopata shida kuwafanya Waangaza wawe ni Taifa moja na Wangoni kwani waneweza kuwa ni Taifa moja na wahutu na watutsi na kuwa ni sehemu ya taifa lingine. Hali kadhalika wangoni wangeweza kuwa ni sehemu ya nchi nyingine.
Huyo aliyeifanya ardhi yenye makabila 125 kuwa ni nchi moja yenye kutawaliwa na kuongozwa kwa sheria moja huyo ndiye aliyetuunganisha.
Tusemeni tu ukweli sio kila jambo alilolifanya mkoloni lilikua baya kwetu sisi waafrika.Mengi yalikua mazuri sana. Ndio maana tunashindwa kusonga mbele mana kila kila kiongozi anakuja kumpinga aliyemtangulia hata kwenye mazuri tunayaita mabaya. Lakini ukikutana na wazee walioishi enzi za mkoloni na ambao hawakua na madaraka ya kisiasa watakuambia kuwa mkoloni alifanya mambo mengi mazuri hasa kimiundo mbinu ,elimu na uchumi.
Mjerumani alifanikiwa kuunganisha makabila 125 kuwa Taifa moja kwa sababu alikua ni mgeni na hakua na upendeleo wa kabila lolote kwa kuwa hakuwa na ndugu yake humu Afrika zaidi ya maslahi yake na kulinda mipaka ya eneo lake.
Mwafrika kamwe asingeweza kumuunganisha mwafrika mwenzake enzi hizo kabla ya mkoloni mana kila kabila lilijiona ni bora kuliko jingine.
Na ili kabila moja litawale lingine enzi hizo ilibidi kabila fulani liwe na nguvu zaidi ya lingine na liweze kulipiga sana na kulinyang'anya kila kitu ikiwemo wake zao na mali zao kama mufugo.
Hata kuoana makabila hayakua yanaoleana kabla ya mkoloni kuja na ilikua ni bala kubwa kwa kijana kuoa au kuolewa na kabila lingine.
Mkoloni akaja dini ya Ukristo ambayo ulikua inamchuka Padri mhaya kwenda kuhudumia watu wa Masasi na mfumo rasmi wa elimu ambapo watu walikua wanakutana huko kwenye maeneo ya kazi baada ya kuajiriwa na kuoana.
Watu walitoka Mbeya kwenda kufanya kazi Dsm ,Arusha n.k na huko walichanganyika na hata kuzaa na watu wa makabila mengine. Hata miji na makao makuu ya mikoa na wilaya yalibuniwa na kujengwa enzi za mkoloni ,ndio maana kila eneo la wilaya utasikia kuna eneo la BOMANI lilokua limeanzishwa na serikali ya awamu hiyo ya Mkoloni Mwingereza. Huko miji pia walikuwepo watu toka kila kabila ambao walikua wanafanya kazi kwenye ofisi na viwanda na mashamba ya wakoloni. Hao pia walikaa kwa pamoja na hata kuoana na kuoleana makabila tofauti. Mfano meneo ya mashamba ya mikonge kuna watu wa kutoka kila eneo la nchi hii na hata nchi za Burundi ,Malawi na Msumbiji. Hawa ni matokeo ya Mkoloni. Kabla ya kuja mkoloni hakuna Mngoni au Mhehe angeweza kukanyaga Kilimanjpkaro ,Mwanza, Tabora ,Tanga ,Arusha, Lindi na kwingineko bila vita. Watu wa makabila mengine walikua wanahamie au kukaa ardhi ya kabila lingine kwa mikataba maalum tena baada ya kupigana sana au baada ya kununuliwa toka nchi jirani kama Kenya kwa ajili ya ulinzi mfano Wakamba walitumika kama mamluki wa kulinda baadhi ya himaya kule Kaskazini kutokana na umahiri wao wa kutumia pinde na mishale.
Mwalimu kama kiongozi wa kwanza mwafrika kuitawala Tanganyika na anapaswa kuheshimiwa sana na kusifiwa sana kuweza kugombea uongozi na kumshinda mkoloni wakati huo ambapo uhuru wa mtu mweusi kisiasa ulikua mdogo sana.Pia tunamshukuru kuwa aliendelea kulinda umoja wetu na mipaka ya nchi yetu aliyoirithi toka kwa mkoloni kwa kutumia sheria na kanuni za mkoloni.
Tofauti na sasa ni kwamba Waliopigania uhuru hawakulenga sana maendeleo ya vitu kama ilivyo leo.
Walilenga kwanza UHURU na UTU wa mwafrika katika nchi yake. Haya mwalimu aluyasimamia kwa kiwango kikubwa.