Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Tumewaomba watutajie tu hayo makosa tuyajue. Yatajeni jamani. Hivi hamuoni kumdhihaki mtu na kumpachika makosa hata usiyo na uwakika nayo kama aliyatenda?
 
Hukunielewa kabisa, nadhani ni ktk post zote. Hivi unajua unapomkosoa Nyerere kwa mfumo wa kiutawala, unajua mnakijua mnachokimaanisha? Ujamaa ni mfumo mbaya na ubepari ni mfumo bora, ndo mnachosema kama hamjui.

Sasa hiyo mifumo mnaijua vyema yote? Ujamaa na uchumi, kisiasa, utawala, kijamii, sera za ardhi ktk ujamaa, shule nk. Pia ubepari na uchumi siasa utawala, kijamii ardhi, elimu nk. Mkishaijua vyema ndo unapata nafasi nzuri ya kukosoa.

Kuhusu lile nililo husisha na utawala wa Mungu, nia yangu ni kukuonesha tu kuwa hii muitayo demokrasia na Uhuru wa aina mbalimbali ni zao la Lucifer. Ndiye mpigania haki za viumbe wa kwanza, ndiye mwanzilishi wa mfumo wa vyama vingi na kutaka utawala uwe na vikomo. Je alifanya vyema, kwahiyo nyuma ya pazia nilitaka ujue waasisi haya mambo huwa na nayo.

Hivi nchi za magharibi zinawapenda sana? Kwanini hufadhili vyama vya kisiasa wala si kuleta madawa bure hospitali?
So ukimkosoa Nyerere basi wewe ni mpenda Ubepari!? Hiyo definition imeanza lini!? Kama Demokrasia ni mfumo wa Lucifer then Ujamaa ndio maisha halisi ya Lucifer. Hivi unajua Urusi chini ya Stalin iliua wakristo na mapadre wa Orthodox wangapi? waliua zaidi ya watu Milioni Ishirini, Na Mcomunist mwingine Mao tse tung aliua mamilioni huko China, Na hoa ndio machampion wa ukomunist. Na hapa mimi siungi mkono Ubepari wala siuungi mkono Ujamaa hiyo mifumo yoote ni extremist na kandamizi. Mimi naunga mkono mfumo mchanganyiko, 50/50.
Mimi ninacho kipinga kwa Nyerere ni yeye kuwa mbinafsi na kujiona kua yeye na mitazamo na maoni yake pekee ndio best interest za watz. Na hicho kitu ndio mzizi wa umasikini, ufisadi na uonevu unao endelea nchini. Nyerere alishindwa kutuwekea mifumo sahihi inayo kubalika na watz. Ogopa sana mtu asiyependa kushauriwa wala kukosolewa, huyo mtu ni zaidi ya Jinamizi, infact mtu wa aina hiyo manufaa atakayo yaleta ni ya muda mfupi tuu.
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?

Mkuu! Ukiona mwenzio anatabasamu wakati mambo hayaendi sawa ..Wee jua tu keshapata mtu wa kumshushia lawama.
 
Halafu tumeshawaomba mtuorodheshee makosa aliyoyatenda Nyerere, yatajeni hata ya utotoni hadi hospitali alikofia. Yatajeni hapa, inawezekana wengine hatuyajui. Pia inawezekana nanyi kwa kuyokuelewa kwenu vyema ama kukaririshwa na wapinzani wa ule utawala pasi kusumbua kichwa mnayahubiri. TUTAJIENI, YEYOTE AYAJUAYE AYATAJE.
Qwi Qwi Qwi......... Eti mtu orodheshee Makosa ya Nyerere!! Let me put it this way; Nyerere hakua na kosa lolote, alikua ni sawa na malaika, hata ile hutuba aliyo itoa na kusema kua katika uongozi wake kafanya mambo mazuri na pia kafanya mambo ya kijinga ilikua Feki ile hotuba iliandikwa na upinzani yeye akapewa asome tu. Na hata zile shutuma na makosa ambayo the late Mtikila ali yaandika na kuyatuma Vatican yakasababisha mchakato wa kumfanya kuwa mtakatifu kusitishwa nayo sio kweli. Nyerere was a saint. Are you happy now.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Yaani tokea Nyerere atoke madarakani mwaka 1984, na tokea mlipoua Azimio la Arusha...Still bado mnaamini kuwa Nyerere ni kikwazo kwa maendeleo yenu??

Hamataki kushughurisha akili zenu kujua mnatokaje hapo..ila mnakaa kulaumu yalitokea karibuni miaka 30 nyuma...

Nyerere pamoja na makosa yake alifanya yaliyoletwa mbele zake kwa uwezo wake na kwa pindi chake...Nanyinyi toka mwaka 1984 mlitakiwa kufanya yaliyombele zenu kwa uwezo wenu na kwa kipindi chenu ili mjileteee mandeleo..vinginevyo nyinyi ndio wabaya zaidi...

"We are able to see far ahead beyond the mountains simply because we are dwarfs standing on the shoulders of a very big giant man"..Peter Msigwa (Mp)
 
Soma vizuri, ni wapi nimeandika "Nyerere ni kikwazo kwa maendeleo yenu"?

Hayo ni maneno yako si yangu.
 
Tumewaomba watutajie tu hayo makosa tuyajue. Yatajeni jamani. Hivi hamuoni kumdhihaki mtu na kumpachika makosa hata usiyo na uwakika nayo kama aliyatenda?

Hana kosa lolote. Ni kama malaika.

Tusidai katiba mpya, ina tatizo lipi katiba ya Nyerere? Haina makosa.
 
Qwi Qwi Qwi......... Eti mtu orodheshee Makosa ya Nyerere!! Let me put it this way; Nyerere hakua na kosa lolote, alikua ni sawa na malaika, hata ile hutuba aliyo itoa na kusema kua katika uongozi wake kafanya mambo mazuri na pia kafanya mambo ya kijinga ilikua Feki ile hotuba iliandikwa na upinzani yeye akapewa asome tu. Na hata zile shutuma na makosa ambayo the late Mtikila ali yaandika na kuyatuma Vatican yakasababisha mchakato wa kumfanya kuwa mtakatifu kusitishwa nayo sio kweli. Nyerere was a saint. Are you happy now.
Yap niko happy, Umesema ukweli tena ukweli tupu japo kinafiki. Kuhusu mwenyewe kusema alifanya makosa nililijibu hilo, wenye hekima husema hivyo.

Nyerere ktk hotuba yake mbele ya wanafiki nadhani ndiyo hiyohiyo mnayoitumia alisema "huwa natembea na vitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha, bado nalisoma, tena kwa kulirudiarudia, nakiri hadi sasa sijaona tatizo lake, limeweka misingi ya utu"

Hapo hujaona amewakebehi mliodhani amesema alishafanya makosa? Kumbuka alikuwa akiongea na walioliua azimio na kubadili mifumo, angesemaje? Hii ni falsafa ya kuwasilisha hoja Mkuu.

Kuhusu utakatifu au lolote hilo mi haliniusu, simtetei Nyerere nikitaraji maombezi yake ya kiroho wala kutaraji kukutana naye peponi, bali alikuwa kiongozi mzuri, mtiifu, mwema na mwenye maono na alikuwa na upendo ulopitiliza kwa watu wake. Hayo tu, usiniambie sijui hakwenda kanisani au hakutoa sadaka nk hayo mi jaji wa hayo.
 
Mkuu wenye maono ni wewe, Sizonje na Bashite. Chuki zako kwa Mwalimu Julius Nyerere, zinakufumba macho kuto kuona yanayoendelea sasa, kupotea kwa Ben, kutekwa kwa msanii wa muziki na wenzake, kuwekwa kwa viongozi madarakani wenye veti vya kufoji. Wewe kila kukicha ni Mwalimu Nyerere. Mzee wawatu ameisha kufa, hivi ki bibi kwenye dini yako hakuna kipengele cha kuheshimu binadamu waliotangulia mbele ya haki. Basi subiri na wewe mwenyezi Mungu akikuchukua uende ukampe hizo lawama zako huenda atakupa majibu huko. Ingekuwa jambo la msingi mijadala uielekeze kwa hawa wanaoongoza leo kwa sababu wapo majibu wataweza kutoa. Mjibu kwa marehemu huwezi kuyapata because dead men don't talk.

Hta wakati wa Nyerere wengi tu walipotea, au hulijuwi hilo?
 
Yap niko happy, Umesema ukweli tena ukweli tupu japo kinafiki. Kuhusu mwenyewe kusema alifanya makosa nililijibu hilo, wenye hekima husema hivyo.

Nyerere ktk hotuba yake mbele ya wanafiki nadhani ndiyo hiyohiyo mnayoitumia alisema "huwa natembea na vitabu viwili, Biblia na Azimio la Arusha, bado nalisoma, tena kwa kulirudiarudia, nakiri hadi sasa sijaona tatizo lake, limeweka misingi ya utu"

Hapo hujaona amewakebehi mliodhani amesema alishafanya makosa? Kumbuka alikuwa akiongea na walioliua azimio na kubadili mifumo, angesemaje? Hii ni falsafa ya kuwasilisha hoja Mkuu.

Kuhusu utakatifu au lolote hilo mi haliniusu, simtetei Nyerere nikitaraji maombezi yake ya kiroho wala kutaraji kukutana naye peponi, bali alikuwa kiongozi mzuri, mtiifu, mwema na mwenye maono na alikuwa na upendo ulopitiliza kwa watu wake. Hayo tu, usiniambie sijui hakwenda kanisani au hakutoa sadaka nk hayo mi jaji wa hayo.

Halina tatizo kabisa azimio la arusha. Na ndilo tunalotumia hadi hii leo.
 
Soma vizuri, ni wapi nimeandika "Nyerere ni kikwazo kwa maendeleo yenu"?

Hayo ni maneno yako si yangu.

Hahahahaa! usipate shida nimeelewa uliyoandika vizuri sana..Habari ndiyo hiyo fanyeni kazi mjiletee maendeleo msibebeshe wengine mizigo ya umasikini wenu.
 
Yaani tokea Nyerere atoke madarakani mwaka 1984, na tokea mlipoua Azimio la Arusha...Still bado mnaamini kuwa Nyerere ni kikwazo kwa maendeleo yenu??

Hamataki kushughurisha akili zenu kujua mnatokaje hapo..ila mnakaa kulaumu yalitokea karibuni miaka 30 nyuma...

Nyerere pamoja na makosa yake alifanya yaliyoletwa mbele zake kwa uwezo wake na kwa pindi chake...Nanyinyi toka mwaka 1984 mlitakiwa kufanya yaliyombele zenu kwa uwezo wenu na kwa kipindi chenu ili mjileteee mandeleo..vinginevyo nyinyi ndio wabaya zaidi...

"We are able to see far ahead beyond the mountains simply because we are dwarfs standing on the shoulders of a very big giant man"..Peter Msigwa (Mp)
Halafu hana hata alichokosea huyu mzee wetu, kwa kipindi kile zile ndo zilikuwa sera bora kabisa. Sisi ndo wehu kwa kutokuona mbele. We ivutie tu picha kama zile falsafa zingeshamiri.

Huduma za jamii nzuri, ktk kipato kidogo alichokuwa nacho kitaifa. Ukabila, udini, ukanda nk si jambo dogo kulitokomeza. Sisi watanzania hatujawahi kuwa wamoja hapo kabla, na bado tuko safarini.

Siasa za kidemokrasia zingechelewesha tu maendeleo, leo watu wanapinga hata maendeleo kisiasa. Uhuru ungetumika vibaya kinyume na utekelezaji wa sera za kiuchumi na kijamii ktk mfumo wa ujamaa. Jamii za kikristu zingekuwa wapi kielimu wakati shule nyingi zilikuwa za kimisionari.

Nani angemiliki ardhi mbele ya mabilionea wachache wa kihindi? Mzee aliona mbali sana, leo anaonekana mjinga mkosaji. Nilishawaambia kosa kuitwa kosa ni lazima liwe na ufalme wa utendaji na ufalme wa ubongo, bad Will.
 
Halina tatizo kabisa azimio la arusha. Na ndilo tunalotumia hadi hii leo.
Mliua, ila tumeua msingi thabiti kwa taifa. Tulitakiwa tujiulize kwanini wapinzani wa nchi wa nje waliwatumia vichwa maji wa ndani kuliua? Je walikuwa na nia njema kwetu? Wanatupenda sana, wameona lile azimio lisingetufaa. Maajabu.
 
Mimi ninacho kipinga kwa Nyerere ni yeye kuwa mbinafsi na kujiona kua yeye na mitazamo na maoni yake pekee ndio best interest za watz. Na hicho kitu ndio mzizi wa umasikini, ufisadi na uonevu unao endelea nchini. Nyerere alishindwa kutuwekea mifumo sahihi inayo kubalika na watz. Ogopa sana mtu asiyependa kushauriwa wala kukosolewa, huyo mtu ni zaidi ya Jinamizi, infact mtu wa aina hiyo manufaa atakayo yaleta ni ya muda mfupi tuu.

Wacha ujinga, Unaposema "Nyerere alishindwa kutuwekea mifumo sahihi inayo kubalika na watz" ulitataka Nyerere peke yake ndiyo akuwekee hiyo mifumo? kwanini usimuulize babu na baba yako wao walikuwa wapi wakati Nyerere anaweka hiyo mifumo isiyofaa?
Kama wao walimwani Nyerere pekee kwanini baadae nyi mje mumpe lawama kwa kutokufikiri kwenu na kwa wazazi wenu?

Ok! Baada ya Nyerere kuondoka madarakani...mlishindwa nini kubadirisha hiyo mifumo na kuweka mifumo sahihi...Je mlihisi mmechelewa mpaka hii leo?...Je ni uzembe wa akili zenu?... Au Nyerere ameondoka na mashine ya kuchakata hiyo mifumo sahihi?

Je Azimio la Zanzibar halikuwa mwanzo wa kubadirisha mifumo hio...na yapi ni mafanikio yake mpaka sasa?
 
Hana alipikosea hata punje, tukifanya marekebisho popote pale ndo tunapotea zaidi. Kumbuka, haya maisha ya leo, wizi, ufisadi, drugs, ushoga, usagaji, ukanda, udini, ukabila, ujinga, matabaka, kutokuwa na sauti kimataifa, ombaomba, kila kitu ni mazao ya kumrekebisha hayati kwa viubongo vyetu vya kuku.
Huu ndio ukweli. Hebu muone raisi wa sasa anapojaribu kuyashughulikia hayo, anavyotukanwa, kudhalilishwa na kubezwa hata watu ambao hawajui watokako na waendako?
 
Hana kosa lolote. Ni kama malaika.

Tusidai katiba mpya, ina tatizo lipi katiba ya Nyerere? Haina makosa.
Katiba ni nini kwani? Lazima ibadilike kwakuwa hata mazingira nayo yanabadilika. Lazima sheria zibadilike pia. Akina Nyerere hawapo tena, wenye uadilifu, unadhani katiba ya Nyerere si wataitumia vibaya? Leo hakuna sababu ya kumlundikia raisi mamlaka, hawaaminiki hawa.
 
Hta wakati wa Nyerere wengi tu walipotea, au hulijuwi hilo?
Kupoteaje labda unamaanisha? Kama ni kule kuangamizwa, hiyo ni kanuni tu ya ASILI, matawi yasiofaa lazima yakatwe ili mti ukue vyema. Mungu hufanya hivyo, na hapajawahi kutokea hapa duniani utawala usiotumia hii kanuni.

Imetumika hata na mitume ilipotawala, narudia ni kanuni ya ASILI. Tena alikuwa mpole sana, wapinzani hawakustahili kuwepo kabisa.
 
Huu ndio ukweli. Hebu muone raisi wa sasa anapojaribu kuyashughulikia hayo, anavyotukanwa, kudhalilishwa na kubezwa hata watu ambao hawajui watokako na waendako?
Mi nko na mashaka na mfumo wa elimu, tuko vilaza saana. Hata hatujui mifumo ya utawala, ajabu sana. Hapa hoja ilitakiwa iwe ni ujamaa na ubepari upi ni mfumo bora?
 
Hisia zako tu la mhm alilofanya nyerere na ambalo linakufanya ht ww ukae hapo uandike upuuzi huu ni kuondoa ukabila na ndoa mana tuna amani hadi leo mengine watafanya wengine ila huwezi elewa ila cheki kenya tu hapo ...ujifunze
 
Back
Top Bottom