Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
Umetumwa na Tundu Lissu
 
Hahahahaa! usipate shida nimeelewa uliyoandika vizuri sana..Habari ndiyo hiyo fanyeni kazi mjiletee maendeleo msibebeshe wengine mizigo ya umasikini wenu.
Umasikini ulikuwa wakati wa Nyerere.

Nchi nzima hohehahe.
 
Hisia zako tu la mhm alilofanya nyerere na ambalo linakufanya ht ww ukae hapo uandike upuuzi huu ni kuondoa ukabila na ndoa mana tuna amani hadi leo mengine watafanya wengine ila huwezi elewa ila cheki kenya tu hapo ...ujifunze

Nyerere alipokelewa na akina nani alipokuja Dar kutokea Kisarawe?

Kungekuwa na ukabila angepokewa?

Sijapatapo kusikia tatizo la ukabila kabla ya Uhuru, labda ulete mengine.

Tena umenikumbusha, umeshawahi kusikia "undugu naizesheni" unajuwa ulianza lini? Huo ni ubaguzi ulioibuka wakati wa Nyerere.
 
Kwahiyo haya ndo makosa makubwa aliyoyatenda Nyerere? Hadi nimecheka kwanza. Unasema ukabila haukuwepo kabla ya Nyerere? Kwahiyo watu walikuwa wakioa kabila lolote lile, hapakuwepo walojiona wao bora zaidi ya wengine nk
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?
Lugha ya malkia ni shida,correction
He has been died for a long time- he died long time ago.
And he has been out of power for even longer-(and he is no longer in power) sawa mkuu
 
Kwahiyo haya ndo makosa makubwa aliyoyatenda Nyerere? Hadi nimecheka kwanza. Unasema ukabila haukuwepo kabla ya Nyerere? Kwahiyo watu walikuwa wakioa kabila lolote lile, hapakuwepo walojiona wao bora zaidi ya wengine nk

Unajifanya hukielewi kilichojibiwa kwenye hiyo post? Au huelewi kweli unakurupuka tu?

Rudi juu kasome kilichojibiwa kuhusu ukabila.

Hilo la makosa mbona nimekujibu zamani sana. Nyerere hana makosa ni malaika na kuna mtu kalijibu hilo juu huko.

Mimi nimekubali hoja zako zote, Nyerere hakuwa na makosa kabisa ni malaika aliyeletwa kwa umbo la kibinadamu au siyo?

Tatizo nini?
 
Umasikini ulikuwa wakati wa Nyerere.

Nchi nzima hohehahe.
Alijaribu kadiri ya uwezo wake maana kipindi hicho wasomi walikua wachache watu wamesoma bure tena kwa kulipiwa hadi nauli, wengi wao ndio wamekosa uzalendo. Fikiria leo pamoja kukua kwa teknolojia bado miundo mbinu ya mawasiliano haijawa asilimia mia hapa nazungumzia barabara hata simu. Nyerere walianzisha viwanda Leo viko wapi? Kipindi tunakosea kwa sababu ya kutokua makini na vipaumbele Leo umeme wa maji kesho gesi hatutafika. Inatakiwa tukubali tuko chini na kilimo maana kimeajiri asilimia kubwa ya wananchi pia soko lipo wazi kwa majirani zetu kuliko kufikilia kufanyabiashara na mabepari wa magharibi. Hivyo vyote alivyovisimamia nadhani ilikua ngumu kuweka mfumo haswa katiba yenye mtizamo wa mda mrefu. Hapo ujazungumzia vita ya Uganda ilishusha uchumi wetu
 
Kwahiyo haya ndo makosa makubwa aliyoyatenda Nyerere? Hadi nimecheka kwanza. Unasema ukabila haukuwepo kabla ya Nyerere? Kwahiyo watu walikuwa wakioa kabila lolote lile, hapakuwepo walojiona wao bora zaidi ya wengine nk

Kwanini wasioe kabila lolote?

Mtazame Salim Ahmed Salim aliyezaliwa kabla ya Uhuru kwa miaka mingi, baba'ke kabila gani mamake kabila gani?

Tueleze kuhusu Karume wale wake zake wanne ni kabila yake?

Kuoana kabila moja si muhali ni utaratibu wa kulinda mila na tamaduni ambao mpaka leo hii upo na pia kuoana makabila tofauti ilikuwepo kabla ya Uhuru. Kumbuka hilo, hakulianziaha Nyerere hilo.

Tazama mashombe wote waliopo Tanzania ambao ndiyo rahisi sana kuelewa kuwa wamechanganya makabila, wote hao walioana na kuzaana baada ya uhuru.

What an idiotic way of thinking.
 
Unajifanya hukielewi kilichojibiwa kwenye hiyo post? Au huelewi kweli unakurupuka tu?

Rudi juu kasome kilichojibiwa kuhusu ukabila.

Hilo la makosa mbona nimekujibu zamani sana. Nyerere hana makosa ni malaika na kuna mtu kalijibu hilo juu huko.

Mimi nimekubali hoja zako zote, Nyerere hakuwa na makosa kabisa ni malaika aliyeletwa kwa umbo la kibinadamu au siyo?

Tatizo nini?
Wa ajabu kweli! Sa kwa mantiki hiyo nani hana makosa, we Umesema ana makosa makubwa, tena ndo msingi wa mabaya yote hapa nchini. Unatokomea gizani.

Kwa mantiki ya umalaika, hata mtume alifanya dhambi tena ndani ya utume tena kwa kumsikiliza tu mkewe, aliharamisha asali. Sembuse Nyerere, kama Alishawahi kumpiga mkewe kamvunja mkono, hapa halihusiki kabisa.
 
Alijaribu kadiri ya uwezo wake maana kipindi hicho wasomi walikua wachache watu wamesoma bure tena kwa kulipiwa hadi nauli, wengi wao ndio wamekosa uzalendo. Fikiria leo pamoja kukua kwa teknolojia bado miundo mbinu ya mawasiliano haijawa asilimia mia hapa nazungumzia barabara hata simu. Nyerere walianzisha viwanda Leo viko wapi? Kipindi tunakosea kwa sababu ya kutokua makini na vipaumbele Leo umeme wa maji kesho gesi hatutafika. Inatakiwa tukubali tuko chini na kilimo maana kimeajiri asilimia kubwa ya wananchi pia soko lipo wazi kwa majirani zetu kuliko kufikilia kufanyabiashara na mabepari wa magharibi. Hivyo vyote alivyovisimamia nadhani ilikua ngumu kuweka mfumo haswa katiba yenye mtizamo wa mda mrefu. Hapo ujazungumzia vita ya Uganda ilishusha uchumi wetu

Hilo la viwanda tumeshalijihu juu huko, kaisome.

Miundombinu tulioachiwa na mkoloni pia tukaiua wakati wa Nyerere.

Waulize waliokuwepo kabla ya Uhuru kama ilikuwa unaenda Kenya ili ufike Mwanza ukitokea Dar. Au kama treni ya kati ilishakaa bila kutumika kwa muda wake na treni za kila siku kwenda na kurudi kwa wakati. Tukafanyaje baada ya Uhuru, tukaifanya nyang'a nyang'a.

Tatizo si kukosa wataalam tatizo kukosa misingi bora ya uendeshaji, tuliona waliotuachia nchi wajinga tubadili mfumo wao. Hapo ndipo tukaharibu kabisa.

Hata Mugabe hana makosa kuimaliza Zimbabwe.

Unaniaminisha kuwa hata Nyerere hakuwa na makosa. Nimekubali hoja zako. Kuanzia sasa naamini Nyerere hakuwa na makosa alikuwa ni malaika asiyefanya makosa.
 
Kwanini wasioe kabila lolote?

Mtazame Salim Ahmed Salim aliyezaliwa kabla ya Uhuru kwa miaka mingi, baba'ke kabila gani mamake kabila gani?

Tueleze kuhusu Karume wale wake zake wanne ni kabila yake?

Kuoana kabila moja si muhali ni utaratibu wa kulinda mila na tamaduni ambao mpaka leo hii upo na pia kuoana makabila tofauti ilikuwepo kabla ya Uhuru. Kumbuka hilo, hakulianziaha Nyerere hilo.

Tazama mashombe wote waliopo Tanzania ambao ndiyo rahisi sana kuelewa kuwa wamechanganya makabila, wote hao walioana na kuzaana baada ya uhuru.

What an idiotic way of thinking.
Kuna kitu nakiacha ntakujuza siku nyingine, ila msijipofushe saaana. Kuna walio sekondari humu. Hivi baba wa Salim Ahmed Salim ni msukuma wa Kahama na mama wake ndiye mwarabu au?

Hilo nilikuwa silijui. Kumbe waafrika, tena weusi walikuwa wakiwaoa mabinti wa kiarabu tena hata kabla ya Uhuru freely.

Yaani mwanaume wa kijaluo ilikuwa sawa tu kuja kuoa uzaramoni na wala kwao wasimuone wa ajabu, tena yote ni kabla ya Uhuru. Mi kweli ni idiot kwakuwa sikuwahi hata kudhani kama yalikuwepo.
 
Wa ajabu kweli! Sa kwa mantiki hiyo nani hana makosa, we Umesema ana makosa makubwa, tena ndo msingi wa mabaya yote hapa nchini. Unatokomea gizani.

Kwa mantiki ya umalaika, hata mtume alifanya dhambi tena ndani ya utume tena kwa kumsikiliza tu mkewe, aliharamisha asali. Sembuse Nyerere, kama Alishawahi kumpiga mkewe kamvunja mkono, hapa halihusiki kabisa.

Hayo ya mitume yako wewe si yangu.

Nakwambia nimekubali hoja zako zote, ni nzuri sana na umenikinaisha kuwa Nyerere hana kosa hata moja na sasa nnauhakika alikuwa ni malaika.

Kuna lingine?
 
Kuna kitu nakiacha ntakujuza siku nyingine, ila msijipofushe saaana. Kuna walio sekondari humu. Hivi baba wa Salim Ahmed Salim ni msukuma wa Kahama na mama wake ndiye mwarabu au?

Hilo nilikuwa silijui. Kumbe waafrika, tena weusi walikuwa wakiwaoa mabinti wa kiarabu tena hata kabla ya Uhuru freely.

Yaani mwanaume wa kijaluo ilikuwa sawa tu kuja kuoa uzaramoni na wala kwao wasimuone wa ajabu, tena yote ni kabla ya Uhuru. Mi kweli ni idiot kwakuwa sikuwahi hata kudhani kama yalikuwepo.

Karume alikuwa Mwarabu akaoa mwarabu.

Kingunge alikuwa Mhindi akaoa mhindi.

Kuna zaidi?
 
Hilo la viwanda tumeshalijihu juu huko, kaisome.

Miundombinu tulioachiwa na mkoloni pia tukaiua wakati wa Nyerere.

Waulize waliokuwepo kabla ya Uhuru kama ilikuwa unaenda Kenya ili ufike Mwanza ukitokea Dar. Au kama treni ya kati ilishakaa bila kutumika kwa muda wake na treni za kila siku kwenda na kurudi kwa wakati. Tukafanyaje baada ya Uhuru, tukaifanya nyang'a nyang'a.

Tatizo si kukosa wataalam tatizo kukosa misingi bora ya uendeshaji, tuliona waliotuachia nchi wajinga tubadili mfumo wao. Hapo ndipo tukaharibu kabisa.

Hata Mugabe hana makosa kuimaliza Zimbabwe.

Unaniaminisha kuwa hata Nyerere hakuwa na makosa. Nimekubali hoja zako. Kuanzia sasa naamini Nyerere hakuwa na makosa alikuwa ni malaika asiyefanya makosa.
Halafu wewe nadhani hujui maana ya neno lenyewe "KOSA" uwezi ukaita nia njema iliyoshindishwa kuifikia kuwa ni kosa? Narudia tena, ili jambo liwe kosa ni lazima kuwe na utendaji ndani ya ubongo wa kuhitaji kulitekeleza hilo jambo kimakosa, kwa lugha yenu inaelezwa, With malice aforethought.

Ndo maana nahitaji mnitajie hapa yapi yalikuwa ni makosa Hayati aliyatenda? Sio mistakes au negligence, crimes.
 
Hilo la viwanda tumeshalijihu juu huko, kaisome.

Miundombinu tulioachiwa na mkoloni pia tukaiua wakati wa Nyerere.

Waulize waliokuwepo kabla ya Uhuru kama ilikuwa unaenda Kenya ili ufike Mwanza ukitokea Dar. Au kama treni ya kati ilishakaa bila kutumika kwa muda wake na treni za kila siku kwenda na kurudi kwa wakati. Tukafanyaje baada ya Uhuru, tukaifanya nyang'a nyang'a.

Tatizo si kukosa wataalam tatizo kukosa misingi bora ya uendeshaji, tuliona waliotuachia nchi wajinga tubadili mfumo wao. Hapo ndipo tukaharibu kabisa.

Hata Mugabe hana makosa kuimaliza Zimbabwe.

Unaniaminisha kuwa hata Nyerere hakuwa na makosa. Nimekubali hoja zako. Kuanzia sasa naamini Nyerere hakuwa na makosa alikuwa ni malaika asiyefanya makosa.
Sijasema hakuwahi kosea ila alisimamia vipaumbele vyake aliweka kipaumbele kwenye elimu nasikitika wale halio wapeleka kusoma wamemwangusha hadi Leo unaweza maikia aliesoma Cambridge, harvad au Stanford ukashindwa mtofautisha na mtu wa mtaani. Na uzuri mwenyewe alishawahi kilikua mfumo huu ukimpata kiongozi mwingine anaweza kuwa kama dikteta kwa sababu mfumo unaruhusu. Ila nyerere kafanya kazi kubwa kutuunganisha Leo hii ubinafsi unatutenganisha. Kwani nyerere alishindwa kumpa cheo kikubwa mkewe na ndugu zake. Alichofanya kikubwa sema tumeshindwa endeleza wenyewe. Kumbuka nyerere kaondoka wakati wa chama kimoja Leo vyama vingi nadhani wakati wanaanzisha vyama vingi ndio ulikua mda mwafaka wa kuweka mfumo mpya na sio kuziba viraka. Tuombe Mungu atuongozee uzalendo mi naamini kilimo ndio mwarobaini wa maisha ya waliowengi mengine tutachelewa sana
 
Kwahiyo bi foxy unataka kusema ni kheri hata ukoloni usingeondoka. Wangeziboresha Huduma za reli, leo tungeshakuwa na ya umeme. Utumwa wa kifikra ni mbaya zaidi kuliko hata wa kutumikishwa umanamba.
 
Karume alikuwa Mwarabu akaoa mwarabu.

Kingunge alikuwa Mhindi akaoa mhindi.

Kuna zaidi?
Karume? Kingunge? Hawa walioa walipokuwa makuli au walima mtama? Tena la Karume ndo kabisa labda ziwe ni stori za vijiweni, kuhusu yeye kuoa mwarabu.
 
Huna ulijualo. Nahisi hata mama Fatma Karume haumuelewi.
 
Halafu, tuangalie isije ikawa hata fedha zilizo wasomesha nje zilikuwa za uhujumu uchumi,wazazi wenu au wenye mmeyafirisi mashirika ya umma, mmedhorotesha falsafa za Mwl. Leo mnakuja hapa kukosoa, hapo lazima laana iwashike. Utakuwa ni zaidi ya unafiki hapo. Mungu haupendi.
 
Back
Top Bottom