Mwalimu Nyerere
Amefanya jambo kubwa moja ambalo ni la maana kupita yote
Kutuleta pamoja Watanzania kwa kuimarisha UPENDO kati yetu
Leo Tanzania ndiyo nchi ya kwanza Duniani kwa raia wake kupendana.
Ijapokuwa tunaangushwa na viongozi wachache wenye uwezo mdogo wa kuongoza kwa kuweka maslahi yao mbele
Mtanzania wa leo anaweza kuishi sehemu yoyote hapa nchini kwenye kabila lolote na akuchukuliwa kama mtoto wa nyumbani.
Kama atakuwa mwema basi atapewa shamba ajenge, ataozeshwa, atagombea cheo chochote na kuchaguliwa bila ubaguzi wa aina yoyote.
Kwangu mimi upendo huu ni kitu cha msingi kuliko Azimio la Arusha au serikali tatu.
Leo ndugu zetu wazanzibari wanafulahia maisha huku bara bila usumbufu nasisi tunaishi zanzibar kama nyumbani
Upendo huu ni zaidi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea, ni zaidi ya udikteta wa Chama kimoja ni zaidi ya Nyerere mwenyewe.
Angalieni kwa wenzetu mara vita vya msituni mara vita vya kikabila na mauaji ya kimbali,
Mara vita vya kidini huko Afrika ya kati hadi watu wanajiita anti baraka, boko haramu, eli shababa sijui
Dhana ni kuwa msingi wa UPENDO haukujengwa, haupo.
Nyerere alifanya hili, wengine wafanye hayo mengine, nchi haikamiliki kujengwa na Raisi mmoja au awamu moja ya utawala.
Kwa hili la kutuweka pamoja kama nchi mimi nimemsamehe Mwalimu kwa kosa lolote alilofanya, yeye sio malaika, hata wewe ulishakosea katika majukumu yako lakini jiulize ushafanya jambo lolote la maana kwenye jamii yako?
Asante Mwalimu Nyerere.