Nijibu hoja zako kwa aya moja tu. Nashukuru nitambua kuwa hukuwa na misingi ambayo ambayo kwayo Mwl Nyerere aliianzisha na sasa inadunisha maendeleo yetu. Ninchokiona unataja baadhi ya matukio yaliyofanywa na baadhi ya maraisi waliofuata tena waislamu na kusema wamefanya vizuri. Kwa taarifa yako marais wote hawa wanatekeleza mpango wa taifa ulioasisiwa na Mwl Nyerere. Kabla ya kuuhishwa miaka ya 1990 ulisomwa na Mzee Kingunge pale Kizota mwaka 1987. Huo ulikuwa mpango wa miaka 15. Wakati huo Mwl Nyerere alikuwa mwenyekiti wa ccm. Baada ya mwenye kuweka msingi wa uendeshaji uchumi; Mh Mkapa aliimarisha uchumi mkubwa na kuuanza mkakati wa kutengeneza barabara kwa kauli mbiu kutoka Dar-Kagera kwa taxi au wengine walikoleza bajaji. Muda uliisha akiwa kamalizaa daraja la Mkapa. Mh Kikwete hakuwa na kingine ni kumalizia barabara zilizoachwa atake asitake. Kama unakumbuka alianza kwa kusuasua mpaka serikali ikawa inalipa faini kwa kutokupeleka pesa. Mh Kikwete baada ya matokeo magumu 2010 ndipo alipojitenga na wanamtandao wake na kumrudisha Mh Magufuli kwenye ujenzi huku wakimzuia baadhi ya maamuzi kama vile swala la uzito wa malori. Haya yote yanafanywa kwenye misingi aliyoiweka Mwl Nyerere kwa viongozi kubadilishana kwa amani na kutekeleza mpango wa maendeleo.Hizo barabara zote unazozisema zilijengwa na makampuni ya nje na 90% hazikujengwa wakati wa Nyerere.
Kikwete ndiye aliyefanya mapinduzi ya barabara Tanzania.
Wakati wa Nyerere hata Dar mjini kulijaa mahandaki na tulizikuta na lami walivyotuachia wakoloni.
Hivi uliziona barabara za Dar alizowachiwa Mwinyi na Nyerere?