Nyasa: DC Kanali Laban Thomas aagiza polisi kuwakamata wanaovaa nguo fupi na "milegezo"

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.

DC%20WEB.jpg

Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo
 
Eti huyu naye aliapa kutumikia hiyo nafasi yake!

Mbona viongozi mnashindwa kutatua matatizo makubwa waliyonayo wananchi badala yake mnaruka kufanya kazi za ajabu ajabu.

Wanyassa wilaya yenu haina matatizo kumbe ni vimini na milegezo tu?
 
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo
Na huko Mahakamni atataka wahukumiwe kwa sheria ipi? Hizi sio enzi za Magufuli watu walihujumiwa kwa "sheria" ya maagizo ya Magufuli

Uhanga unamsumbua huyu hawezi kuvumilia kuona mini
 
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amepiga marufuku mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.

View attachment 1905898
Mkuu wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lulimbo
Safiii, bado wanaume wenye tabia za kike kusuka nywele na kuvaa hereni
 
Ndio maana watu tunataka katiba mpya ili ikafute hivi vyeo vigine watendaji wake waakula kodi zetu bure!
Hapo ukimuuliza akupe takwimu za miradi ya maedeleo kama shule, zahaati, barabara, na miradi ya maji amavyo bado havijakamilika na wananchi wanateseka kukosa huduma hizo muhimu wala hawezi kukujibu chochote, maana anashughulika na vitu vidogo sana!
 
Back
Top Bottom