Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Hebu ngoja niandike -----
Ni kweli kabisa hili gazeti la m a w i o sijui limewakosea nini.

hata neno mwa.na.ha.li.si jaribu kuandika sijui wanabifu gani na ngoja nijarbu jina la gazeti lingine MZALENDO..
Hakika mzalendo limekubali.. sijui ndo mafisadi washaanza kuiteka jf!!!????
cc Matola Mzito Kabwela
 
Last edited by a moderator:
Mwandishi Mahiri wa Makala na Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam Nyaronyo Mwita Kicheere amehamia CCM, kati ya sababu kubwa zilizomhamisha CHADEMA, anasema Viongozi wake hawana sura ya Tabasamu, tofauti na viongozi wa CCM, Kikubwa zaidi anasema ameamua kuipenda CCM kwa kuwa Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete ni mtu Rahimu, anayependa watu wake na kuwahurumia kutokana na magumu ya maisha, Juzi juzi ametangaza jinsi alivyopelekewa orodha ya majangili 40 wanaotikisa mbuga zetu lakini hakuwachukulia hatua yeyote kwa kuwa wanafanya ujasiriamali kujikimu na wanaweza kuwekeza. Nyaronyo amesema pia, anahamia CCM kwani kesho au keshokutwa akikamatwa na ngozi ya Chui, ya Mamba, au meno ya Tembo atapata msamaha kama wale 40 waliosamehewa na Kikwete.

Nyaronyo anasema, CHADEMA wangekuwa madarakani leo, ambao viongozi wao hawana tabasamu, akamtaja Mbowe Slaa, Lissu na Lwakatare nchi isingekalika, maana ni wazee wa visasi, maana Wezi wangekamatwa, watekaji wangesakwa, wauza dawa za kulevya wangekuwa wote gerezani.

Tena akaongeza kuwa hii si mara ya kwanza Kikwete kusamehe. Amesamehe Majangili 40, kama alivyosamehe wezi wa EPA, Nyaronyo anasema Tumshukuru Mungu kwa kuwa na Kikwete, Rais anayesamehe. = Chanzo gazeti la -----

kasoma sheria za nini mbona vi vihoja mahakamani?tunamtakia kila la kheri ana lake jambo, hapendi watu wanaona uchungu na nchi ok tumemuelewa
 
Kweli naakubali 2mekaa miaka 9 bila raisi, ngoja 2malizie umebaki mmoja 2
 
Ni mtu makini sana anajiamini sana, ana watoto wazuri kweli ningekuwa sijaoa ningemuoa RHOBI au Tumaini, makala zake zina fasihi sana na ukiingia kichwakichwa utaweza kumuelewa.......... nakumbuka ndio aliyemtimua nchimbi jangwana.... Ukimuona yupo simple sana, nampenda sanaaaaaaaaaa.

mwenyekiti wa kuchekacheka nasikia ameandaa mkutano wa kumkabidhi kadi
 
hahahaha napenda sana uandishi wa kicheere...ccm sijui useme nn ili wabadilike? mfano mwaka 2007/08 kikwete akihutubia ktk viwanja vya mashijaa bukoba alilalamika juu ya mchwa anayetafuna halmashaur ya bk.....huwez kuamin hakuna kilichotokea mpaka mwaka jana mwishon madiwan wa ccm wanaanza kushikana uchawi!!!! dhaifuuuuuuuuu
 
mwanasheria nguli mkali wa fasihi umefikisha ujumbe kwa mkuu wa kaya.mzee wa tabasamu,mtu wa kusamehe ingawa anawajua majangili,wezi ,wauza poda,.......kweli nyaronyooooo kicheeeeeeere umetisha

mkuu wewe ndo umemwelewa mtoa uzi hapo maana wengine wanaweweseka hawajui kama hiyo stori ni kweli au hapana. fasihi imetumika vilivyo kuwakilisha ujumbe!
 
Back
Top Bottom