Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'


Huyu si alisema Kikwete anamchukia bila ya sababu? Kafuata nini tena huko CCM?


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cheere-kikwete-ananichukia-bila-sababu-3.html

Nyaronyo-Mwita-Kicheere.jpg

Mkuu soma tena ile post ya mleta mada.
 
Mwandishi Mahiri wa Makala na Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam Nyaronyo Mwita Kicheere amehamia CCM, kati ya sababu kubwa zilizomhamisha CHADEMA, anasema Viongozi wake hawana sura ya Tabasamu, tofauti na viongozi wa CCM, Kikubwa zaidi anasema ameamua kuipenda CCM kwa kuwa Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete ni mtu Rahimu, anayependa watu wake na kuwahurumia kutokana na magumu ya maisha, Juzi juzi ametangaza jinsi alivyopelekewa orodha ya majangili 40 wanaotikisa mbuga zetu lakini hakuwachukulia hatua yeyote kwa kuwa wanafanya ujasiriamali kujikimu na wanaweza kuwekeza. Nyaronyo amesema pia, anahamia CCM kwani kesho au keshokutwa akikamatwa na ngozi ya Chui, ya Mamba, au meno ya Tembo atapata msamaha kama wale 40 waliosamehewa na Kikwete.

Nyaronyo anasema, CHADEMA wangekuwa madarakani leo, ambao viongozi wao hawana tabasamu, akamtaja Mbowe Slaa, Lissu na Lwakatare nchi isingekalika, maana ni wazee wa visasi, maana Wezi wangekamatwa, watekaji wangesakwa, wauza dawa za kulevya wangekuwa wote gerezani.

Tena akaongeza kuwa hii si mara ya kwanza Kikwete kusamehe. Amesamehe Majangili 40, kama alivyosamehe wezi wa EPA, Nyaronyo anasema Tumshukuru Mungu kwa kuwa na Kikwete, Rais anayesamehe. = Chanzo gazeti la -----

cc: Salva Rweyemamu - Magogoni Dar es Salaam
 
Nimekuelewa...
Katumia lugha ya sanaa kidogo...
 
For those of you who did not understand, the guy is insulting mr.president kutokana na tabia yake ya kusamehe watuhumiwa!
 
Back
Top Bottom