Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Kumbe Kicheeere kagndua pa kupigia deal!! Huko kwa MaCCM ukiwa mwizi, muuza poda, ndovu awe mzima au meno yake pouwa tu, ukibaka hata kuambukiza ngwengx pouwa tu, ukisafirisha bange, hata ukipiga deal la kusafirisha wahamiaji haramu huko ni pouwa tu. Jamani hadi raha!
 
Hawa walikuwa wanacheka cheka hovyo wakati wanadai uhuru, ama kuyakomboa mataifa yao kutoka kwenye makucha ya mabeberu weusi wanyonyaji? taifa letu linahitaji ukombozi wa kuwatokomoeza hawa mabepari weusi wanaolitafuta bila huruma.
images
images
images
images
images
images




Huyu kicheere ni MPIGANAJI hasa siku moja hawezi kwenda Lumumba!! someni tena hoja ya mlete hoja!!

Mkuu unajua lugha ya fasihi ni ngumu sana kwa vijana wetu.cc Toothpick
 
Last edited by a moderator:
Hii habari ya Nyaronyo Kicheere kuhamia CCM imeadikwa leo kwenye Gazeti la ----- yenye kichwa: NIMEHAMIA CCM,CHADEMA HAKUNIFAI.

Hii habari imeandikwa kwa namna ya kimafumbo sana. Inahitaji ubongo uliokwenda shule kujua au kupata maana ya ujumbe ulioko ndani ya habari hii.Wazungu husema, you have to read between the lines. Hapa ndipo unaweza kujua nani walisoma RIWAYA na TAMTHILIA na kufaulu mitihani ya Kiswahili au LITERATURE IN ENGLISH( Theme:CONFLICT,PROTEST,etc). Nashangazwa na Magamba kushangilia ati kweli Nyarocho kahamia CCM!! Hahami mtu hapa. Ebo!

Hapa Nyaronyo amewapiga chenga ya mwili hasa wale ambao husomaga vitu juu juu! Ukisoma kwa makini hii habari utagundua moja kwa moja kwamba hapa HAHAMI MTU HAPA TOKA CHADEMA! Kwa kifupi ni kwamba amemchanachana Rais Kiwete kwa kumkebehi kuwa ni MTU MWENYE SURA NZURI NA MPOLE SANA anayeishia kuwasamehe WAIZI WA FEDHA YA EPA,PEMBE ZA NDOVU na WAUZA MADAWA YA KULEVYA. Ameendelea kumsifia Kiwete kwa kuwa ni mtu mcheshi mwenye tabasamu wakti wote ilhali Viongozi wa CHADEMA hawana.

Kwamba Viongozi wa CHADEMA WANA SURA MBAYA,WEUSI,WAKALI NA WAKTI WOTE WAMENUNA!Hawa hawana huruma na mtu kwa hiyo Kicheere ameamua kuhama CHADEMA kwa sababu hizi ambazo kiukweli zinanogesha tu hii habari yenyewe ili kujaribu kuonyesha tofauti iliyoko kati ya CCM na CHADEMA!!!

HAHAMI MTU HAPA!
 
Someni vizuri na kutafakari mtaona kuwa mtoa mada anamlaumu mtawala wa nchi kwa kuachia mambo yaende kama hakuna mtawala. Wa tz wengi tunakimbia huku tumefumba macho matokeo yake tunabaki mbumbumbu. Hiyo ni fasihi jamaniiiiiii.
 
Rais ni bwana malalamiko hawezi kutenda. Oh mara nina majina ya vigogo wauza unga, mara majangili yako 40 na yanaongozwa na tajiri mmoja kule Arusha tunayafahamu. So what?
 
@nyaronyo mwache kikwete apumue kaka,
maana hizo makala zako zinamuumiza ila basi anashindwa afanyeje.
 
Safari njema Nyaronyo, huenda mtakuwa katika mahusiano mazuri na Kikwete, maana wiki iliyopita ulilalamika kuachwa katika uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba, licha ya kukidhi vigezo vyote

Mkuu sina hakika kama kweli anaweza kuhamia huko kwa hizo sababu zilizotolewa. Hiyo ni kumponda mkuu was pori kwa mgongo wa nyuma
 
Nimegundua humu ndani kuna watu wenye upeo mdogo sana Wa kufikiri dah shida..
 
Mkubwa usisumbuke kichwa hicho ni kipimo kuwa matoto ya Lumumba huwa hayasomi. Kicheere ametumia tasfida kutukana ila matoto ya Lumumba a.k.a Mavisebengo hayajaambulia kitu.

mkuu hivi kweli mtu anaweza kuamliwa aukalie ubongo wake namna ile naye akakubali kweli?
 
Changia hoja, acha kunitamani. Au uantaka kusema sura yangu inafaa niwe nimehamia CCM tangu zamani? Mimi wa huku huku kwa sura mbaya ila sheria tunafuata

Hahaha msg sent na mimi nahamia ccm nikavune rasilimali zetu serikali sikivu itansamehe tu sababu ntatoa pia mchango kwa chama najua uchaguzi unakuja na bila hela hawatashinda
 
Mwandishi Mahiri wa Makala na Mwanasheria wa Jijini Dar es Salaam Nyaronyo Mwita Kicheere amehamia CCM, kati ya sababu kubwa zilizomhamisha CHADEMA, anasema Viongozi wake hawana sura ya Tabasamu, tofauti na viongozi wa CCM, Kikubwa zaidi anasema ameamua kuipenda CCM kwa kuwa Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete ni mtu Rahimu, anayependa watu wake na kuwahurumia kutokana na magumu ya maisha, Juzi juzi ametangaza jinsi alivyopelekewa orodha ya majangili 40 wanaotikisa mbuga zetu lakini hakuwachukulia hatua yeyote kwa kuwa wanafanya ujasiriamali kujikimu na wanaweza kuwekeza. Nyaronyo amesema pia, anahamia CCM kwani kesho au keshokutwa akikamatwa na ngozi ya Chui, ya Mamba, au meno ya Tembo atapata msamaha kama wale 40 waliosamehewa na Kikwete.

Nyaronyo anasema, CHADEMA wangekuwa madarakani leo, ambao viongozi wao hawana tabasamu, akamtaja Mbowe Slaa, Lissu na Lwakatare nchi isingekalika, maana ni wazee wa visasi, maana Wezi wangekamatwa, watekaji wangesakwa, wauza dawa za kulevya wangekuwa wote gerezani.

Tena akaongeza kuwa hii si mara ya kwanza Kikwete kusamehe. Amesamehe Majangili 40, kama alivyosamehe wezi wa EPA, Nyaronyo anasema Tumshukuru Mungu kwa kuwa na Kikwete, Rais anayesamehe. = Chanzo gazeti la -----

Hii Nyaronyo kaaiandika kwa mtindo wa kejeli so inataka kuwa angalu mwelewa wa fasihi angalau kidogo kuing'amua
 
Back
Top Bottom