Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nyaronyo Kicheere 'ahamia CCM'

Nimesoma post ya kwanza na nyingine kama nne hivi nikagundua kwamba watu huwa wanasoma heading na kuanza kuchangia! Kwenye hii post eti unakuta mtu anamini kwamba Nyaronyo kaenda CCM na kuuliza kafuata nini huko wakati alikuwa akiitukana!
Tena Nyaronyo kaitukana vibaya CCM lakini ajabu eti watu wanashangilia na kusema Chadema inazidi kufa kwa watu kama Nyaronyo kwenda CCM. Wanashindwa kusoma makala yenyewe vizuri wanaishia kushangilia ujinga. Nyaronyo makala zake nyhingi anatumia lugha ya Picha na kama una akili fupi huwezi kumuelewa vema au ukiishia kusoma kichwa cha habari unapotea
 
Kwa Hii michango katika thread Hii elimu ya Tanzania IPO mashakani. Kama sie ndio wasomi hapa nchini and yet hatuwezi hata kutofautisha aina za uandishi ni hatari. Makala Hii bila hata kuwa elimu kubwa unaona kabisa kwamba imeadikwa kwa mfumo wa kejeri(ironic). Kawambwa una kazi!
 

Huyu si alisema Kikwete anamchukia bila ya sababu? Kafuata nini tena huko CCM?


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...cheere-kikwete-ananichukia-bila-sababu-3.html

Nyaronyo-Mwita-Kicheere.jpg

Umejidhalilisha sana wewe! Kumbe wewe ni Zombie kiasi hicho!
 
Kwa Hii michango katika thread Hii elimu ya Tanzania IPO mashakani. Kama sie ndio wasomi hapa nchini and yet hatuwezi hata kutofautisha aina za uandishi ni hatari. Makala Hii bila hata kuwa elimu kubwa unaona kabisa kwamba imeadikwa kwa mfumo wa kejeri(ironic). Kawambwa una kazi!

Mkuu vijana wa sasa hivi hawawezi kuchambua habari. Wamebakiza kukariri. Utakuta wote wanaopiga kelele ni under 30.
 
Mkuu New Force, jameni hizi avatar nyingine!, muwe na huruma japo kidogo, wengine wenzenu tuu dhaifu, hivyo avatar kama hizi ni kutiana tuu majaribuni!, badala ya concenrate na suject matter unajikuta unaishia kukodolea macho avatar huku mawazo yakikupeleka kwengine!.

Hebu wewe jifikiriea avatar kama hii halafu msomaji post ni mtu wa Kanda ya Ziwa!.

image.tiff


Pasco.

Mzee mwenzangu Pasco nimependa joke yako ila unajaribu kuwaponya jamaa kiaina. Kusema kweli watu kama T2015CCM na thatha ni wachangiaji wakubwa sana kwenye jukwaa hili la siasa, lakini bila kuchenga chenga uwezo wao wa kuelewa ni mdogo mno. Sasa kama alivyo andika Nyarongo kicheere katika lugha ya fasihi inayoweza kutafsiriwa na kijana makini wa kidato cha pili hawa watu niliowataja hapo juu watakuwa na elimu gani?
Nilipata kushauri huko nyuma kuwa JF pamoja na uhuru wake kuchangia,sio lazima kila kitu mtu achangie. Waweza mtu kusoma na kujifunza na hiyo ni faida ya bure kabisa. Wapo watu humu hata mada hajaielewa lakini unakuta kesha weka zaidi ya post 20 kwenye thread hiyo hiyo na ni pumba tuu mpaka watu makini wana zira kuchangia wakati wana mambo ya msingi wangeweka humo na watu kufaidika.
Hivyo kaka tusiwaonee haya wachafuzi wasioelewa bali tuwape kavukavu kuwe ni mbumbumbu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom