Nyaraka: Mkutano wa CHADEMA na Rais Kikwete - Ikulu ya Dar es Salaam

Juma Duni Haji alikuwa analijibu swali hilo kupitia ITV usiku huu.

Alimtaja Nyerere kuwa ndiye aliyeifuta Tanganyika na waraka alikuwa nao mkononi anausoma, siukumbuki ni upi.

ni suala la muda tu tanganyika yetu ya ukweli itarudi.
 
Juma Duni Haji alikuwa analijibu swali hilo kupitia ITV usiku huu.

Alimtaja Nyerere kuwa ndiye aliyeifuta Tanganyika na waraka alikuwa nao mkononi anausoma, siukumbuki ni upi.
Aseee!! Msahaulifu sana wewe eeh!!
 
Kweli dunia ya Mungu ina mambo! Waraka uliowakilishwa mreeeeeefu makubaliano yaliyosainiwa na Mnyika na Nchimbi hata ukurusa hayafiki! Kuna makubaliano mawili tu ambayo nadhani si makubaliano ila wamekubaliana kutokukubaliana kama alivyosema hap FF!
 
Duh! Nimeona kikubwa ni chadema wanataka wapate wawakilishi wengi kwenye bunge la katiba kuliko CUF bac.
 
I wish ... Tungepata kwa KINA makubaliano Rasmi Kati ya Rais na CDM yaliyofikiwa kutokana na nyaraka hizi!!
Wamekubaliana kutokukubaliana.
Kwa namna hii, Kila jambo litaendelea sawa na kama Kikao hicho hakikuwahi kuwepo.. Yaani Mswaada Utasainiwa na kuwa sheria na CDM hawakufanikiwa kuleta 'impact' yeyote?
Subiri tu; tutayapata. Haipiti Ijumaa
Leo Jumatatu! Hadi ijumaa? Kumbe ni siri kiasi hicho?
 
Ukisoma mikinzano iliyopo kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Tanzania bara unajikuta unahitaji mwanasheria kutueleza nini kinaendelea Tanzania.

Si ajabu ndo maana tunatumia leseni za aina mbili na zote zinakubalika, noti za aina mbili na zote zinakubalika. Kila kitu OVYO!

Na katiba za aina mbili, na zote zinakubalika!
 
Huo ni muziki mnene, wenye uwezo waucheze!! Tunaambiwa tujadili kuuboresha jinsi ulivyo!! Kazi kwelikweli!!!!
Toeni maoni yenu kwenye hii ambayo tumeshaamua, msibadilishe kitu!!
sasa maoni ya nini kama hakuna kubadili kitu!!
 
Kingine kikubwa kwenye mapendekezo "ni swala marekebisho ya katiba ya zanzibar" inaonesha chadema hawakuwayafurahia hata kidogo...

Lakini big up kwa kutaka kuleta Tanganyika ..yes we can tunahitaji Tanganyika
 
Nadhani ukiutazama huo waraka wa magwanda wanashindwa kuelewa kuwa Zanzibar ni nchi, ina Rais wake, ina Katiba yake, ina Bendera yake, ina Wimbo wake wa Taifa. Na hapa ni nchi zimeungana tu, na hata huo waraka uliwekwa wa 1964 ni amendment tu, jee waraka orijino kabla haujawa amended uko wapi?
 
Hivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?

Limekuwa ni swali langu la msingi tangu nilipopata ufahamu mzuri mwaka 1967 nikiwa darasa la nne hadi leo. Na bado najiuliza je tanganyika ilipotelea wapi????????????????
Leo hii bila aibu wala hata kwa kukosa soni usoni wanasema wanasheherekea uhuru wa Tanzania bara. Hii ni nchi gani? is it the same Tanganyika or is the bastard..............?????
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Umewahi kusoma thread hii?

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/1438-muungano-na-kero-zake-tuuvunje.html

Uka-download attachment hii?

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=5120&d=1246436738

utiajisaini.jpg

Mkataba wa makubaliano ya kuanzisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukisainiwa mwaka 1964.

Nimekupata mkuu.... nimedownload haraka sana. Thanks
 
Ndugu zangu, hii taarifa naona ina kosa la kiuandishi, theluthi moja ya 81 ni 55?

Kweli nimeona, sasa hapa magwanda ndipo wanaponichosha

  • Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, jumla ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa sasa ni 81;

  • Sheria inaelekeza kwamba idadi ya wajumbe wanaotoka Zanzibar katika Bunge Maalum la Katiba ambao wanatoka nje ya Bunge na Baraza la Wawakilishi "... haitapungua theluthi moja ya Wajumbe hao." Theluthi moja ya wajumbe hao ni wajumbe 55;
 
Kweli nimeona, sasa hapa magwanda ndipo wanaponichosha

Jumulisha wabunge 81 wa baraza la wawakilishi na 83 wabunge toka zanzibar ambao wapo bunge la muungano unapata 164 ukigawa kwa 3 unapata 54.67 (sawa na watu 55 maana hakuna mtu 0.67)
 
Hivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?
Ukiangalia vizuri ni kama vile ZnZ wamefanya mbinu..........Tanganyika sasa ni koloni la Zanzibar.

Huwezi ukawa rafiki yangu, halafu ukataka kuhusika 100% kwenye matambiko ya kabila na ya kiukoo..........urafiki wetu kama uppo kwenye bar na ushabiki wa Man U basi unatakiwa uishie huko huko.
 
Limekuwa ni swali langu la msingi tangu nilipopata ufahamu mzuri mwaka 1967 nikiwa darasa la nne hadi leo. Na bado najiuliza je tanganyika ilipotelea wapi????????????????
Leo hii bila aibu wala hata kwa kukosa soni usoni wanasema wanasheherekea uhuru wa Tanzania bara. Hii ni nchi gani? is it the same Tanganyika or is the bastard..............?????
Hakuna swali linaloniumiza kichwa kama hili.Wapi Tanganyika ilifia?Kwanini Zamnzibar hawakuua jina lao?Pongezi kwa wazanzibar katika hili kuendelea na jina alo la asili.Sisi tunajidai tunajua wakati leo hii Muungano ukifa sisi tunapaswa kubadilisha jina hili la Tanzania.Bila zanzibar hakuna Tanzania.Naungana na wazanzibari wote wanaodai sis wabara tunawakandamiza.
Swali kubwa Uhuru wa Tanzania Bara au Tanzania?Kwanini tusiwe wakweli kuwa uhuru wa Tanganyika?Maana unaposema uhuru wa Tanzania unawajumuisha na wazanzibari.Kumbe kimsingi Zanzibar haipaswi kusherehekea sikukuu hii kwani nao wanasubiri yao.Je ikifika siku hiyo kwanini wasisherehekee?Pia kuna mkanganyiko unaoletwa na wazanzibar wenyewe.Kwanini hawana tarehe ya kusherehekea uhuru wao badala yake wanaungana na Tanganyika kusherehekea Desemba 9?Kusema uhuru wao ulikufa na kupewa wa kwetu?Watu wa historia wajibu hili.
 
Nadhani ukiutazama huo waraka wa magwanda wanashindwa kuelewa kuwa Zanzibar ni nchi, ina Rais wake, ina Katiba yake, ina Bendera yake, ina Wimbo wake wa Taifa. Na hapa ni nchi zimeungana tu, na hata huo waraka uliwekwa wa 1964 ni amendment tu, jee waraka orijino kabla haujawa amended uko wapi?
Tukuulize wewe na CCM yako mliotutawala tangu mwanzo..........nyie ndo wapangaji wa kudumu wa ikulu ..... kwa mujibu wa yule waziri asiyejua kazi yake......yule ambaye wajomba zake wapo wengi sana kule Kigoma.

Usilete hadithi za Nyerere hapa..........Sema CCm mmepeleka wapi original documents??
Kumbe huu mchezo wa ku-forge documents hamkuuanza leo sio??!!
 
Acheni ujinga wenu hata kama Muungano Zanzibar waende kivyao na sisi tubaki na Tanzania yetu,mimi sitaki kusikia upuuuzi unaoitwa Tanganyika
 
Back
Top Bottom