Nyaraka: Mkutano wa CHADEMA na Rais Kikwete - Ikulu ya Dar es Salaam

"mwongozo wa chadema umekaa vyema sem tatizo tuna wabunge vihiyo wengi sana kupitia ccm.ila naamini mapambano yanaendelea na ipo siku ccm itabakia historia kuwa waliwahi kuwa chama tawala
 
"mwongozo wa chadema umekaa vyema sem tatizo tuna wabunge vihiyo wengi sana kupitia ccm.ila naamini mapambano yanaendelea na ipo siku ccm itabakia historia kuwa waliwahi kuwa chama tawala

Mkuu unaongelea mambo naomba nikupe summary:

1. Katiba ya zanzibar na ubaya wake kwa JMT-hayo siyo issue kwa muswada uliopo kwa hiyo outright tuliweke kwenye dustbin

2. Wajumbe wa CUF wako wengi kupita wa chadema kwenye tume itakayoundwa - malalamiko ya ulaji -wakapambane bungeni wakishinda ok..

3. Tuuunde Tanganyika -kabla ya katiba mpya kwenye dustbin kabla ya kwenda -maana wenye kutaka hayo ya muundo wapeleke maoni tume..

Hakuna kitu hapo...nioneshe mimi sijaona hapo mkuu. eti wabunge na wataalamu wa chadema wamekaa wanalalama as if they if sometinh very important kumbe oops
 
Jumulisha wabunge 81 wa baraza la wawakilishi na 83 wabunge toka zanzibar ambao wapo bunge la muungano unapata 164 ukigawa kwa 3 unapata 54.67 (sawa na watu 55 maana hakuna mtu 0.67)
Dada FF
Hii signature yako vipi "Show forgiveness, speak for justice and avoid the ignorant." (Qur'an 7:199)
Nahisi ilipaswa iseme "forgive, do justice and educate the ignorant."
 
Wakuu, nimezinasa nyaraka hizi ambazo nimeziambatanisha kama attachment toka kwa sosi wangu ndani ya CDM na nimeona niwashirikishe:

Mosi, CHADEMA imemwambia Rais atumie mamlaka yake kwa mujibu wa ibara ya 97 akatae kusaini muswada kwa sababu zilizoelezwa kwenye sheria hii.
Pili, iwapo serikali haitafanya mabadiliko katika muswada husika CHADEMA haitashiriki mchakato ambao hautaleta katiba bora badala yake itaendelea kuunganisha nguvu ya umma kutaka mabadiliko ya msingi.
Tatu, CHADEMA imetaka suala la sheria hii lisiwe la mapendekezo ya CHADEMA pekee ila mjadala wa muswada huu urudi kwa wananchi na wadau wengine ili kuwa na wigo mpana wa marekebisho.
Nne, wakati marekebisho yakisubiriwa, CHADEMA itaendelea na mikutano nchi nzima katika ngazi mbalimbali ili kutoa elimu ya uraia kwa umma kuhusu sababu za kupinga muswada wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa na bunge ili kuuandaa umma kwa hatua za ziada kwa kadiri ya maazimio ya kamati kuu ya chama.

Barua ya awali ilitoka kwa Dr. Slaa na kusambazwa nchi nzima, na mapendekezo attachment ni yale waliyoyapeleka Ikulu (17pages).

Kazi ni kwenu!!!!

=============

tumekupata mkuu,nadhani Mh Raisi atayafanyia kazi,kwani ni msikivu na anajari sana maslahi ya nchi
 
Jamani mswada unasainiwa au la? Sijaona makubaliano hapo. Wapi Tundu na Mnyika, kamanda Mbowe ni mwana Jamvi. Wakiusaini huo mswada maana yake wameweka kapuni maombi yenu yote. Swala la kufanya marekebisho baada ya signature litakuwa alinacha. Tupeni kinagaubaga nini ni makubaliano sio mistari miwili isiyoeleweka.
 
Badala ya kujadili kile walichokutana Chadema na rais Kikwete, tunajadili nyaraka za siri za Chadema ambazo hazina maana yoyote kwenye katiba mpya
 
Nadhani chadema imechemsha. Makubaliano na serikali hayasemi wamekubaliana nini. Kama ni kwamba rais atautia saini huo mswada kabla ya kesho, na sheria inaanza kutumika kuanzia desemba 1, 2011, hakuna sababu ya kuamini kutakua na usahihishaji wowote wa hiyo sheria. Cdm wame "to let down" ile mbaya.

Macinkus
 
Hivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?

Mkuu ndiyo maana hatuendelei na kubaki maskini kwa kuisujudia Zanzibar, kuungana na Zenji kumetupotezea mwelekeo wa neema ya maziwa na asali, mzanzaibari anajiona ni zaidi mkuliko mbara, bisha! Tuchape kazi kwa kuachana na Zenji.
 
Juma Duni Haji alikuwa analijibu swali hilo kupitia ITV usiku huu.

Alimtaja Nyerere kuwa ndiye aliyeifuta Tanganyika na waraka alikuwa nao mkononi anausoma, siukumbuki ni upi.
Kama Nyerere aliifuta Tanganyika basi Watanganyika tunaitaka Tanganyika yetu leo hii. Hakupata ridhaa yetu ya kuifuta Tanganyika bali alitumia mamlaka ya u rais tu.
 
Hii ni nafasi nzuri sana kwa Watanganyika kudai Tanganyika yetu ambayo ilipotezwa kinamna kwa miaka zaidi ya 47 sasa. Na kwa maoni sioni sababu yoyote ya kubadili bendera wala mwimbo wa Taifa pindi Tanganyika itakaporudishwa rasmi kama nchi kwenye katiba mpya.
awa jamaa walifanya mlinganyo huu;

t[SUB]1[/SUB]+ z = t

where t[SUB]1[/SUB]= tanganyika
z= zanzibar
t= tanzania

but t[SUB]1[/SUB] ~ t
then the equation becomes t + z = t

hapo ndipo TANGANYIKA yangu ilipo fia duh !!!!!
H
 
awa jamaa walifanya mlinganyo huu;

t[SUB]1[/SUB]+ z = t

where t[SUB]1[/SUB]= tanganyika
z= zanzibar
t= tanzania

but t[SUB]1[/SUB] ~ t
then the equation becomes t + z = t

hapo ndipo TANGANYIKA yangu ilipo fia duh !!!!!
H
Ma Eng utawajua na assumption zao, upo juuu mkuu kwa kutoa derivation ya Tanganyika ilipopotelea.
 
Taarifa nzima imeshiba maslahi ya Taifa Tupu asanteni CDM kwa kuweka maslahi ya Taifa mbele.


MUSWADAwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 uliopitishwa na Bunge hivi
karibuni utasainiwa na Rais Jakaya Kikwete kama ilivyopangwa.

Hali hiyo inatokana na makubaliano yaliyofikiwa jana kati ya Rais na Kamati ndogo ya Chadema iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe.
 
Hivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?

Kuna Mzee wetu mmoja mwenye kuheshimika sana na ambaye ni 'icon' hapa nchini na mmoja wa waasisi wa muungano aliwahi kutufundisha hesabu akasema '1 na 1 ni 2 na siyo 3 wala 1!! Ndiyo maana Tanganyika na Zanzibar zilipoungana zilitokea serikali 2 ( ya muungano na ya Zanzibar)!! Pamoja na kumheshimu sana mheshimiwa huyo katika hili nilichagua upande wa kukosa maksi kwenye hiyo hesabu.
 
Back
Top Bottom