Nyaraka: Mkutano wa CHADEMA na Rais Kikwete - Ikulu ya Dar es Salaam

Rais akiomba ushauri kwa watu type ya maralia sugu na faizafoxy jamaa watakuwa wamepoteza muda wao bure wa kunywa beer na mbuzi katoliki.
 
Acheni ujinga wenu hata kama Muungano ukivunjika Zanzibar waende kivyao na sisi tubaki na Tanzania yetu,mimi sitaki kusikia upuuuzi unaoitwa Tanganyika
 
Nadhani ukiutazama huo waraka wa magwanda wanashindwa kuelewa kuwa Zanzibar ni nchi, ina Rais wake, ina Katiba yake, ina Bendera yake, ina Wimbo wake wa Taifa. Na hapa ni nchi zimeungana tu, na hata huo waraka uliwekwa wa 1964 ni amendment tu, jee waraka orijino kabla haujawa amended uko wapi?
Nchi zipi ziliungana na kama ziliungana mbona moja bado ipo nje ina maana yenyewe haikuingia ndani.
 
Wanaficha huo Mkataba kwa manufaa ya nani wakati nchi ni yetu sote? Ukiona mtu anatumia nguvu kuficha kitu, ujue ndani yake kuna sumu.
 
​Ngoja nikaongee na pande zote mbili kwanza nipate ufafanuzi wa hoja zao halafu ndo nitakuja nichangie.
 
Hii kitu imenivutia sana hii...........labda tuanze kudai Tanganyika yetu kutoka pale Lumumba.
 
Rais akiomba ushauri kwa watu type ya maralia sugu na faizafoxy jamaa watakuwa wamepoteza muda wao bure wa kunywa beer na mbuzi katoliki.
kwahiyo JK akipewa nondo kama hii anamuita FF na MS ndo wampe ushauri???
kweli kabisa Tundu Lissu angeenda zake kula mdudu na nyagi tu!!! kama unafanya kazi kama hii halafu inaenda kujadiliwa na that type........Lukuvi !! nchimbi???!!
 
Nchi zipi ziliungana na kama ziliungana mbona moja bado ipo nje ina maana yenyewe haikuingia ndani.
Mkuu, ukisoma vizuri alichoandika huyu mama utagundua she is just bluffing!!
By FaizaFoxy
Nadhani ukiutazama huo waraka wa magwanda wanashindwa kuelewa kuwa Zanzibar ni nchi, ina Rais wake, ina Katiba yake, ina Bendera yake, ina Wimbo wake wa Taifa. Na hapa ni nchi zimeungana tu, na hata huo waraka uliwekwa wa 1964 ni amendment tu, jee waraka orijino kabla haujawa amended uko wapi?
 
Nimefurahi sana, Chadema kuwa wawazi na kuamua kuweka mambo hadharani, nawapongeza viva. Sasa tunapata picha ya utata uliopo kwenye huu muungano, walificha sasa wanaumbuka. Wazanzibar wenyewe ndio walianza kuukataa muungano sasa na sisi tunapigilia nyundo. Lakini inaonyesha hapo Zanzibar pana siri fulani lazima tuwemakini, wameshaunda katiba yao na wana Rais wao waendelee kivikwao na tuwaache wawe huru wajenge nchi yao. Waliofanya muungano walikuwa watu wawili Nyerere na Karume bila kushirikisha watanzania na sissi hatuwezi kuunga mkono wakati wezetu wamekunja shingo.
 
Kuna wengine hawajui hata tunachodai hatudai jina la Tanganyika tunachodai ni sovereignty ya tanganyika, kazi kweli ndio maana kina Lissu wanapata shida bungeni.

Tukipata sovereignty ya Tanganyika ndio itatusaidia vipi kiuchumi? Ndio tuseme ufisadi unaisha, barabara zinajengwa zaidi, watoto yatima wanapungua, nk? Mbona mawazo yako mafupi kama mkia wa mbuzi?
 
Hivi, Zanzibar iliungana na Tanganyika zikatengeneza Tanzania. Tanganyika ilipotelea wapi?


Hii ni nafasi nzuri sana kwa Watanganyika kudai Tanganyika yetu ambayo ilipotezwa kinamna kwa miaka zaidi ya 47 sasa. Na kwa maoni sioni sababu yoyote ya kubadili bendera wala mwimbo wa Taifa pindi Tanganyika itakaporudishwa rasmi kama nchi kwenye katiba mpya.
 
Hii ni nafasi nzuri sana kwa Watanganyika kudai Tanganyika yetu ambayo ilipotezwa kinamna kwa miaka zaidi ya 47 sasa. Na kwa maoni sioni sababu yoyote ya kubadili bendera wala mwimbo wa Taifa pindi Tanganyika itakaporudishwa rasmi kama nchi kwenye katiba mpya.

Tukiipata Tanganyika ndo kinafuata nini? Siamini kama maoni ya wanaJF wanaodai Tanganyika si Wazanzibari waliovaa uTanganyika!
 
Acheni ujinga wenu hata kama Muungano ukivunjika Zanzibar waende kivyao na sisi tubaki na Tanzania yetu,mimi sitaki kusikia upuuuzi unaoitwa Tanganyika
mkuu, unajua kuwa bila ya Tanganyika huwezi kuwa na Tanzania?

Okay! Nisibishe alimradi. Tafadhali tujuze kwanini
basi huo ujinga wetu. Naomba tuelimishe kwanini mwenzetu unaona upuuzi hata kusikia tanganyija?
 
Hakuna swali linaloniumiza kichwa kama hili.Wapi Tanganyika ilifia?Kwanini Zamnzibar hawakuua jina lao?Pongezi kwa wazanzibar katika hili kuendelea na jina alo la asili.Sisi tunajidai tunajua wakati leo hii Muungano ukifa sisi tunapaswa kubadilisha jina hili la Tanzania.Bila zanzibar hakuna Tanzania.Naungana na wazanzibari wote wanaodai sis wabara tunawakandamiza.
Swali kubwa Uhuru wa Tanzania Bara au Tanzania?Kwanini tusiwe wakweli kuwa uhuru wa Tanganyika?Maana unaposema uhuru wa Tanzania unawajumuisha na wazanzibari.Kumbe kimsingi Zanzibar haipaswi kusherehekea sikukuu hii kwani nao wanasubiri yao.Je ikifika siku hiyo kwanini wasisherehekee?Pia kuna mkanganyiko unaoletwa na wazanzibar wenyewe.Kwanini hawana tarehe ya kusherehekea uhuru wao badala yake wanaungana na Tanganyika kusherehekea Desemba 9?Kusema uhuru wao ulikufa na kupewa wa kwetu?Watu wa historia wajibu hili.
Ukirejea kwenye somo la historia, ZNZ ilipata uhuru wake wa bandia (nadhani tarehe 10 dec. 1963 - sina hakika na tarehe wala mwezi) wakati Mdhungu alipoondoka na kuikabidhi nchi kwa vibaraka wa wamanga. Kuona huo sio uhuru, mwezi mmoja baadaye, Wazanzibari wakafanya Mapinduzi (matukufu?) hapo tarehe 12 Januari 1964. Hii ndio siku yao rasmi ya uhuru wao. Hata Watanganyika ikifika siku hii nao angalau hupata mapumziko hawaendi kazini. Watanganyika wao wanasherehekea siku ya uhuru wao tare 9 Dec., na Wazanzibar nao hupata siku ya mapumziko, na wote kwa pamoja, Watanganyika na Wazanzibari, husherehekea tarehe 26 Aprili, kama siku ya Muungano. Sasa nongwa ziko wapi?

Kuhusu nani aliua Tanganyika, bahati mbaya muuaji wa Tanganyika ameshakufa (na hapa ni kama kufiwa na mganga aliyekuroga). Kabla ya kutiliana saini mkataba wa Muungano, Nyerere alimtaka Karume aiite Zanzibar Tanzania Visiwani. Karume kwanza alicheka, "Wewe Nyerere zimakupungukia nini, nani asiyejua kuwa Zanzibar ni visiwa. Kwa nini basi Tanganyika tusiite Zanzibar Bara? Zanzibar itabaki kuwa Zanzibar,, kama ilivyoitwa na mababu wa mababu zetu; kama hutaki hamna Muungano" [Source: Babu yangu - R.I.P]. Masikini Nyerere akapwaya, mwenzake akaondoka na jina la nchi yake, yeye sijui alifanya nini na Tanganyika, kwani mpaka mkataba wa muungano unasainiwa, katika mkataba wote majina lyaliyotumika ni Tanganyika na Zanzibar, na hakuna popote pametajwa Tanzania. Soma hapa kwa maelezo zaidi: http://www.zanzinet.org/zanzibar/history/articles_union.html
 
Back
Top Bottom