Nyama ya NYANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyama ya NYANI

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MAMA POROJO, Feb 16, 2012.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kwa miaka mingi wakulima wa Kisarawe tumekuwa tukisumbuliwa sana na wanyama waharibifu hasa nyani na nguruwe, mwaka huu neema ya ajabu imetuzikia, kwani sasa hivi wapo wawindaji wengi sana kutoka jijini Dar es Salaam wakiwinda na kutega mitego kuwakamata wanyama hawa. Ni wiki ya pili sasa niko shamba sijaona nyani wala kishindo cha nguruwe mwitu usiku kama tulivyozoea miaka ya nyuma, tulikuwa tukiweka mtego jioni, asubuhi mtakuta bonge la nguruwe limeshikwa kwenye mtego, jamani leo ni wiki ya pili tukiamka asubuhi mitego zaidi ya mitano haina kitu.

  Nyama ya nyani inauzwa Dar kama nyama ya mbuzi, baada ya watu wengi kushidwa kuhimili bei za nyama ya ng'ombe na mbuzi kwenye mabucha. Naomba hali hii ya iendelee hadi msimu wa mwaka huu uishe, utupunguzie gharama za ulinzi wa mashamba.
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kama ni tamu kama ya mbuzi haina neno. Asante kwa kutujuza.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  utamaduni wa kula kila kitu sasa unaingia taratibu nchini, si ajabu tukajikuta tunakulana wenyewe kwa wenyewe huko mbeleni kama Asia.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  sili tena nyama!
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ni sisi tulichelewa kidogo kulijua hili, nyama ya nyani kule Mbinga/Songea ni bei mbaya kuliko nyama ya ng`ombe.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana kwa kuchelewa kugundua mbinu hii shirikishi.

  Nina kashamba kangu fulani mahali fulani huku Pwani, nilipopeleka kuku walisumbuliwa sana na vicheche. Nikatunga uongo, nikawaambia jamaa wa jirani pale kuwa siku wakimkamata kicheche wanipigie simu. Nikafika pale nikawapa 50,000/ na nikaondoka na yule kicheche, mbele ya safari nikamtupa.

  Jamaa wale majirani wakaniuliza, yule kicheche ulimfanya nini? Nikawaambia hamjui kuwa nyama ya kicheche inaongeza nguvu za kiume !!! hasa ukipata maini yake. Mpaka leo kuku wangu wanalala nje ya banda kwa raha zao.
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ha haa haa! Kweli Malila wewe ni mbunifu. Kwa hiyo unataka kusema umegeuza kicheche kuwa dawa kwa baadhi ya watu huko Pwani, sasa unastahili hata kubadil proffession (hamia JF Doctor). Yaan utakuwa umewandaa kisaikolojia kweli. Nimeipenda hii
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa itabidi nami nirudi Msanga nikachukue shamba, kwani uwepo wa wanyama hawa ulinikatisha sana tamaa. Nashukuru sana kwa taarifa zilizonifikia kwa wakati muafaka
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ukiweza kucheza na mazingira vizuri hupati taabu. Pale Vianzi kwa chini kidogo unapovuka kwenda kwa Wakorea,kuna kijito,zamani kulikuwa na mamba kibao,walisumbua watu sana. Kaja jamaa kawageuza mtaji. Baada ya mavuno ya mamba na shamba kaacha anafanya biashara nyingine kabisa. Ukipata changamoto fulani,usiiangalie upande mmoja tu,huenda ukiigeuza upande wa pili kukawa na dili.
   
 10. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hata Arusha mto wa mbu mika ya 1996 nyama ya sokwe ilikuwa inauzwa sana pale sijui kwa sasa
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Wao ndio wamepata faida kuliko mimi,nimewaongezea idadi ya vitoweo,kwa sababu zamani kicheche alikuwa haliwi,pili wanapata protein natural kabisa,tatu wanapata kitowea kwa gharama karibu na sifuri. Na mimi kuku wangu wanaongezeka, hii ndio inaitwa win-win !!!!!!!!!
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  au ndo ileeem mishkaki ya pale mwenge kuanzia jioni ya sa moja hvi??????
   
 13. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Angalia usiharibu biashara za watu humu, Mikatabafeki
   
 14. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ngoja siku uende ukatembelee mifugo yako halafu wanakijiji wenzio wakukaribishe Ugali. Sijui utafanyaje?
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kwisha habari yako!
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Tayari yalishanikuta,

  Siku hiyo nikavamia ugali kwa nyama,baadae ndio wakasema,eti kweli mimi mkulima. Nikawauliza kwa nini? Tulidhani wewe huwezi kula nyama pori. Kumbe walipika nungu nungu mkuu, nyama ya nungunungu ni tamu balaa.
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Anzia na Buguruni Chama pale na hata pale posta mbele ya Bilicanas............mchana kweupe! hata sasa naelekea hapo kuila!
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  kuwa nimeshakula nyama ya nyani,,,,,,,,haiwezekani..:shock:
   
 19. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haa haaa haaaa, kwii kwii kwiii. Huko ndo kusocialize sasa na wanakijiji. Lakin kama hukudhurika, right? Itabidi nami nitaitafute ili niionje kama ni tamu namna hiyo. Mimi kuna nyama niliwahi kula pale zizi la ng'ombe (Iringa) lakini habari iliyotokea sasa! nadhan si busara nikiweka hapa.. (Sijui alikuwa Mbwa yule).
   
 20. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asia wanakulana???:lol::lol: hawayaisha tu?
   
Loading...