Mkuu,mafanikio unayatafsiri wewe mwenyewe muhusika na sio kusubiri kutafsiriwa na watu wengine,
Mafanikio ni kutimiza malengo uliyojiwekea,mfano ukiwa na Baiskeli ila ukawa una malengo ya kuja kununua Pikipiki,na ukainunua hiyo Pikipiki,basi hayo ni mafanikio kwako,umepiga hatua na umefanikisha lengo lako,
Jambo lolote ukiliwekea mikakati,plani na juhudi kisha ukalitimiza,basi hayo ni mafanikio kwako,
Tusisubiri maisha yetu kutafsiriwa na watu wengine.
Love the life you live
Live the life you love.