Nukuu 10 za Jenerali Mabeyo

Kwanini alishangaa CDF kushindwa kuwaamuru madaktari ili aondolewe Hosptal?

Yeye kama AMIRI JESHI kwanini hakutoa amri hiyo?

Je,ni kwanini alikuwa na uwezo wa kufanya maandalizi ya kifo? Au kuna kitu alikiona kisicho kuwa sawa alitamani kukiepuka lakini protocol za kitabibu zilimzuia?

Vyovyote itakavyokuwa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Jenerali Mabeyo anaielewa, anaifahamu, aliapa kuitunza, na ameitunza vilivyo Katiba ya JMT. Kwa hili Jenerali Mabeyo apewe maua yake!
Lakini tumesikiliza upande mmoja tu. Tungesikiliza na wengine waliotuhumiwa kwenye hili (si wapo?) tungepata picha kamili
 
Walijua ni mwanamke na upokeaji wake wa taarifa za msiba ungeweza usiwe na uvumilivu kama kwa wanaume!!

Kumuita na kumwambia leo mzee kaandaa sherehe ikulu! Halafu ndiyo anapewa ujumbe
Wakati alikuwa tanga? Au alirudi magogoni kwanza?
 
Katk yote sijaona naFas ya Jaji mkuu ambae ndio mratb wa maswala ya kiitifak na kikatba akipew nafas
 
Kwanini alishangaa CDF kushindwa kuwaamuru madaktari ili aondolewe Hosptal?

Yeye kama AMIRI JESHI kwanini hakutoa amri hiyo?

Je,ni kwanini alikuwa na uwezo wa kufanya maandalizi ya kifo? Au kuna kitu alikiona kisicho kuwa sawa alitamani kukiepuka lakini protocol za kitabibu zilimzuia?

Vyovyote itakavyokuwa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Order zinafuata channels. Na kwa walio kuwepo mtu wa kwanza kupokea amri ni huyo venance. Ila kwakuwa magu alikuwa kitandani na hajiwezi hakuwa na namna hata kama angegomewa na DAS kuna wakati ukifika cheo mamlaka utajiri heshima nguvu vyote vinakuwa havina msaada kwako. Hata mwanao akitaka kukuzaba makofi anaweza na huwezi mfanya lolote
 
Katiba inavunjwa kila mara na kuleta madhara makubwa kwa nchi..watu wasiofaa kuwa viongozi wanakuwa viongozi kupitia uchaguzi haramu unaovunja katiba ya nchi kwa kupata viongozi wasiostahili kuwa viongozi..kunapotokea nafas ya kiti cha urais ni nafasi pia ya kujisahihisha inawezekana hao walitaka kuvunja katiba wakati huo wa msiba wangeleta nafuu na kurekebisha makosa yaliyofanyika na pengine hali ingekuwa njema kuliko ilivyo sasa..ukisoma jinsi Mungu alimuweka Mfalme Daudi badala ya Mfalme Sauli si kwa njia inahojenga amani..lakini angalia baada ya Mfalme Daud kushika madaraka mambo yalibadilika kuwa mazuri zaidi ya wakati wa Mfalme Sauli..sisi ndio tunasema katiba ilitaka kuvunjwa na si Mungu alipanga nini baada ya Rais aliyekuwepo kufariki...!
Bora angewasikiliza hI wenye maono nchi isingekuwa mikononi mwa mafisadi kama ilivyo sasa
 
INASIKITISHA KWA KWELI. hata hivyo, ndugu zangu, tujiandae kwa vitu viwili au vitatu, hata wale watu wa hali za kawaida na wa hali za chini. cha kwanza, jiandae nini utaachia watoto wako utakapokufa ghafla (ukifikiria hili utakuwa pia na nidhamu ya kuishi, acha dhambi usife mapema), pili, jiandae kufa katika Bwana, ni bora ufe katika Kristo kuliko kufa ukiwa na dhambi (bila kuokoka), mwisho ambalo linafanana na la pili, andaa moyo wako, kwamba ikiwa hautakufa hadi Yesu arudi basi usiachwe.

kuna kitu kingine, achana na imani potofu, imani ambayo hata mitume hawakuwa nayo, unapokuwa mgonjwa, kuita padre (ambaye hata hajaokoka ila ni mshika dini) ati akupake mafuta. mafuta hayasafishi dhambi, unatakiwa kutubu dhambi zako ili usamehewe, kafara la Damu ya Yesu Kristo ndilo linafuta dhambi, sio mafuta yaliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, Yesu hakufa bure, hakuna mbadala wake. Biblia inasema aziungamaye dhambi zake atasamehewa ila yule anayezificha hatafanikiwa. padre naye ana dhambi zake, akupake mafuta wewe usamehewe dhambi au akupeleke mbinguni si angeyaoga kabisa yeye ili aende mbinguni kulivyo kuzuri? mbona tumekuwa vipofu?

Mwisho, kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa. unaweza kuwa rais, waziri, kiongozi wa dini, askofu n.k, utakuwa personally accountable kwa Mungu, hivyo ni jukumu lako kutengeneza moyo wako na Mungu kibinafsi ukiwa hapa duniani, baada ya kifo ni hukumu hakuna kuombewa na padre ili maiti isamehewe dhambi, never.
Hii comment na mada,wapi na wapi! Kwa hiyo,wanaowahi kutoweka,wana dhambi? Kwamba we unaeandika, ni msafi huna dhambi! Haya,anaeongelewa hapa, unamaanisha dhambi zilifika wingi wake ndo zikamtoa uhai??
Imani nyingine ni ajabu sana.
 
Tatizo hata imani za mitume huenda zikawa ni imani potofu : hatujui imani sahihi ni ipi for sure . Unayodhani kuwa ni imani sahihi., kuna maeneo inaonekana ni imani za majini na uchawi.

Imani bora ni kuheshimu imani za wengine, mila na desturi zao.
Kama zimo,aelewe
 
Kwanini alishangaa CDF kushindwa kuwaamuru madaktari ili aondolewe Hosptal?

Yeye kama AMIRI JESHI kwanini hakutoa amri hiyo?

Je,ni kwanini alikuwa na uwezo wa kufanya maandalizi ya kifo? Au kuna kitu alikiona kisicho kuwa sawa alitamani kukiepuka lakini protocol za kitabibu zilimzuia?

Vyovyote itakavyokuwa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Kuna watu watajisifia walikokaa,wengine watasifu, na wengine watalaumu.
Je, uliwahi kujiuliza kwa nini meza ya kikao cha mawazili au kamati ya raisi hua ni duala, na si mmoja anakaa nyuma ya mwenzake?

Unadhani mambo mengine yanayoonekana ya ajabu au ya ovyo,hao CDFs wanapopokezana,hawayaoni! Unadhani, hicho kiti wao hawatamani kukikalia?
Je, kwa nini hawajaribu! Unahisi nguvu ndo hawana!

Ila, kati yao na hivyo vitu kuna fensi.
Na hili jambo ukilifikilia kwa mapana, nyuma yake kuna mengi sana. Na hapo ndo kaongea kwa mafumbo,hakika wengi hawataelewa.

Kikawaida,si yo yeye alietakiwa kutangaza hizo taarifa.
Na kama alikuwa ameruhusiwa,basi hilo jambo lilienda kirafiki kuliko kikazi.

Enewe,ni mengi ya kuongelewa,na kila mtu ataongea ya kwake,ila,wale watu wa karibu,wanaokaa ile meza,ndo wenye majibu sahihi. Japo pia na wao hawatakwambia,maana hayakuhusu. Tujilie wali wetu,dona au sembe,tununue bando zetu, tuingie jf tuburudike,lakini mambo ya huko juu,hatuyawezi.
 
1. Magufuli aliomba akafie nyumbani kwake, maana alisema hawezi kupona.

2. Alishangaa nilipomwambia sina mamlaka ya kuruhusu hilo.

3. Aliomba aitiwe Paroko wake, Pd Makubi na Kard. Pengo ambao walifika na kumpa upako wa wagonjwa!

4. Alikata roho mbele yetu wakuu wote watatu wa vyombo vya usalama.

5. Makamu wa rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi hawakuwepo Dar. Tukaamua kuwaita Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi ambao walifika na kuwapa taarifa ya msiba.

6. Ilibidi tutumie njia nyingine kumjulisha makamu wa rais ambaye ndiye alitakiwa kutangaza taarifa ya msiba.

7. Kulikuwa na mjadala kipi kianze kati ya mazishi na kumwapisha makamu wa rais kuwa rais.

8. Wengi walishauri yafanyike mazishi kwanza, lakini nilishauri uapisho uanze kwanza, kwa sababu marais wa nchi nyingine walitakiwa wapokelewe na rais wa nchi.

9. Lilikuja suala la gwaride la uapisho ambapo walishauri kusiwe na gwaride. NILIWAKATALIWA kwa sababu aliyekuwa anaapishwa ni amiri jeshi mkuu,na lazima bendera ya amiri jeshi mkuu ipandishwe kwa gwaride. Kinyume na hilo, jeshi LISINGEMTAMBUA kama amiri jeshi mkuu.

10. Kulikuwa na baadhi ya mawazo, kwamba inakuwaje juu ya makamu wa rais kushika nafasi ya urais. Nadhani walisahau kuwa katiba ya nchi inasema nini, ikiwa rais aliye madarakani anafariki au akishindwa kuongoza. Nami nilisema ni vema utaratibu huo ukafuatwa na ni jambo jema.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mabeyo (vipengere 7-10) VIONGOZI WOTE WAKUU walikuwa hawajui muendelezo wa madaraka ya Urais (succession) ikitokea Rais amekufa au hawezi tena kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya JMT.
 
Back
Top Bottom