CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,066
Ni miaka 3 imepita tangu Rais Magufuli afariki. Ni jambo la kawaida, hasa siku ya maziko au wakati wa kutangaza kifo, kutolewa taarifa za kina za mazingira ya kifo cha marehemu, na kama pengine marehemu alitoa kauli yoyote. Haikuwa hivyo kwa Hayati Magufuli.

Wengi walipenda na walikuwa na shauku, msiba tu ulipotokea, wafahamu kwa kina aliugua lini, alifikishwa hospitali lini, jitihada zilizofanywa katika harakati za kuokoa uhai wa marehemu, mpaka kushindikana, na hatimaye kuyapokea mapenzi ya Mungu. Kukosekana kwa taarifa hizo, kumesababisha maneno mengi, ya kweli na yasiyo ya kweli.

Miaka 3 baadaye, baadhi ya taarifa za kina zimetolewa na CDF. Siamini kama taarifa hizi zimetolewa tu ili kujifurahisha, bali kuna ujumbe umetumwa kwa wananchi.

UJUMBE MUHIMU
Kuna shida kwenye katiba ya nchi. Kuna vitu havijawa sawa na kwa uwazi. Kwa maelezo ya CDF, ni kwamba ni yeye CDF ndiye aliyetoa msisitizo wa kuwa ni Makamu wa Rais ndiye anatakiwa kuwa Rais, na siyo mwingine yeyote. Tena ameeleza kuwa ni yeye CDF ndiye aliyeelekeza kuwa inabidi makamu wa Rais aapishwe kabla ya maziko ya Rais maana bila hivyo jeshi haliwezi kumtambua kama ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.

Lakini pia zipo habari ambazo hazijawekwa wazi, huenda zikawekwa wazi siku za mbeleni, kuwa wale waliokuwa wakipinga Makamu kuchukua nafasi ya Urais baada ya kifo cha Rais, walieleza kuwa katiba inasema kuwa Rais akitoka bara, makamu atatoka visiwani. Na kwa vile aliyefariki alikuwa anatoka bara, urais ulikuwa nafasi ya bara, nafasi ya visiwani ilikuwa ni umakamu, hivyo makamu aendelee kuwa makamu.

HATARI ILIYOPO
Tusistegemee nyakati zote tutakuwa na CDF wa aina ya Mabeyo. **** siku tutakuja kuwa na CDF mwoga wa kutoa maamuzi na wanadiasa wakatii, au tukawa na CDF mwenye tamaa ya madaraka, anaweza kutumia nafasi ya kukosekana maelewano miongoni mwa wanasiasa, akayanyakua madaraka yeye CDF.

HITIMISHO
Tumepewa ujumbe ambao ni angalizo, kuwa tunatakiwa kuiweka sawa katiba ili kila jambo liwe wazi kwenye katiba, na katiba izibe mianya yote ya tafsiri zisizokusudiwa.

Mapungufu yetu ya katiba hayapo tu pale ambapo Rais atafariki akiwa madarakani, yapo maeneo mengi. Tangu enzi za Tume ya Jaji Nyalali, mapungufu ya katiba yamekuwa yakiainishwa, lakini wafanya maamuzi wamekuwa magumegume, wanafanya mabadiliko madogo madogo kwenye maeneo yale tu wanayoona yanawahakikishia kubakia madarakani hata bila ya matakwa ya umma.

Hata Samia ambaye nusura asiwe Rais kwa sababu ya sintofahamu za katiba, baada ya kuipata Urais, hataki katiba mpya kwa vile anaona iliyopo inamhakikisha mamlaka ya kuwa hata dikteta akitaka, bila ya kubughudhiwa. Amesahau kuwa bila ya hekima ya CDF huenda asingekuwa Rais. Manufaa yake binafsi yamefifisha hekima yake katika kuyaangalia maslahi ya Taifa.

Ni lini tutampata Rais mzalendo anayelitazama zaidi Taifa kuliko madaraka yake binafsi na manufaa ya chama chake? Kuwa na hawa viongozi wanaojali zaidi madaraka kuliko madlahi ya Taifa, kuna siku nchi itakwenda kwa namna isiyotarajiwa. Pongezi kwa CDF kwa kujali maslahi ya Taifa.
 
Ni miaka 3 imepita tangu Rais Magufuli afariki. Ni jambo la kawaida, hasa siku ya maziko au wakati wa kutangaza kifo, kutolewa taarifa za kina za mazingira ya kifo cha marehemu, na kama pengine marehemu alitoa kauli yoyote. Haikuwa hivyo kwa Hayati Magufuli.

Wengi walipenda na walikuwa na shauku, msiba tu ulipotokea, wafahamu kwa kina aliugua lini, alifikishwa hospitali lini, jitihada zilizofanywa katika harakati za kuokoa uhai wa marehemu, mpaka kushindikana, na hatimaye kuyapokea mapenzi ya Mungu. Kukosekana kwa taarifa hizo, kumesababisha maneno mengi, ya kweli na yasiyo ya kweli.

Miaka 3 baadaye, baadhi ya taarifa za kina zimetolewa na CDF. Siamini kama taarifa hizi zimetolewa tu ili kujifurahisha, bali kuna ujumbe umetumwa kwa wananchi.

UJUMBE MUHIMU:

Kuna shida kwenye katiba ya nchi. Kuna vitu havijawa sawa na kwa uwazi. Kwa maelezo ya CDF, ni kwamba ni yeye CDF ndiye aliyetoa msisitizo wa kuwa ni Makamu wa Rais ndiye anatakiwa kuwa Rais, na siyo mwingine yeyote. Tena ameeleza kuwa ni yeye CDF ndiye aliyeelekeza kuwa inabidi makamu wa Rais aapishwe kabla ya maziko ya Rais maana bila hivyo jeshi haliwezi kumtambua kama ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.

Lakini pia zipo habari ambazo hazijawekwa wazi, huenda zikawekwa wazi siku za mbeleni, kuwa wale waliokuwa wakipinga Makamu kuchukua nafasi ya Urais baada ya kifo cha Rais, walieleza kuwa katiba inasema kuwa Rais akitoka bara, makamu atatoka visiwani. Na kwa vile aliyefariki alikuwa anatoka bara, urais ulikuwa nafasi ya bara, nafasi ya visiwani ilikuwa ni umakamu, hivyo makamu aendelee kuwa makamu.

HATARI ILIYOPO
Tusistegemee nyakati zote tutakuwa na CDF wa aina ya Mabeho. **** siku tutakuja kuwa na CDF mwoga wa kutoa maamuzi na wanadiasa wakatii, au tukawa na CDF mwenye tamaa ya madaraka, anaweza kutumia nafasi ya kukosekana maelewano miongoni mwa wanasiasa, akayanyakua madaraka yeye CDF.

HITIMISHO
Tumepewa ujumbe ambao ni angalizo, kuwa tunatakiwa kuiweka sawa katiba ili kila jambo liwe wazi kwenye katiba, na katiba izibe mianya yote ya tafsiri zisizokusudiwa.

Mapungufu yetu ya katiba hayapo tu pale ambapo Rais atafariki akiwa madarakani, yapo maeneo mengi. Tangu enzi za Tume ya Jaji Nyalali, mapungufu ya katiba yamekuwa yakiainishwa, lakini wafanya maamuzi wamekuwa magumegume, wanafanya mabadiliko madogo madogo kwenye maeneo yale tu wanayoona yanawahakikishia kubakia madarakani hata bila ya matakwa ya umma..

Hata Samia ambaye nusura asiwe Rais kwa sababu ya sintofahamu za katiba, baada ya kuipata Urais, hataki katiba mpya kwa vile anaona iliyopo inamhakikisha mamlaka ya kuwa hata dikteta akitaka, bila ya kubughudhiwa. Amesahau kuwa bila ya hekima ya CDF huenda asingekuwa Rais. Manufaa yake binafsi yamefifisha hekima yake katika kuyaangalia maslahi ya Taifa.

Ni lini tutampata Rais mzalendo anayelitazama zaidi Taifa kuliko madaraka yake binafsi na manufaa ya chama chake? Kuwa na hawa viongozi wanaojali zaidi madaraka kuliko madlahi ya Taifa, kuna siku nchi itakwenda kwa namna isiyotarajiwa. Pongezi kwa CDF kwa kujali maslahi ya Taifa.
Andiko linajitosheleza, hongera Bams kwa kulitendea haki.

All in all pamoja na kuwa na CDF aliyenyooka, vilevile tumepata Rais muungwana sana.

Waliyoyafanya akina Bashiru Ally, Ndugai na Majaliwa Kassim Majaliwa kutaka kupora u-Rais wa Samia ni uhaini kwenye macho ya sheria.

Lakini Samia bado anafanya kazi na Majaliwa Majaliwa na bado amewaacha Bashiru Ally na Ndugai kama wabunge
 
1710738601909.png
Gen Venance Mabeyo akiwa na viongozi waandamizi wa Ulinzi na Usalama

Nimesikiliza clip ya mahojiano ya Mstaafu CDF Gen Venance Mabeyo na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali, Daily News.

Udhubutu wa kuyaweka mambo wazi ni kipaji na ujasiri ambapo nampongeza kwa dhati Gen Mabeyo kwa hilo.

Mambo mengi imekuwa utamaduni kuyafutika futika na hivyo ukweli kutojulikana.

Kwa dhamira njema kabisa, Gen Mabeyo amethibitisha kuliweka mbele Taifa kama kiapo chake kinavyomtaka, kulinda Katiba.
Huu ni ujasiri usio kawaida, maana kwa watu walafi wangeweka maslahi yao mbele kuliko matakwa ya Taifa na Katiba.

Tunaona umuhimu wa viongozi waadilifu, ambao siku hizi ni wachache.

Mungu akulinde Gen. Venance Mabeyo.
 
Back
Top Bottom