INASIKITISHA KWA KWELI. hata hivyo, ndugu zangu, tujiandae kwa vitu viwili au vitatu, hata wale watu wa hali za kawaida na wa hali za chini. cha kwanza, jiandae nini utaachia watoto wako utakapokufa ghafla (ukifikiria hili utakuwa pia na nidhamu ya kuishi, acha dhambi usife mapema), pili, jiandae kufa katika Bwana, ni bora ufe katika Kristo kuliko kufa ukiwa na dhambi (bila kuokoka), mwisho ambalo linafanana na la pili, andaa moyo wako, kwamba ikiwa hautakufa hadi Yesu arudi basi usiachwe.
kuna kitu kingine, achana na imani potofu, imani ambayo hata mitume hawakuwa nayo, unapokuwa mgonjwa, kuita padre (ambaye hata hajaokoka ila ni mshika dini) ati akupake mafuta. mafuta hayasafishi dhambi, unatakiwa kutubu dhambi zako ili usamehewe, kafara la Damu ya Yesu Kristo ndilo linafuta dhambi, sio mafuta yaliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, Yesu hakufa bure, hakuna mbadala wake. Biblia inasema aziungamaye dhambi zake atasamehewa ila yule anayezificha hatafanikiwa. padre naye ana dhambi zake, akupake mafuta wewe usamehewe dhambi au akupeleke mbinguni si angeyaoga kabisa yeye ili aende mbinguni kulivyo kuzuri? mbona tumekuwa vipofu?
Mwisho, kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa. unaweza kuwa rais, waziri, kiongozi wa dini, askofu n.k, utakuwa personally accountable kwa Mungu, hivyo ni jukumu lako kutengeneza moyo wako na Mungu kibinafsi ukiwa hapa duniani, baada ya kifo ni hukumu hakuna kuombewa na padre ili maiti isamehewe dhambi, never.