Habari wanajamvi!
Hoja yangu ni kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuwa na mzunguko mrefu kwa wateja wanaodai mafao yao.
Wanachama tumekuwa tukikatwa fedha kila mwezi na mwajiri hivyo hivyo kwa ajili ya kumsaidia huyu mwajiriwa pindi anapokosa ajira, kustaafu, na faidi zingine kama zilivyoelezwa kwenye taratibu zao za kuwahudumia wanachama.
Matarajio ya wengi ambao ni wachangiaji yamekuwa tofauti sana hasa kwa wanaokosa ajira, licha ya kuwa kwenye kipindi kigumu kifedha NSSF nao ambao kutokana na kukosa kwako ajira nataraji wakuongezee nguvu kwa kukupa stahiki yako mapema, badala yake wamekuwa na mzunguko mrefu sana na ahadi hewa unaweza kuambiwa subiri baada ya miezi mitatu itakuwa tayari lakini wapi.
Wanachama tunaomba mbadilike. Matarajio yetu ni hizo akiba zetu zitusaidie pale tu tunapokuwa na uhitaji nazo. Mlolongo wenu unatuumiza sana.