NSSF Tanzania na mzunguko mrefu wa ulipaji mafao

Uvombile

Member
Mar 23, 2014
73
51
Habari wanajamvi!

Hoja yangu ni kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF kuwa na mzunguko mrefu kwa wateja wanaodai mafao yao.

Wanachama tumekuwa tukikatwa fedha kila mwezi na mwajiri hivyo hivyo kwa ajili ya kumsaidia huyu mwajiriwa pindi anapokosa ajira, kustaafu, na faidi zingine kama zilivyoelezwa kwenye taratibu zao za kuwahudumia wanachama.

Matarajio ya wengi ambao ni wachangiaji yamekuwa tofauti sana hasa kwa wanaokosa ajira, licha ya kuwa kwenye kipindi kigumu kifedha NSSF nao ambao kutokana na kukosa kwako ajira nataraji wakuongezee nguvu kwa kukupa stahiki yako mapema, badala yake wamekuwa na mzunguko mrefu sana na ahadi hewa unaweza kuambiwa subiri baada ya miezi mitatu itakuwa tayari lakini wapi.

Wanachama tunaomba mbadilike. Matarajio yetu ni hizo akiba zetu zitusaidie pale tu tunapokuwa na uhitaji nazo. Mlolongo wenu unatuumiza sana.
 
Pole sana.
Mkuu hawana pesa hao..fedha zenu wamejengea majumba na nyingine wamekopesha.
Labda Wanavuta muda mliostaafu mpungue..wengine warip ili kupunguza makali ya ulipaji.

Ninafikiri mateso ni kwa mashirika yote ya hifadhi ya jamii ikiwemo PPF sidhani kama ni huko kwenu tu.
 
Mtoa mada umesema kweli isiyo na shaka labda mimi napendekeza waziri anayehusika na nssf atume vijana wake katika baadhi ya matawi nchi nzima wakaangalie hali ilivyo wanachama wanateseka sana kupata fedha zao.
 
Hili nimelisikia naona itakuwa vizuri kama litawafikia wahusika...
 
Wanashindwa kukuambieni ukweli, huko ndani Hakuna Pesaaa!!!!!
Itafika mahali tutakuwa tunawaambia waajiri wetu wasikate fedha zetu na kizipeleka huko NSSF, yani bora ikae benki niwe na kafixed account kangu hiyo inakuwa haina shida.
 
Mtoa mada umesema kweli isiyo na shaka labda mimi napendekeza waziri anayehusika na nssf atume vijana wake katika baadhi ya matawi nchi nzima wakaangalie hali ilivyo wanachama wanateseka sana kupata fedha zao.
Hapa ni kugomea mfumo wao ukipata ajira kwa wanaoendelea kitafuta ni kunegotiate na mwajiri hakuna kupeleka michango huko, huo mchango ni bora wakulipe tu kwenye mshahara wako.
 
Itafika mahali tutakuwa tunawaambia waajiri wetu wasikate fedha zetu na kizipeleka huko NSSF, yani bora ikae benki niwe na kafixed account kangu hiyo inakuwa haina shida.
Huyo muajiri hiyo jeuri ataitolea wapi!? Ila ni bora kila mtu angekuwa anakufa na chake tu.
 
A
Pole sana.
Mkuu hawana pesa hao..fedha zenu wamejengea majumba na nyingine wamekopesha.
Labda Wanavuta muda mliostaafu mpungue..wengine warip ili kupunguza makali ya ulipaji.

Ninafikiri mateso ni kwa mashirika yote ya hifadhi ya jamii ikiwemo PPF sidhani kama ni huko kwenu tu.
Asante mkuu ni mateso kwa kweli mwezi wa kumi nipo tu mafuatilia mafao ambayo ni halali ya jasho langu, utafikili naomba mkopo.
 
Hahaha unaanza kazi ukiwa na miaka 30, unafanya kazi kwa miaka 35 unastaafu ukiwa na 65, unaanza kufuatilia mafao kwa miaka 5, unaanza kulipwa ukiwa 70, unafariki baada ya miaka 5 mbele ukiwa 75.

Kwanini u hustle hivyo ili kuishi miaka 5 tu ya hayo mafao?!
 
jamani mm naomba namba za branch manager nssf temeke miezi inayoyoma kila siku kupigwa kalenda au ata za jenister mwagama
 
Back
Top Bottom