Kwanini watu wengi wanatumia muda mwingi kufuatilia mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii?

DOMINGO THOMAS

JF-Expert Member
Feb 16, 2023
266
227
- Tanzania kuna mifuko ya hifazi ya Jamii miwili:-
1. NSSF ( huu nikwa wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta zisizo rasmi )
2. PSSSF ( huu nikwa wafanyakazi walio ajiriwa na serikali pekee )
  • Mafao ni haki ya kila mwanachama wa mfuko, pindi anapo pata Janga la aina yoyote mfano uzee, kukosa ajira, kufiwa, na ulemavu.!
  • Pindi upatapo janga lolote una haki ya kupata mafao ikiwa unasababu kamili za kupata hilo fao.
- SABABU ZINAZO SABABISHA WATU WENGI KUFUATILIA MAFAO KWA MUDA MREFU :-

1. Mwanachama kutofuatilia michango yake kama ni kweli anachangiwa na muajiri wake. Ni haki ya kila mwanachama kuangalia Taarifa za michango yake ili kuhakiki kama muajiri wake anamchangia pesa, ili kuepuka usumbufu wakati wa kudai mafao.

2. Kukosa uelewa/Elimu juu ya nyaraka zipi na sababu zipi zinazoitajika pindi unapo kwenda kudai mafao, mfano fao la kukosa ajira nyaraka ya kwanza unayo takiwa kuwa nayo ni Barua ya kufukuzwa kazi/ukomo wa mkataba.

3. Office za NSSF/PSSSF kuwa mbali na makazi ya watu... mtu kusafiri umbali mrefu kwenda ofisini kudai mafao.! hii inaweza kutatuliwa kwa mifuko kuongeza office kupatikana kila wilaya au kuanzisha mfumo kwa wanachama kudai mafao yao kwanjia ya mtandao.!

4. Mwanachama kuto hakiki Taarifa zake kwa wakati....>>🙌🏿
 
Back
Top Bottom