sasa wewe nae bhana... binti wa watu umemkuta tayari ana mtoto (kitu ambacho kwako ni disqualification), pili umemkuta kaishia form 3 (kitu ambacho kwako ni disqualification pia), sa ilikuwaje mpaka ukaanza kuishi nae chini ya paa moja (chumba/kitanda kimoja) kama mume na mke for the year now??!!! ushamtafuna weeee, ulimpa ahadi nyingi feki binti akajiachia kwako mazima, umemzeesha kwa migegedo yako... afu now unataka kumdump!! jamani wanaume tufikie hatua tuache kuwanyanyasa hawa ndugu zetu, it's a real 'hurt therapy' kwa anaetendewa.
On the other side of the coin... mkifikisha two years ukiishi nae ivyo kama mke na mume (yaani consecutive two years ndani ya chumba kimoja kama mume na mke) na majirani zetu wakiwa wanajua nyie ni mke na mume, then kisheria utakuwa bound na kitu kinaitwa 'Presumption of Marriage' (dhana ya ndoa).
Presumption of Marriage (dhana ya ndoa) ni ile hali ya watu wawili (ke na me) kudhaniwa au to be considered kwamba wapo kwenye ndoa halali, though in reality hawajawahi kufunga ndoa rasmi. Yaani jamii inayowazunguka inawachukulia kama wanandoa halali, japo bado hamjafunga ndoa rasmi. Viashiria (indicators) vikuu vya 'Dhana ya Ndoa' ni hivi:
(a) Parties (yaani me & ke) wawe wameishi pamoja kama mume & mke, chini ya paa moja (yaani chumba au nyumba moja) kwa muda wa miaka miwili au zaidi. i.e. The parties to cohabit for over two years.
(b) Majirani wawatambue kama mume & mke (ndani ya hiyo miaka miwili). i.e. The parties have acquired the reputation of husband and wife
(c) There was no formal marriage ceremony between the said couples/parties.
Essence kubwa ya hii 'dhana ya ndoa' ni mambo mawili:
MOJA, inatoa unafuu kwa both parties/couples kuachana kirahisi pale wanapoona kuwa hawawezani kuishi kwenye ndoa. Hasa kwa wakristo ambao dini hairuhusu kuachana, yaani ktk ukristo ndoa ni kitu cha milele, haitambui talaka, ukishaingia kwenye ndoa, ndo basi. As such, dhana ya ndoa (presumption of marriage) inatoa loop-hole kwa both parties kuachana kirahisi pale wanaposhindana, bila legal implication. Yaani apa hakuna kuombana talaka, bcoz there's no marriage at all, but it's just a mere presumption of marriage. So mkishindana, then any party yupo kusepa kirahisi! And for the interest of truth, kwa sasa ndoa za aina hii (presumption of marriage) ndo zipo nyingi ktk jamii, wenyewe wanaita 'kupimana kwanza before hujaingia rasmi'. lol
PILI, dhana ya ndoa inalenga kumlinda mwanamke towards maslahi na haki zake. Yaani unapoishi na mwanamke under presumption of marriage na ikatokea kwamba mmechuma mali (jointly acquired properties), utapotaka kumuacha basi izo mali mtagawana pasu regardless kwamba hamkuwahi kufunga ndoa rasmi. Miaka ya nyuma wakati sheria ya ndoa ilipokuwa haija-incorporate presumption of marraige, wanawake wengi waliokuwa wakiishi under cohabitation walikuwa wakidhulumiwa sana haki zao. Mfano mwanaume anamchukua mwanamke, anaishi nae ata miaka 6 na zaidi huku mwanamke huyo akizaa na kuzalisha mali, but mwisho wa siku dume likimchoka linamdump bila kumpa chochote. As such, baadae sheria ya ndoa ndo ikaingiza kipengele icho cha 'presumption of marriage' ili kuwapa legal back-up wanawake wanaoishi ktk muungano huo.
Mkuu Allency, so chukua maamuzi now ili usizidi kumpotezea muda na kumzeesha binti wa watu. Ebu na wewe imagine upate mchumba/mwanamke akuchune haswaa vizuri,
umuhudumie na kumgharamia mambo mengi kwa some years, afu siku anakutamkia kuwa hakutaki na hataki umuoe, utafeel vipi? Si ndo utamfanya kama Ufo Saro? Wakati mwingine tujifunze kuwa wakweli mapema kwa wenzetu.
N:B. I stand to be corrected!