Jinsi tamaa ya utajiri ilivyomponza na akawa Shetani Mkuu

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,626
TAMAA YA UTAJIRI ILIVYONIPONZA

Akiwa ni kijana bado Nico anaamua kuanza maisha mapya na mpenzi wake aliyempenda sana. Mpenzi wake anaitwa Anna. Nico ni kijana anayeishi kijijini mpambanaji anayetamani kuyafikia mafanikio makubwa. Analima,anafuga na lengo lake ni kufanikiwa na kufika mbali na anaishi kwenye maisha ya kimasikini sana. Alimaliza kidato cha nne na akaamua kuishi na kufunga ndoa na mpenzi wake walipomaliza kidato cha nne kijijini kwao kiufupi ni kuwa wawili hawa walioanana utotoni na wameshaishi muda mrefu sana na wamekua vijana wazima na watoto wawili.

Mwaka huo kulitokea ugonjwa wa mazao ulioharibu mazao kiasi kikubwa sana kiasi cha kumfanya Nico kupata hasara kubwa liyompelekea kwenye umasikini zaidi ya mwanzo." Dah hebu una mke wangu Anna mwaka huu tutaishije? Ona mazao yote yamekwisha na ugonjwa shambani na mifugo yenyewe ndo hii haieleweki mambo yanazidi kuwa mabaya sana hata sijui tutaishije mpenzi wangu" anaongea nico kwa uchungu sana
"Usijali mume wangu hayo yote tutayavuka tu tutalima tena mwakani ila usijali kwa kua hatuna chakula ndani nitaenda kuomba kwa shangazi yangu walau unga kidogo utusaidie mlo kwa siku kadhaa"

Maisha yao ya kijijini ni magumu sana.Wanaishi kwenye kijumba cha udongo juu kimeezekwa na mabati machakavu kitanda cha kizamani na godoro na ndani kuna vyombo,kitanda chao,godoro la watoto la kulalia,majembe, na taa ya chemli pamoja na vibatari kadhaa inayoashiria kwamba Wana maisha magumu sana.

Nico anaishi mbali kidogo na kwao kilomita 3 kutoka nyumbani hadi makazi ya Nico. yeye na mkewe Ana na amejenga hicho kijumba cha matope kwenye shamba alilopewa na wazazi na ndo hulitumia kwenye shughuli za kilimo.

"Kesho asubuhi nitaenda kwa shangazi kuomba unga au mahindi alivuna sana alipata gunia 40 na alilima na terekta natumai atanipa unga au mahindi"anaongea Anna huku akiwa kampampasa mume wake Nico kifuani wakiwa wamelala.

"Sawa tu ukajaribu tuone kama utafanikiwa ila shangazi yako kama kavuna najua atakupa tu"...."ndio mume wangu bila shaka".
Baada ya kunong'ona na mkewe wanaamua kulala usiku huku wakiwa na mawazo mazito sana kuhusu Hatma ya maisha yao ya kimasikini wanayoishi.Kulipokucha mke wa Nico alienda hadi kwa shangazi yake ambao kidogo maisha yao yalikua mazuri kiasi maana walikua wakulima wa kisasa na walikua wanatumia zana za kisasa kwenye kilimo na walivuna sana mwaka huo maana walitumia dawa za kisasa na wataalamu katika kupambana na magonjwa yanayoshambulia mimea.

Ana aipofika kwa shangazi yake alimsalimu pamoja na aliowakuta nyumbani.Walianza kuongea mengi sana na alielezea kuhusu jinsi walivyopata hasara ya mazao na hawajui watakula nini.Ndipo shangazi yake akampa pole sana Anna kwa yaliyowatokea.

"Asante sana shangazi kwa kunipa pole ila nina shida kubwa sana yaani hata sijui nitamlilia nan?"..."ipi hiyo niambie mimi nitakusaidia"...shangazi nakuomba tu msaada wako wa hata vibaba viwili vya unga tukale nyumbani au hata ukinipa mahindi sawa tu au hata ukinikopesha mahindi walau kidogo vibaba vichache tu niende nikale na wanangu na mume wangu nyumbani hali ni mbaya sana nimeacha watoto wanalia njaa tu wanaokota hadi maganda ya miwa njiani wanatafuna kwa hali ilivyo"anaongea mke wa Nico yaani Anna kuonyesha kuwa ana shida sana na anataka msaada
Shangazi naye anafikiria kwa dakika kadhaa kisha anamjibu "Yaani mimi nilikulimia wewe?

Umejuaje nilivuna sana kama siyo umbea umbea tu mimi sina unga wa kuwapa wala mahindi na mungu ananisimamia kwamba nawanyima kwa roho nyeupe tu mkalime huko chini mjue uchungu wa jembe biblia inasema asiyefanya kazi na asile kwa kweli nisiwe mnafiki kabisa mahindi ninayo lakini siwapi hata punje huyo baba mkwe wako (babake nico) alivyokua anauza mashamba hovyo hovyo alitaka huyo nico wake aje kulima wapi hata kama mnalima lakini baba yake nico aliuza mashamba mengi sana zamani kisa pombe sasa hivi mnateseka mnaomba omba kama matonya mimi sina mahindi ya kuchezea mwanangu"anaongea shangazi yake Anna kwa harakaharaka utadhani ni cherehani.

"Sawa nimekuelewa shangazi"anajibu mke wa nico kwa upole kabisa."Sasa hata nikiwakopesha mahindi mtanilipa na nini unajua nyie mna mambo ya ajabu sana hebu ukashike jembe huko"anaongea tena shangazi mtu akitumia maneno ya kashfa na masimango.

Mke wa Nico baada ya kuona maneno ya shangazi yake alianza kuondoka huku akianza kufuta machozi. Shangazi yake Ana alivyoona machozi ya Anna yakianza kumtiririka kutokana na maneno aliyomtolea anaamua kuingia ndani anachota unga kilo mbili anampa mke wa nico "haya huu utakusaidia mwanangu Anna nenda na huu"anasema shangazi yake Anna lakini tayari ashamsimanga Ana vya kutosha.

Baada ya kupewa unga Anna anashukuru ili aondoke lakini kabla hajaondoka,shangazi anamwiita "kwanza nimesahau Ana kuna mradi wa kusaidiwa na Uchumi saccos mnapewa mkopo na usimamizi wa kilimo chukua hili jarida lao ni taasisi nzuri humo pia zipo namba zao". Mke wa Nico yaani Ana anakabidhiwa Jarida na analipokea na kuondoka nalo.

Alipofika nyumbani alikuta watoto wanalia njaa sana na nico yupo hana hata mia mfukoni ikabidi akoroge uji kwanza wakanywa na familia yake na watoto wakafurahi kwa ule unga aliyopewa na Shangazi yake."Halafu mume wangu nimepewa hili jarida na shangazi yangu kasema hawa wanakopesha na usimamizi wa mradi unaokopeshwa nao kila kitu" alisema Ana akimkabidhi Nico lile jarida na nico akaanza kulisoma.

Baada ya kulisoma Nico akavutiwa na hiyo saccos ya kukopesha,anamweleza mkewe ana nia ya kukopa huko kwenye hiyo sacoss maana maelezo ya sacoss ni kwamba wanakukopesha pesa unafanya mradi wako na wanakusimamia na kukushauri kwa muda kisha unaendeleza mradi wako lakini unarejesha deni lao kwa riba.Baadaye Ana naye akasoma na kuridhishwa na hilo jambo la kwenda kukopa saccos.

Siku zilisogea na ndipo Nico alipoamua kwenda kwenye ofisi za Uchumi saccos ambazo zipo sehemu inaitwa Bomang'ombe Kilimanjaro.Alienda ofisini ambapo alieleza kuvutiwa na saccos hiyo na akaomba akopeshwe pesa.Baada ya mazungumzo marefu Nico aliomba akopeshwe milioni 5 ili akaendeleze kilimo na dhamana aliamua kuliweka shamba lake la hekari sita ambalo ndo anaishi na kulima huko na ni shamba la kupewa na familia yake.
Ndipo wakakubaliana kwamba Saccos waje wakague na wathibitishe kwamba muhusika yaani Nico ana vigezo vya kukopeshwa.Ndipo Nicco akakubaliana nao na Nico akaondoka kurejea nyumbani kusubiria siku saccoss wanakuja kutazama kujiridhisha.

Nico alipofika nyumbani alimwelezea mkewe kila kitu na kwamba ameaumua kukopa milioni 5." Mhh ila mume wangu si tulikubaliana ukope milioni 2 tu?sasa mbona umesema unakopa milioni 5 sasa?huoni kama itakua ni ngumu kurejesha ukizingatia wana riba kubwa?"...."usijali kwani shida iko wapi weee nataka nifanye kilimo kikubwa hapa cha umwagiliaji mfereji unapita hapa hapa nyumbani tukikopa milioni 5 tukilima nyanya hekari hizi zote 6 nina uhakika tutapata hata milioni 30 na tutalipa deni lao kabisa na tutabakiwa na pesa nyingi na sisi tunajenga mke wangu tukipata milioni 30 zinatutosha kabisa nimeshapiga mahesabu".

Baada ya maneno ya Nico mkewe alijikuta akifurahi sana na kumwambia mumewe "yaani nico ndo maana nakupenda yaani umenifanya niwaze zaidi kachukue mume wangu tuje tulime kwa bidii tupate hela".."sana mke wangu nina ndoto ya kuja kuwa tajiri mkubwa sana".

Kesho yake saccos walikuja na kukagua eneo ambalo nico anaweka dhamana ili apewe mkopo lilikua ni hilo eneo la hekari 6 aliamua kuliweka dhamana lote.Baada ya taratibu zote za uhakiki na kuhakikisha eneo ni kweli ni la Nico,mwishoni wakaandikishana kila kitu na sahihi wakaweka.Ndipo akaambiwa kuwa ataenda ofisini kupewa mkopo huo."Tumeridhika sana na tumeshasaini kila kitu kimeenda sawa Bwana Nicolas na mke Anna kwa sasa mnaweza kuja kuchukua pesa yenu baada ya siku 3 ofisini hongera sana kwa kua mnufaika wetu"

Nico hakuamini maneno yale na aliuliza mara mbili mbili na kuambiwa ni kweli kakidhi vigezo vya mkopo.Alifurahi sana na kurukaruka huku akiwabeba wanae juu na kusema kwamba safari ya mapambano ya kuuaga umasikini yanaenda kuanza.

Ilikua ni furaha kwa Nico na Anna na watoto wao kwani waliona kwamba kwa kua wangali vijana wanaenda kuanza mapambano ya kilimo cha kufa na kupona ili wauondoe umasikini.Siku zilienda huku wakitamani siku ya kwenda kuchukua hizo pesa hatimaye hiyo siku ilifika.

Ilikua ni asubuhi nzuri sana ambapo Nico alijiandaa kwenda mjini kuchukua pesa za mkopo kwani ndo siku ya kukabidhiwa rasmi.Akiwa anajiandaa mke wa Nico aling'ang'ania waende na mumewe yaani amsindikize."Sijui tuende wote jamani nikusindikize tu natamani kweli nikashuhudie"...."hapana mke wangu nitalishugulikia mwenyewe we baki tu na watoto naleta pesa mamaaaa" nico alimjibu mkewe kwa mbwembwe kweli na akimtaka abaki japo Anna aling'ang'ania aende na mumewe lakini Nico alikataa

Safari ya kuelekea mjini nico aliianza na akawasili pale mapema tu na kusubiri utaratibu akiwa na form zake.Mwisho akapata nafasi ya kuhudumiwa ili akabidhiwe pesa zake lakini akaulizwa "Ndio mkopo wako wa milioni 5 upo tayari tupe namba ya account yako ya Bank tukuwekee itakua poa zaidi"alisema mmoja wa wafanyakazi wa ile saccos.

Katika kitu ambacho Nico alielezwa siku ile maafisa wa saccos walipokuja kujiridhisha na eneo lake aliloliweka dhamama ni kuwa aliambiwa ajitahidi awe na account ya bank ili iwe awekewe pesa zake huko kuliko kubeba pesa taslim na mabegi kwani siyo salama. Lakini kutokana na Nico kuwa na furaha iliyozidi siku ile hakukumbuka hata kidogo."Haina haja ya akaunti ya benki mimi najiamini nipewe tu kwa cash nimekuja na mfuko wa kiroba kikubwa tu nitaweka humo.

Kutokana na kuamua hivyo ilibidi tu Saccos wamueleze awe makini maana milioni 5 bado ni kiwango kikubwa sana kubeba kwenye mfuko wa kiroba.Baada ya kusaini tena walielekea benki ambapo ni dakika chache tu kutoka hapo ambapo alikabidhiwa fedha zake milioni 5 cash na akaziweka kwenye kiroba lakini Saccos wakataka wampeleke hadi nyumbani kwa usafiri.Lakini Nico aliona kama utakua ni mlongolongo mrefu au atachelewa sijui aliwaza nini akakataa kupelekwa hadi nyumbani na aliona labda atachelewa yeye ashapata pesa zake anataka azipeleke mwenyewe nyumbani.Basi wakamwacha na pesa zake wakaondoka zao.

Nico akiwa na burungutu la fedha taslimu shilingi milioni 5 kwenye mfuko akiwa anatoka hapo benki wa nje alitokea Dada mmoja mrefu aliyeshuka kwenye gari mpya aina ya Harrier nyeusi mpyaa huyu mwanadada alikua mrembo hatari mrefu na mwenye umbo namba 8,lakini Nico hakubabaishwa na huyo mwanamke maana alikua anawaza tu kuwahi nyumbani na hizo pesa.

Lakini ghafla yule mwanamke aliteleza na kiatu kirefu alichovaa kikamdondosha chini "puuu",Nico alishtuka ghafla na kuwahi kumnyooshea yule dada mkono anyanyuke."Pole sana dada kuwa makini"alisema Nico na kumnyanyua yule mdada.Yule dada alinyanyuka na kumshukuru nico lakini akasema kaumia na hawezi kutembea vizuri."nimeumia kiasi siwezi kutembea vizuri oooh mungu wangu kaka samahani naweza kukuomba kitu?" ......"nambie dada"alisema nico akiwa mkono mmoja kabeba roba lenye milioni 5.

"Unaweza kunishika bega mpaka hapo ndani ya bank pls nitoe tu pesa maana nimeanguka nimeumia naogopa nitateleza kwenye tiles/tailizi za hapo benki plzz"huyu mdada alidai kaanguka kaumia hivyo anaomba nico amshike japo begani hadi hapo ndani benki maana alidai ataanguka.
Nico aliwaza akakubali kumsaidia huyo mwanamke na akamshika bega na kuingia naye benki huku yule mwanamke akitembea kwa kuchechemea.

Walipoingia ndani yule mwanamke alijikongoja mwenyewe hadi kwa wahudumu na akajaza fomu ya kutoa pesa kisha akamuomba nico amshike tena hadi nje kwenye ATM mashine maana zilikua kwa nje. Nico alifanya hivyo hadi akamshika yule mwanamke bega ili asianguke akitembea hadi kwenye Atm mashine na akaingiza card yake na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja. Yule mwanamke baada ya kutoa milioni moja aliondoka na nico akiwa kamshikilia bega kuelekea kwenye gari yake na yule mwanamke ghafla alinyanyua simu na kuanza kupiga na kuongea "asante sana nimetoa milioni moja mshahara wangu wa siku moja kweli hii fursa ni nzuri sana na haiihitaji hata elimu mimi nina elimu ya la saba tu lakini napokea milioni moja kwa siku kweli hii fursa ni nzuri asante sana boss"
Kisha akakata simu.

Maneno ya yule mwanamke kupokea milioni moja kila siku yalimgusa Nico na akajikuta amemuuliza yule mwanamke "unapokeaga milioni moja kwa siku?"..."ndio Kaka milioni moja kama mshahara ila usiongee kwa sauti ndugu yangu watu wakitusikia naweza kuporwa"aliongea yule dada.
Kisha akaendelea kusema "mimi nimeishia la saba tu lakini hii fursa nilijiunga leo hii nina magari na unatajirika majibu ni muda huo huo"..."kivipi jaman?" Nico aliuliza."Naitwa Rosemary wewe je?" Naitwa "Nicolaus au kwa kifupi "nico"...Yule dada alianza kumweleza nico hiyo fursa inavyonufaisha watu na akaenda mbali zaidi akatoa vithibitisho,uhalali,na kila kitu ili nico aweze kuamini.Yule dada alimfanya Nico atamani hiyo fursa na mwisho wakaingia kwenye gari yake na akaanza kumuonyesha Nico majumba na magari anayomiliki kupitia hiyo fursa kwenye laptop ndani ya gari. "namiliki nyumba na magari kwa hii fursa na ukiweka pesa nyingi yaani dau kubwa ndo unapata zaidi" Nico alijikuta akitamani akauliza mfano mtu akiweka milioni 5 itakuwaje "milioni 5 ukiweka ndani ya masaa kadhaa tu utaingiza milioni 25 kwa mpigo maana hii fursa ni mtandao wa kimataifa.

Mawazo ya Nico yalibadilika hapo hapo akitamani hiyo fursa badala ya kwenda nyumbani.Yule dada alimuahidi nico kwamba atamsaidia kujiunga na mwishowe wakawasha gari ili nico akajiunge.Waliondoka bomang'ombe hadi moshi mjini na kutua nje ya jengo la bank moja hivi ambayo huyo dada alidai ndo hapo mtu hujiunga na hiyo fursa na pesa zinaanza kuwa nyingi.

Baada ya kufika pale walipokelewa na dada mmoja aliyejiita customer care wa benk ile na huyo Rosemary alimtambulisha Nico kwa yule customer care "oooh kaja kujiunga na fursa eeh sawa ila tuongee taratibu jamani maana hii fursa ni hela nyingi sana na wakitusikia tutaporwa fedha"aliongea yule mdada na Rosemary huyo aliyekuja na Nico akakubaliana na yule Dada.

Mwishoni kabisa Nico aliambiwa aweke milioni moja akakubali na zile pesa zikaingizwa ndani na akaambiwa asubiri kwa dakika chache tu akiwa na Rosemary pale nje,ndani ya dakika 10 tu akaletewa mabulungutu ya fedha milioni 2 akafurahi sana akasema mambo si ndo hayo?akapanda dau akawa milioni 3 analetewa milioni 4 tena ,akaona isiwe tabu akatoa pesa zote milioni 5 pamoja na hiyo milioni 3 jumla aliyoipata pale jumla ikawa milioni 8 na Huyo rosemary naye akasema naye fursa hiyo isimpite akaweka ile milioni moja aloitoa bank ikawa jumla milioni 9.Nico akaahidiwa asubiri tena dakika kadhaa na ataletewa hapo hapo jumla milioni 20 na rosemary naye akaahidiwa milioni 2 maana aliweka milioni moja.

Ili kusubiri kwa kua ilikua pesa nyingi hiyo waliambiwa waingie ndani wasubirie pesa zao ndipo Nico na rosemary wakaingia ndani kusubiria pesa ziletwe maana zilikua zinachezeshwa kwa chumba cha ndani ya hiyo benki.Ndipo ghafla Rosemary akamwambia nico kuwa kabanwa na haja ndogo anatoka ajisaidie huku akimwachia Nico Mkoba wake."nishikie huu mkoba wangu una hela milioni 2 hizi huku (akafunua akamuonyesha)naenda kujisaidia dakika moja tu na kurudi tuje kuchukua magawio yetu maana hii fursa ni nzuri na ya kitajiri sana"...."sawa fanya haraka"alisema nico na rosemary akatoka haraka haraka hadi alipoegesha gari lake na kuwasha gari kimya kimya na kuondoka.

Nico alisubiria akicheka akijiona ashakua tajiri na akawaza jinsi atakavyopata milioni 20 kwa haraka kichwani aliwaza mengi sana akawa anaona jinsi atakavyokabidhiwa na jinsi atakavyofika nyumbani na kuanza maisha upya mazuri.Na aliwaza mengi sana pia kuhusu Rosemary na kumuona kama mkombozi mwaminifu maana aliacha hadi vitambulisho pale."ana hela sana huyu dada hii fursa imemfanya tajiri sana milioni moja kila siku daaah pesa mingi sana ana hela sana daaah hadi huu mkoba anatembea na milioni mbili sio mchezo na mimi leo naandika historia napokea milioni 20 zangu mie" aliwaza hayo nico akicheka kimoyomoyo kwa furaha.

Alisubiri lisaa lizima rosemary hakurudi.Alijshangaa lile jengo yupo peke yake na kwenda huko kwenye vyumba na kukuta patupu "inamaana mimi na rosemary tumedanganywa?hapana hatuwezi kudanganywa kirahisi hivyo maana hata rose mwenyewe kaweka pesa zake tena ngoja nimwiite labda kabanwa na haja chooni" aliwaza na kuongea mwenyewe akilini hayo nico.
Alitoka nje na kumtafuta Rosemary hakumuona akatizama gari ya rosemary pia haikuwepo akaanza kutafuta nyumba nzima lile jengo likawa kimyaaa hakuna mtu alikwenda hadi njiani kuulizia wapita njia kama wamemuona rosemary wakabaki wakimshangaa sana "hatumjui unamzungia nani hatujamuona yoyote huku njiani tanzania ina warosemary wapo maelfu unamzungumzia yupi umechanganyikiwa?"

Watu walimshangaa na kumjibu nico hivyo.Nico alizidi kuchanganyikiwa akaona hebu achukue zile pesa kwa mkoba wa rosemary alioachiwa ile kufungua hivi mungu wanguuu!!!!!!!!!!hazikua pesa yalikua ni mabulungutu ya karatasi zilizofanana na fedha zilizofungwa kwa "raba band" utadhani ni fedha kweli.Na vile vitambulisho vilikua ni feki,na vya uongo,na pale hapakua benki bali hilo jengo liliwahi kuwa bank zamani lakini miaka 20 iliyopita
Rosemary alikua tapeli wa kimataifa mwenye kujua ulaghai na utapeli wa kila aina.

Nico akawa amekwishatapeliwa milioni 5 ya mkopo mchana kweupe,na hakubakiwa na hata senti tano mfukoni akawa ameshachezewa kekundu. Nico hakuamini alichokiona, alihisi yupo ndotoni, alihisi labda ni utani tu alijikuta akiangua kilio umma ukajaa na kumshangaa na watu wakamwambia "kaka umelizwa matapeli ni wengi mjini.Nico ndipo alipata kichaa zaidi akajikuta anavua hadi suruali na kuanza kutembea uchi njiani huku akipiga mayowe ya msaada maana alikua keshachanganyikiwa.
Jee B
Nico atamwambia nini mkewe?

ITAENDELEA
 
Leo lazima BAYERN afe
479877323.jpg
 
SIMULIZI TAMAA YA UTAJIRI ILIVYONIPONZA
SEHEMU YA 2
ILIPOISHIA
Rosemary alikua tapeli wa kimataifa mwenye kujua ulaghai na utapeli wa kila aina.Nico akawa amekwishatapeliwa milioni 5 ya mkopo mchana kweupe,na hakubakiwa na hata senti tano mfukoni akawa ameshachezewa kekundu.Nico hakuamini alichokiona,alihisi yupo ndotoni,alihisi labda ni utani tu alijikuta akiangua kilio umma ukajaa na kumshangaa na watu wakamwambia "kaka umelizwa matapeli ni wengi mjini.Nico ndipo alipata kichaa zaidi akajikuta anavua hadi suruali na kuanza kutembea uchi njiani huku akipiga mayowe ya msaada maana alikua keshachanganyikiwa.
SONGA NAYO
Watu walimcheka na wengine walimuonea huruma hakuamini kilichotokea mwisho alienda polisi kulalamika katapeliwa lakini haikusaidia chochote alihangaika sana pale Moshi mjini kumtafuta rosemary lakini hakumuona.Ilibidi wasamaria wema wampe nauli Nico ya kurejea nyumbani.Ilikua ishafika Saa tatu siku Nico ndo anarejea nyumbani.Mkewe yaani Anna alikua na wasiwasi sana toka Asubuhi kwamba mumewe mbona hajarejea?Kichwa cha Anna kilikua na maswali mengi mno kiasi cha kumfanya achoke akilini mwake.
"Toka asubuhi hajarejea kakwama wapi?,kaporwa au,au kanyimwa?sasa hata kama hajapewa si arudi mpaka saa hizi jamani huyu mtu?"mke wa Nico aliongea huku akiwa kakaa nje na kiti akimsubiri mumewe na mbalamwezi ukiwaka.Punde si punde Nico aliwasili na mke wake akasimama kumshangaa na ghafla akasema "hee umerudi mume wangu nilikua nakufikiria hapa sasa hivi"(akawasha tochi kumulika mwanga).
Kucheki tu hakua nico yule aliyemzoea mchangamfu,na mwenye tabasamu hata kama yu matatizoni,Nico wa siku hiyo alikua macho ni mekundu,amepooza,kimya,mwenye huzuni.Mke wa Nico alijikuta akiuliza swali moja tata sasa na lililomfanya Nico kudondosha machozi "Pesa ziko wapi?mbona mikono mitupu?"hili swali lilimfanya Nico aanze kulia na kwikwi zikimpanda.Wanasema La mgambo likilia kuna jambo na mwanaume hadi akilia machozi ujuwe jambo limemzidi nguvu na ujue limemfika haswa.
"Hata nisemeje sasa niseme nini,niseme nini mimi,hata sijui nitaongea nini unielewe Anna"nico alimwambia mkewe maneno hayo huku akitiririkwa na machozi.Ilibidi Anna amsogelee Mumewe na kumuuliza kwa sauti ya chini maana alijua kabisa kuna kitu hakipo sawa "Kwani mume wangu imekuaje jamani?"aliuliza kwa sauti ya upole huku mkono akiwa kauweka begani kwa nico.
"Ni hadithi ndefu mke wangu..nilikwenda ofisini asubuhi,nikasaini na nikapelekwa benki kukabidhiwa pesa zangu lakini ametokea mwanamke anaitwa Rosemary amenitapeli zote shilingi milioni 5 nimetapeliwa"...."Wooooooooooh haiwezi ikawa kweli hivi ni kweli unaongea au unatania mume wangu?".."ni kweli nimetapeliwa pesa zote milioni 5"...Nico ilibidi amwelezee mkewe ilivyokuwa na hadi akatapeliwa.Anna alinyanyuka na kujizungusha huku ameweka mikono kichwani "ooooh yesuuuu ruwaaa,kristooo,mungu wangu,Uwiiiiiiiiii ruwa mndumi sitaki kuamini milioni 5 zimekwenda sitaki kuamini ooooh yesuuuu niokoe sitaki kuamini Nico ananiambia nini eeeeh bwana wa majeshi hivi Nico si nilikuambia tunatakiwa tuende wote sasa ninini hichi umetenda?Yaani milioni 5 zimekwenda na maji yesuuuu ruwa ngumu kumeza hii"
Mke wake alichanganyikiwa na akikumbuka kuwa hilo deni linakuja kulipwa kwa njia gani?aliiona hatima yao ikiwa ngumu sana.Alichanganyikiwa hadi akaanza kuongea kichaga "ooooh ruwa mndumi mbon lukeshesokwa kiamba/ooooh mungu wangu tunakuja kunyang'anywa shamba".Anna alichanganyikiwa mnooo na akawa anamuuliza mume wake maswali na akapandwa na hasira na kumuita Nico kwamba ni mzembe wa kupindukia na kafanya ujinga wa hali ya juu.Alikasirika zaidi na akaanza kumtukana mumewe matusi "Kukee mtondo tena isembo mnu kapsa wewe ni mjinga tena mpumbavu kabisa unatapeliwa vipi kijinga namna hiyo?"
Nico hakujibu chochote kwa mke wake alinyanyuka na akaenda kulala.Anna aliongea usiku kucha akimtuhumu mumewe kwamba ni mzembe sana.Zilipita siku kadhaa ndio nico na mkewe wakakubali ukweli kwamba wametapeliwa na kwamba maisha lazima yaendelee na wakubali matokeo,na wafikirie namna watakavyolipa pesa za Saccos maana ule ni mkopo tena una riba.
Habari za Nico kutapeliwa zilizagaa pale mtaani sana na ikawa wanawaza watakaporudisha pesa za watu walipambana hawakufua dafu,wakaanza kuomba hadi misaada nyumba za ibada ili wasaidiwe kulipa hilo deni lakini hawakusaidiwa siku zilisogea na hatimaye mwaka na miezi ikakatika bila marejesho.Saccos ile wakaja wakachukua lile shamba kwa nguvu na kudai ni hekari zote 6 maana ule mkopo riba yake iliongezeka sana badala ya milioni 5 ikawa deni limekaribia milioni 10.
Ndipo siku hiyo Saccos wakaja na notisi kwamba Nico na mkewe na watoto kuanzia kesho wawe wameondoka hapo wanapoishi maana lile eneo linachukuliwa rasmi na saccoss ili liuzwe kufidia deni wanalodaiwa.Hawakuamini walichokiona kwani kesho yake,polisi waliwatoa kwenye hilo eneo kwa nguvu na lile shamba wakanyang'anywa rasmi.Ilikua ni kilio na huzuni kwa Nico,kwani shamba la ndoto zake limekwishachukuliwa na sasa linapigiwa bei liuzwe ili kufidia deni la mkopo.
Nico hakuacha kumlaani Rosemary na aliapa atamlaani mpaka kaburini na popote atakapomuona atamuua.Nico hakua na pa kwenda ilibidi akusanye virago vyake na wanaye na mkewe wakarudi kwa wazazi wake na hapo ilianza kashkash nyingine kwani walijaribu kugoma kumpokea kwa kusema hawamtaki kwani alishapewa haki yake yaani shamba na hivyo hana haki yoyote na wala hawataki kumuona nyumbani."Sitaki kukuona hapa wewe Nico wala mkeo wala wanao usije kwangu nilikupa shamba kama urithi wako na hati kila kitu kumbe umeenda kukopa ukaweka rehani hata hukunambia wala kunishirikisha na mungu ni mwema ukatapeliwa sasa umekuja kwangu kufanya nini?ondoka hapa wewe kabla sijaenda kwa mtendaji wa kijiji ninakushtaki wewe sio mtoto wangu tena usipoondoka nakulaani"hayo yalikua maneno ya baba yake Nico akimwamuru nico aondoke na asikanyage kwake.
Nico ilibidi atii tu yeye na mke wake na virago vyake akaanza kuondoka hawajui hata wataenda wapi ilifika mahali wakachoka wakakaa njiani na vitu vyao ndipo akatokea mama mmoja wa hapo kijijini akawaonea huruma sana akawapa makazi yaani nyumba ya zamani aliyokua analala huyo mama,na ilikua ya matope kabla hajaamia nyumba nyingine ya kisasa."Nimekuita hapa nimeona unazungukazunga tu kijana wangu moyo ukaumia sana ila nimeona ile nyumba ya matope niliyokua naishi zamani unaweza kukaa huko?" Yule mama alimuuliza Nico. "Ndio mama manka naweza mama"
Mama manka aliwapa nico ile nyumba ya miti na matope kama sehemu ya kujisitiri kwa muda tu.Walimshukuru sana yule mama.Maisha yakaendelea kuwa magumu kwa Nico na mkewe kwani hawakuwa na shamba tena lilishauzwa ikawa ni maisha ya kutegemea vibarua tu na kubangaiza.Hali ikazidi kuwa mbaya.
Ndipo siku moja Nico akajiwa na mgeni.Huyo alikua ni rafiki yake aliyesoma naye zamani aliitwa Kennedy.Kennedy alikua tajiri mkubwa sana wa ghafla kiasi cha kila mtu kumshangaa pale kijijini kwani hawakujua ule utajiri kaupataje tena wa ghafla hivyo?Aliingia pale kijijini na gari kali aina ya Range ya milioni 85 kila mtu akaduwaa.Ndipo aliamua kumtembelea rafiki yake nico maana walisoma wote toka shule ya msingi na walikua marafiki kweli kweli
Nico alimshangaa Kennedy rafiki yake kwani miaka 3 iliyopita alikua masikini sana leo hii ni milionea na ana utajiri wa kutisha.Baada ya maongezi ndipo rafiki yake akamshangaa Nico sana "Nico umepauka msela wangu,nico umekonda,nico nione mimi nilivyobadilika,nico umekua mweusi tii kwasababu ya shida wakati wewe haukuaga hivi zamani,nico wewe ni wa kulala nyumba za shida shida hivi wewe ni wa kulala hizi nyumba za mbavu za mbwa?nyumba ina matobomatobo kila mahali sasa si fisi ataingia awale usiku wewe na watoto wako,na hii inaonyesha inavuja sana mvua ikinyesha"hayo yote aliyaongea kenedy rafiki yake Nico.
"Unaongea sana msela wangu kana kwamba unaifurahia hali yangu,nisaidie basi ndugu yako nitoke kwenye huu umasikini maana hata chai umepewa umekataa nisaidie nduguyo"alisema nico.
"Nico siyo nakucheka rafiki yangu,siyo nakubeza,wewe ni zaidi ya ndugu yangu urafiki wetu wa toka utotoni tukienda kuchunga mbuzi pamoja,shule na hata kanisani tukienda kipaimara wote sio hivyo tu hata jando tulienda pamoja naanzaje kukudharau rafiki yangu?"aliongea hayo kennedy.
Waliongea mengi sana na Kenedy pamoja na Anna na kennedy aliahidi kumsaidia Nico kwa hali na mali.Alipomaliza aliwaaga na kuondoka lakini akamuomba nico amsindikize.Kenedy na Nicco walitoka hadi wakaingia kwenye gari yake Kennedy ambapo Kennedy alianza kusema "unajua nicco najua unatamani sana utajiri na uwe kama mimi si ndio eeeh,sasa ndo maana nimekuitia huku ili mkeo ana asisikie unataka kuwa tajiri kama mimi au kunizidi?"..."ndio rafiki yangu nataka utajiri nimepata tabu sana" ..."kweli nicco unataka"...."Kennedy hilo sio la kuniuliza mara nyingi hivyo nataka na nipo tayari kwa lolote ilimradi tu niwe tajiri umasikini ushanichosha nataka niwe kama wewe nipo serious"nicco aliongea kwa hisia sana kuonyesha yupo tayari kwa lolote yeye anataka utajiri tu.Na mawazo ya nicco yalikua yakiwaza na tamaa ya kuwa tajiri kwa njia yoyote ile.
"Sawa nicco utajiri upo wa kutosha nakuuliza tena utayaweza mambo lakini?"...."aaaah kaka mimi nimekwambia nipo tayari kwa lolote hata kwa njia gani mimi nataka niwe tajiri rafiki yangu" ...."haya sawa nimekuelewa sasa sikiliza leo ni jumapili mimi alhamis nakuja kukuchukua tuende huko ili nawe uupate utajiri kama mimi na chukua hizi laki mbili hela kidogo tu iwasaidie saidie hapo nyumbani na shemu wangu lakini usimwambie mkeo kama tumeongea chochote kuhusu utajiri hiyo itabaki siri yetu cha muhimu nakuja kukuchukua hiyo alhamis nikupeleke na wewe ukaupate huo utajiri" Kennedy aliongea huku akimpa Nicco zile laki mbili.
"Asante rafiki yangu kennedy mungu akubariki daah pesa nyingi hii itanisaidia sana ni nyingi sana asante na usiache kuja hiyo alhamis uje unipeleke na mimi nikapate huo utajiri"alisema nicco akihesabu zile pesa alizopewa.Nicco alifurahi sana na kuagana na rafiki yake huyo wa utotoni yaani kenedy na Kennedy naye akawasha gari na kuondoka.
Hakika ilikua siku nzuri kwa nicco kwani usiku huo alinunua chakula kizuri na wakafurahia na familia yake.Siku.zilisonga hatimaye Alhamis ikafika ambapo Kennedy alifika kwa nicco saa 12 asubuhi ndani ya ndinga kali na mpyaaa tayari kwa safari na nico na ilikua ni safari ya Nico ili akapewe utajiri.Nico alimuaga tu mkewe kwamba yeye na Kennedy wanakwenda matembezi na hakumweleza zaidi alimwachia tu pesa ya matumizi akaondoka.Hatimaye safari ya Nico na kennedy ikaanza ili apelekwe akapewe utajiri.
Unajua kilichojiri huko?ni
ITAENDELEA

Ukitaka yote njoo watssap 0737 816 299 nakutumia yoteee
 
SEHEMU YA 3
ILIPOISHIA
Siku zilisonga hatimaye Alhamis ikafika ambapo Kennedy alifika kwa nicco saa 12 asubuhi ndani ya ndinga kali na mpyaaa tayari kwa safari na nico na ilikua ni safari ya Nico ili akapewe utajiri.Nico alimuaga tu mkewe kwamba yeye na Kennedy wanakwenda matembezi na hakumweleza zaidi alimwachia tu pesa ya matumizi akaondoka.Hatimaye safari ya Nico na kennedy ikaanza ili apelekwe akapewe utajiri.
SONGA NAYO
Wakiwa ndani ya gari kwa utulivu mkubwa,wakiendelea kukata mitaa ya jiji la moshi ili waelekee Tanga ndipo Kennedy akaanza kumueleza rafiki yake Nico kuhusu utajiri."Kuna mtaalam mmoja huyo mganga ni kiboko atakusaidia sana anakupa vitu ambavyo vitakufanya utajirike haraka sana".
"Yuko Tanga sehemu gani huyo?mimi hata uwe wa aina gani muhimu utajiri tu aisee nimeshachoka na huu umasikini"..."Ni Tangani wilaya ya Pangani tunaenda na huyo mtaalam ni kiboko haswa na sio wa kubabaisha kama wengine".Waliendelea na safari hadi wakafika mkoani Tanga.
Safari yao haikuishia hapo ilikwenda hadi huko Pangani na wakafika kwa huyo mganga."Mzee Salumu majini kama ajulikanavyo alikua ni mganga mashuhuri sana huko Pangani na aliogopwa sana hata na waganga wenzake na kila mtu kwani akiamua kukutoa uhai uondoke duniani haichukui hata nusu saa unakua tayari ushafika mawinguni kuwalaki malaika.Mganga alimpokea Kennedy kwa kumlaki vizuri sana maana kennedy alifahamika pale kwa yule mganga.
Baada ya maongezi mawili matatu Kennedy alimtambulisha Nico kwa mganga."Huyu ni rafiki yangu anaitwa Nicco na nimekuja naye hapa ana matatizo mengi sana kikubwa kwake anahitaji utajiri najua mzee wangu umenielewa"."hilo halina shaka oooh bwana nico karibu sana jisikie upo nyumbani"...."asante mzee wangu nimekaribia".
Baada ya kutambulishwa waliandaliwa maji wakaoga na kupewa mahali wakampumzika.Usiku kulipowadia nico na Kennedy walikua wakiongea mawili matatu kuhusu masuala ya utajiri na uchawi na nicco alikua na wasiwasi juu ya kwamba jee ataupata utajiri kweli? "Kennedy best yangu nawaza sana kana kwamba huyu mzee anaweza akanisaidia maana nakosa imani kabisa hii ni mara yangu ya kwanza kuja kwa mganga toka nizaliwe" ...."jamaa angu nakuambia huyu mzee ni kiboko salumu majini anaogopwa Pangani nzima kwake hakuna anayefurukuta alaaa unadhani ni wa mchezo mchezo?jamaa anaijua hii fani ya uganga haswa"aliongea Kennedy akimtoa wasiwasi nicco.Muda ulisogea na wakaletewa chakula wakala na kisha wakalala usingizi mzito kutokana na uchovu wa safari yao ya kutoka Kilimanjaro hadi Tanga.
Asubuhi kulipokucha Nico alishuhudia msusuru wa watu wakija kutibiwa hapo kwa huyo mganga walikua ni watu wakubwa,wasanii,watu mashuhuri,wanasiasa,na hata viongozi wa dini waliokua wakija pale kwa mambo tofauti tofauti.
Nico yeye aliambiwa kwamba atakua na safari na mganga ya jioni.Basi masaa yalienda watu wakiendelea kumiminika pale kwa mganga hadi jioni mganga alikua ashamaliza kazi yake ya siku hiyo ya kutibia watu wake yaani kuwaagua.
Usiku huo mida ya saa moja ndipo mganga akamwiita Nico na Kennedy akiwaarifu kwamba muda wa kuelekea huko baharini ndo umewadia.Hatimaye wakaanza kuondoka Nico,Kennedy ,mganga na msaidizi mmoja hadi huko ambapo kulikua na msitu uliokua kando ya bahari.Walipofika huko walikuta kichochoro kirefu sana na wakaingia ndani ya msitu huo.Ndipo mganga akamuuliza Nicco kwa mara nyingine tena "unataka utajiri kweli?"..."ndio mzee nautaka"..."sawa ufate masharti nitakayokupa na usiogope chochote"...Nicco alitikisa kichwa kukubaliana na mganga.
Mganga alitoa ngoma ndogo na kuipiga kisha akapuliza kitu kama filimbi na kuongea maneno kadhaa ya kichawi na ghafla pale msituni pakawaka taa pakawa kama mchana.Nico alistaajabu sana ile hali.Mganga alijitambulisha pale akiongea na majini kwamba kaja pale kwa kazi maalum ya kutaka huyo nicco apate utajiri.
Ghafla sauti kubwa ya kutisha ilitikia kwa nguvu "naam tunamkaribisha kwenye mji wetu"kisha sauti ikanyamaza.Ghafla wakiwa pale ikatokea njia inayoelekea kwenye majumba ya zamani yaani yale majengo yaliyojengwa na waarab miaka hiyo.Lilionekana jengo la aina hiyo ndipo mganga na yule msaidizi wake wakaanza kuimba kama dakika 5 hivi kisha wakanyamaza
Kisha mganga akamwambia Nico kwamba anataka afate ile njia aingie kwenye lile jengo na akatakiwa kuvua nguo zake zote.Nicco alivua nguo zake zote na akakabidhiwa kibuyu na yai la bundi aingie nayo na alikua uchi wa mnyama na alitakiwa aende yeye mwenyewe kwani wao watamsubiri pale.
Nicco alianza kutetemeka kwa hofu,kwa uoga sana na akawa kama anasita kwenda.Mganga ndipo akamuuliza tena kwamba kama anataka cha mvunguni sharti ainame ikawa na maana
kwamba kama anataka utajiri shutu afuate hizo kanuni na afate anachoambiwa.Hayo maneno yalimfanya nicco kutafakari upya na mwishoni akakubali kwenda.
Ndipo akaanza safari ya kuelekea kwenye lile jengo na alikua akitetemeka sana akiwaza mengi mno kwenye akili yake kwamba itakuaje na jee likimpata la kumpata?Alikumbuka aliyoyapitia,maisha ya shida,jinsi alivyoenda kukopa na kutapeliwa milioni tano taslimu na kibaya zaidi akaja kuchukuliwa shamba heka sita na saccos na kuuzwa,akakumbuka watoto wake,na mke wake hali yao ya umasikini,na jinsi alivyofukuzwa kwao kama mbwa na kupewa hifadhi na mama manka alijkuta akichuruzikwa na machozi huku akiwa anatembea kulifata lile jengo.
Alimuomba mungu amsamehe sana kwa hiyo hatua hana jinsi tena ya kufanya."Nisamehe mungu wangu sina jinsi" alisema huku akiendelea na safari ile ya kulifata lile jengo akaingie ndani.Alijikuta akisema liwalo na liwe kama ni kufa afe tu na yupo tayari kwa lolote alipokumbuka madhila aliyopitia.
Alitembea na hatimaye akalifikia hilo jengo alifika kwenye mlango wa hilo jengo kama alivyoelekezwa na mganga ni kwamba,akifika tu mlangoni atavunja lile yai la bundi kwa kulipiga chini kwa nguvu kama mtu anavyopiga kitenesi.Alipofika pale alichukua lile yai la bundi na akalipiga chini kwa nguvu na likavunjika na ghafla mlango ukafunguka.
Mlango ulifunguka ambapo aliingia humo ndani na kushangaa sana kwani alikuta huko ndani ni kama hekalu kubwa la kisasa ambalo halina mfano wake,kulipambwa na kila aina ya vito vya thamani na paliwakwa kweli kweli kiasi cha nico kushindwa hata kulifananisha na sehemu yoyote ile duniani kwani palikua pakipekee sana pakiwaka dhahabu,mataa na paking'aa sana.
Alivyoingia ghafla alisikia sauti ikimwiita "wewe njoo huku hiki chumba" ilikua ni sauti ya kiungwana sana ikimwiita aingie katika chumba kimoja kule.Nicco alifuata korido za lile jambo na kukifata kile chumba,na alipofika mlangoni ghafla mlango wa kile chumba ulijifungua wenyewe na Nico akaingia ndani.
Nicco alipoingia ndani ndipo alipata mshangao wa kutisha,alikuta majini ya kutisha sana yaliyokua na maumbo ya kutisha,watu sio watu,mizimu sio mizimu,wanyama sio wanyama.Yalikua majini ya kutisha,yalikua na sura za kutisha na majini wale walikua na mabakuli ya damu wakinywa."Karibu" ilikua ni sauti ya mzee mmoja wa kijini mwenye jicho moja tu linalowaka mithili ya tochi,lilikua jicho kubwa sana kama la ng'ombe na alitisha sana,manyoya ya kutisha na makucha marefu pamoja na ndevu ndefu sana zilizofunika hadi kifua na huyu kiumbe alikua ni mwili mkubwa sana na alitisha sana na sauti yake iliogopesha na walikua wanamkaribisha nico damu waliyokua wakinywa pale.
ITAENDELEA
 
SIMULIZI TAMAA YA UTAJIRI ILIVYONIPONZA
SEHEMU YA 4

Walimwambia Nicco kwamba ikiwa anataka utajiri ni lazima anywe ile damu iliyokua mbichi kabisa "Kama unataka utajiri ufate masharti yetu sisi na usiogope utatumiliki sisi lazima uanze kwa kunywa hii damu kwanza"aliongea mmoja wa yule jini mkuu na kumfanya nicco atetemeke hovyo na akajikuta ameanza kukataa.
Alitoka mbio sana mpaka mlangoni akisema "hapana hapana kama ni hivi sitaki sitaki" kufika mlangoni akakuta pale alipoingilia hakuna mlango tena akabaki ameshangaa sana akaanza kufata korido ndefu za lile jengo kubwa akaanza kukimbia hovyo hovyo tu akipiga kelele kwamba asaidie maana ilikua kama vile kafungiwa mule ndani.
Alianza kupiga kelele kwa nguvu "nitoeni jamaniiii nitoeni sitaki tena utajiri nasema sitaki naombeni msaada mnitoeeee" badala ya kusaidiwa alisikia sauti za kutisha za majini yakicheka kwa nguvu sana.Alianza kupiga kelele sana mwishowe aliona kitu kinamnyanyua juu utadhani anapaa ghafla akaona amekua kama kipofu giza na moshi mtupu kufumba na kufumbua akajikuta amelala chini kwenye ule msitu mbele ya mganga na rafiki yake Kennedy.Ndipo Nicco akazinduka kidogo akimbie maana alidhani bado yu kule."nimefikaje fikaje hapa?"..."yamekurudisha umeharibu kila kitu aisee huwezi maana hii ni fursa kubwa sana maana ungepata utajiri ungekubali tu unywe ile damu ungeipokea wasingekuruhusu unywe kweli ilikua ni kama mtihani wa kukupima ili tu ukafanikiwe turudi nyumbani tu"alisema mganga na kuanza safari ya kurudi kwa mganga kutokea kule msituni.
Njiani kennedy na mganga walikua wanamcheka Nicco sana na kumuona ni muoga sana."wewe jamaa ni muoga sana sasa unafikiri ningekua muoga ningekua na utajiri huu acha uoga tena masharti yenyewe mepesiii sana unakwama wapi nicco?" Alisema Kennedy."Wee kule panatisha aisee maishani sijapata ona kiumbe wa ajabu vile"alisema Nicco huku akijifuta jasho maana lilikua limkimchurizika na kulowa kweli kweli.
Walipofika walipumzika kidogo maana ilikua ni usiku na wakala na kuoga ila Nicco alitakiwa kuna dawa alitakiwa achanjwe na ya kunywa kisha atalala na kuna maagizo atapewa ndotoni.
Alichanjwa dawa zile kisha akapakwa nyingine usoni,mikononi,kwenye kitovu,mgongoni na miguuni na akapewa maagizo kwamba atalala na ataota ndoto kisha ndoto hiyo ndo itakua na maagizo kamili kuhusu utajiri wake.
Kweli alilala na usiku ulipowadia aliota ndoto yupo kwenye mji wa kisasa uliojengwa kisawasawa na katika ndoto hiyo nicco alikaribishwa katika sherehe moja na kukuta watu wakila nyama choma na kisha alivyofika tu akaanza kupokelewa kwa shangwe na kuelezwa kwamba ni yeye tu alikua anasubiriwa ili aweze kuanza kula nyama choma kisha wengine watafuta.Nicco alipewa nyama choma kisha akaanza kula na kushangiliwa sana na baada ya kula wengine wakafuta wakianza kula ile nyama na alikabidhiwa zawadi nyingi sana ilikua nyumba ya kifahari,magari,na vito vya thamani kubwa sana.Aliposhtuka kwenye ile ndoto alikaa na kutafakari sana cha ajabu alivyocheua,alicheua harufu ya nyama kabisa ilhali toka ameenda pale kwa yule mganga hakuwahi kula nyama.
Kulipokucha alimweleza mganga jinsi alivyoota na mganga akamwambia hii ndoto inaendana na kazi ya leo usiku ambayo anapaswa akaifanye.Ilipofika tena usiku wa siku hiyo walielekea tena kule msituni akiwa kaambatana na Kennedy,mganga na vijana wengine watatu.Njiani mganga alimwambia Nicco kwamba safari hii anapaswa kuacha uoga na kwamba ana nyota nzuri ya msimu wa heri kwa majini na utajiri na kwamba aitumie vizuri nafasi ya leo kwani akipoteza nafasi ya leo kuipata tena ni muhali kwasababu majini yanatoa ofa ya heri kwa nyota za utajiri kwa masharti nafuu kwa msimu maalum na nyota maalum.
Kingine mganga alimuonya sana Nicco kwamba asichezee fursa hiyo kwani anammalizia mayai yake ya bundi."unanimalizia mayai yangu ya bundi unapaswa kuwa makini sana leo usiende tena ukavunja masharti sawa?"...."sawa mzee sitavunja na nitajikaza sitoogopa tena"..."vizuri kijana wangu".
Kama kawaida, Mganga alitoa ngoma ndogo na kuipiga kisha akapuliza kitu kama filimbi na kuongea maneno kadhaa ya kichawi na ghafla pale msituni pakawaka taa pakawa kama mchana.Mganga alijitambulisha tena pale akiongea na majini kwamba kaja pale kwa kazi maalum ya kutaka huyo nicco apate utajiri.
Ghafla sauti kubwa ya kutisha ilitikia kwa nguvu "naam tunamkaribisha kwenye mji wetu"kisha sauti ikanyamaza.Ghafla wakiwa pale ikatokea njia inayoelekea kwenye majumba ya zamani yaani yale majengo yaliyojengwa na waarab miaka hiyo.Lilionekana jengo la aina hiyo ndipo mganga na yule msaidizi wake wakaanza kuimba kama dakika 5 hivi kisha wakanyamaza.Ndipo Nico akaamriwa afuate njia kuelekea kwenye lile jengo.
Mkononi alikua na kibuyu na yai la bundi.Na alivyofika mlangoni tena alivunja lile yai la bundi kwa kulipiga chini ghafla ukafunguka na akaingia mule.Cha kustaajabisha alivyoingia kule alikuta sio kama alivyopaona jana.Ilikua ni kama huku duniani na palikua na bustani kubwa iliyojaa majiko yaliyojaa majiko yakichoma nyama tofauti na kulikua na viumbe vya kutisha.Alipofika tu alishangiliwa sana na alikuta kuna kundi kubwa la wachawi wa duniani na watu wengine wenye sura ya kutisha kukiwa na mchanganyiko wa viumbe vya ajabu,majini na binadamu.
Alipofika alimkuta mkuu wa ile sehemu akiwa yeye ndo jini mkuu wa eneo lile ambalo alimuamuru kwamba anatakiwa atafune maiti ya mtoto mchanga."unapaswa utafune maiti ya mtoto mchanga ndio tutasikiliza ombi lako"ilikua ni sauti ya yule jini mkuu.Kitendo hicho kilimpa Nico hofu sana lakini akiwa anawaza alitokea mwanamke nzuri sana aliyeumbika sana lakini alikua na kwato na maziwa yake yaani matiti yalifika hadi mapajani.Alianza kumsemesha nicco kwa sauti ya chini "kama unataka usikilizwe chukua maiti ya mtoto pale umchome hapo ule hutaki utajiri?hutaki kuwa mtu mwenye pesa?"
Maneno ya yule mwanamke yalimpa Nicco ujasiri wa ajabu sana alijikuta akisogea na kusogelea maiti ya mmoja wa watoto wa wachana wanaotolewa duniani huku kwa makafara na kumchomeka kwenye lichuma kama mshikaki na kuanza kumchoma kwenye moto.Hayo aliyafanya kisha baada ya hapo alimchoma vizuri na kuwa tayari kuliwa.Alitakiwa ale ile nyama yaani nyama ya mwili wa mtoto mchanga.Nico alisua sua sana na alianza kulazimishwa na jini mkuu ale la sivyo atatiwa adabu
"Nyie binadam mna viburi sana unataka kula au nikutie adabu"aliongea jini mkuu huku macho yake yakianza kutoa miale ya moto kwa hasira.Nico kuona hivyo alianza kutafuna ile maiti na alianza kula ile nyama akashangiliwa sana na umati wa viumbe waliyokuwepo pale.
Baada ya kula hadi kushiba,ndipo jini mkuu akamuuliza nico aombe chochote anachokitaka."nataka utajiri"alisema nico huku akitizama juu kwenye kile kitu cha jini mkuu."utakua tajiri sana haya nenda" Nicco aligeuka na kuanza kuondoka lakini ghafla alijiona kama anapaishwa kwenye giza kuu akiwa anahisi ubaridi nzuri sana na ghafla alijikuta kwenye uchochoro akiwaendea mganga na rafiki yake Kennedy."Leo umeweza hongera kijana"alisema mganga na kuanza kumkumbatia nico.
"Kweli naenda kuwa tajiri??" Aliuliza nicco huku akitabasamu."Ndio bila shaka"...."natamani sana naiwe hivyo nakuahidi mtaalam nikiwa tajiri nitakupa pesa nyingi sana"alisema Nico akiwa na furaha sana.Waliondoka wakicheka hadi kwa mganga ambapo mganga alisema naye usiku atasafiri kwenda kwenye ulimwengu wa majini na kuna maagizo atampa asubuhi.
Alivyofika waliendelea na mambo mengine kisha wakalala.Kulipokucha asubuhi ndipo mganga akamwiita Nico na kuanza kumpa maagizo."Jana nilisafiri hadi kwenye ulimwengu wa majini na nikapata nafasi ya kuonana na jini mkuu"Mganga aliendelea kumweleza nico kuwa ni kwamba amepewa pete ya kijini ambayo ataivaa muda wote bila kuivua,na ni kwamba hatakiwi kukutana na mke wake kimwili kwa muda wa miezi 6 au mwanamke yoyote yule,pia ahakikishe utajiri ukianza tu achinje ng'ombe nzima na kuwaalika watu wote wale chakula na awe anagawa tu pesa kwa watu."Una bahati sana Nicco huu utajiri wako unaokujia ni wa kufurahisha sana maana hauna masharti makali sana yaani umependelewa sana na majini wewe lakini zingatia hayo mambo niliyokuambia".."sawa mtaalam mimi nangoja kwa hamu hizo pesa tu na utajiri hahahaha" nico aliongea kwa mbwembwe sana.
Walimaliza kazi na nico akakabidhiwa vitu kadhaa na alitakiwa kutomuonyesha mtu yoyote na rafiki yake yaani kennedy alimlipia nico pesa iliyotakiwa mganga alipwe kama ujira wa kazi na wakaanza safari ya kurudi Kilimanjaro kutoka huko Pangani mkoani Tanga.
Njiani waliongea mengi sana na Kennedy alizidi kumsisitizia nico kwamba afuate masharti aliyopewa na ahakikishe kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa.Na nicco alipanga akifika tu akaanze kufanya kazi mgodini. Safari ya kurudi iliendelea na hadi wakafika Kilimanjaro japo ilikua ishafika usiku sana.Alivyofika tu Kennedy alimfikisha nico hadi nyumbani na kisha akaaga na kuondoka zake.
Nicco alipofika alipokelewa na mke wake lakini mkewe alikua akimuuliza maswali mengi sana "wewe si uliniaga unaenda matembezi vipi tena siku kadhaa ulikua wapi?"..."nilikua nimeenda kutafuta pesa ulitaka nikae tu hapa nyumbani?"...."kutafuta pesa si ungesema tangu mwanzo mbona umenitia kwenye wasiwasi mno mume wangu nikiwaza ulikwenda wapi,au una mwanamke mwingine?"...."ushaanza mke wangu Anna niwe na mke mwengine wakati nakupenda wewe tu?".Waliendelea kuongea pale lakini Nico hakutaka mkewe ajue chochote kuhusu kwamba jamaa alienda kwa mganga.
Aliingia ndani na kulala na mkewe akamfuata kwamba anamuhitaji kimapenzi mumewe usiku huo kutokana na masharti nico alikataa akamwambia mkewe kwamba amechoka hivyo amuache apumzike.
Alilala hadi asubuhi na alipoamka alioga kisha akamuaga mkewe anaondoka."mbona ghafla mume wangu sikuelewi jana tu usiku umewasili sasahivi tena unaondoka?"...."samahani mke wangu Anna kipenzi kwasasa siwezi kukuongelesha ingia ndani hapo nimeacha ujumbe usome kisha nakusubiri hapa.
Anna aliingia ndani ili auchukue ujumbe ausome na alivyoingia tu ndani Nico aliondoka mbio mbio akikimbia.Ule ujumbe alimwandikia mkewe "samahani mke wangu sina jinsi naenda Mererani kutafuta pesa mgodini nisamehe sana nitarudi hivi karibuni nakupenda sana na nawapenda wanetu pia endelea kuwalea watoto wetu wakiniulizia wadanganye tu kuwa sijaenda mbali" ulikua ujumbe wa Nico kwa mkewe huku kukiwa na bahasha ya laki moja aliomwachia mkewe ya matumizi .Anna alitoka ili kumuuliza mumewe Kwanini afanye vile ile kutoka tu akukuta mumewe ashasepa.Anna alianza kutiririkwa na machozi kwani aliliita jina la mumewe kwa sauti kumbe mtu ashaondoka Anna alilia sana na alimpenda sana Nico wake aliwaza akaona atakua mpweke sana.
Nico aliondoka hadi Mererani Arusha ambapo ndipo alipanga akatafute pesa.Alipofika huko ndo mambo yaligeuka maajabu matupu kwani....
ITAENDELEA
 
nipekidogo Heavy Metal Lengutee boy lanugo nyakisese ukhty khadija ndulle burdizzo Charlie one mbhaja HELA Its_Penny morgan freeman big jambo mireille Kaijadan mtzmweusi mbududa mr chakubanga njoo kwetu bweke saemonity chaku92 Rich Pol Laki Si Pesa Mjamaa86 kaswiza90 guasa Amboni aggyd REALNEGRONEVABROKE Nuhu39 Sir8 Maja_AK Vangigula nipo2 kudraty Heri Mr Mtete nicksonmoses Waseme kawoli Drizzle mlyn red apple jonoma capitalpool nez-o Edwina Edwin choza choza Baba Swalehe mjanja @M1 Kapumpuli luqman luqman Barca JMA The Super notoriousic @Mr no Mbwiga CORONA ERASER Jeong do jeon Nyaubikra Msichana wa jana Abuu Hafswa The Planner Momole lexas Mr.7 mhuri25 jamiiyakiarabu King Sae Abdzy jr IFRS Mbuyimayi bishororo Naviboy Ernestm Ms Euna gucci GANG magnifico maji ya gundu olonyor engai noel96 Ivan ndaro Jailos Mrisho Sindu mrdalu Petro matei Tusker @Bariiiidi Kali kichele Shomy . I Tua Ngoma Son.j Bendanda Teenager Koala 255Gene ram @Elevat KAPELA yusuf57 santiago01 Habari Zenu historian periodic table Sakalai EnnoMX Ihayabuyaga PTER Shupavu TASLIMA Yorname chacha nyangaka martinezmarty ris MeruA clecla binti mapozi jogoo wa maajabu@ song 16 john tongo kuchikubwa K-wire Mwaronk DreezyD98 Jasmoni Tegga JUAN MANUEL Musundi swahib sinjo Akthoo Nyilamu HaMachiach Jagarld AlmasMAlmas sipii rediicky Sent Kb Behaviourist Mhariri Breki ya Kenge zandrano kingzeddy Zero IQ notorious @boy87 mtafiti com dluv hersiwahaab ikhatibu Chancellor moneytalk Ukitu Panel Emilia22 Attacker Mr Slim Mirlz B Matthew rumplelstiltskin Rumi96 Magema Jr Jerry94 Mjep mezanane Dampa Shaiba CAPO DELGADO Mjamaa1 sumbwi makedonia coverland mbukoi songa Heri Bexb dvj @nasmiletz muxar Blackninja Glucky maubusu @YonDu @Udonta kaburungu Snipes CHOKAMBOVU mkulima2 Dr. Wansegamila SOMK M-mbabe miss gisenyi chaku jr chakutu Abuu bin umar @seydun Franky Samuel Kitoabu 0ozg Tz Madame S benybeny Gamaha Asam Santos06 Balloz Wa Igima Chantaburi Sky Eclat Typical Next Man
 
SIMULIZI TAMAA YA UTAJIRI ILIVYONIPONZA
SEHEMU YA 5
ILIPOISHIA
Anna aliingia ndani ili auchukue ujumbe ausome na alivyoingia tu ndani Nico aliondoka mbio mbio akikimbia.Ule ujumbe alimwandikia mkewe "samahani mke wangu sina jinsi naenda Mererani kutafuta pesa mgodini nisamehe sana nitarudi hivi karibuni nakupenda sana na nawapenda wanetu pia endelea kuwalea watoto wetu wakiniulizia wadanganye tu kuwa sijaenda mbali" ulikua ujumbe wa Nico kwa mkewe huku kukiwa na bahasha ya laki moja aliomwachia mkewe ya matumizi .Anna alitoka ili kumuuliza mumewe Kwanini afanye vile ile kutoka tu akukuta mumewe ashasepa.Anna alianza kutiririkwa na machozi kwani aliliita jina la mumewe kwa sauti kumbe mtu ashaondoka Anna alilia sana na alimpenda sana Nico wake aliwaza akaona atakua mpweke sana.
Nico aliondoka hadi Mererani Arusha ambapo ndipo alipanga akatafute pesa.Alipofika huko ndo mambo yaligeuka maajabu matupu kwani....
SONGA NAYO:-
Mambo yaligeuka maajabu matupu kwani alipofika pale Mererani alipata kazi mgodini siku hiyo hiyo kitu ambacho sio cha kawaida.Kwani alipofika pale tu kuna dawa alipewa na mganga kwamba atajipaka mikononi na kwenye paji la uso huku akiweka manuizi kwamba anataka afanikiwe katika hilo jambo.
Na ndipo alipopata kazi kwenye mgodi na kuanza kazi mara moja ambapo ndani ya siku tatu tu wakati anachimba ndani ya mgodi alipata kipande kimoja kikubwa sana cha Tanzanite baada ya kupasua mwamba mkubwa sana na kutumia mbinu za hali ya juu kuficha ile Tanzanite kwani lakini alijua atakamatwa tu maana kule mgodini kuna ufatiliaji wa hali ya juu na kupekuliwa kila mchimba madini anayekuwepo kule.Yale madini yalimshangaza na hakuna ambaye angepata madini katika upande wa mwamba huo kwani ndani ya huo mgodi wengi hutambua huo mwamba kama usio na madini kwahiyo hakufatiliwa sana hivyo alichimba ndani ya upande huo na akapata kipande hicho kimoja.
Aliamua kukificha ndani ya mfuko wa suruali na alijua atakamatwa tu maana ukitoka ndani ya mgodi mule shimoni ukipanda juu kukaguliwa ni lazima.Alichukua dawa fulani ya unga akanuiza kwamba asikamatwe na alipopanda juu ili atoke mgodini ndipo wakaanza kukaguliwa ila jambo la ajabu yeye ilipofika zamu ya kukaguliwa alipita pale kimaajabu yaani alikwepa na hata mashine,na wakaguzi hawakushtuka chochote kile.Na hiyo yote ilikua ni nguvu ya uchawi.
Ndipo alipoondoka kimya kimya na akatoroka pale mgodini na kwenda Arusha mjini kuna maduka fulani ya wahindi ambao hununua madini na cha kwanza alifanya uchunguzi kwanza na akafungua akaunti ya benki na alienda kuuza kwa wale wahindi waliokua wananunua madini.
Kufika katika mojawapo ya hilo duka,aliweza kuuza kile kipande cha Tanzanite chenye uzito wa Gram 450 kwa jumla ya shilingi milioni 45.Hii ilikua pesa nyingi sana kwa Nicco.Nico hakutaka kufanya makosa tena kama aliyoyafanya wakati ule,alihakikisha zile pesa zimeingizwa bank kwenye account yake.
Nico alihisi kuchanganyikiwa akiwa haamini alichokiona.Alijikuta akitoa chozi na kulia sana akifurahia ile hali kwani hakujua kama ipo siku atakuja kushika mkwanja mrefu namna ile kwake ilikua kama ndoto vile.
Hakutarajia kama ingetokea ile hali baada ya kulia sana,alianza kucheka sana na kushangilia mno kiasi kwamba ungekutana naye ungedhani labda karukwa na akili.Katika zile pesa alitoa milioni mbili cash akabeba kwa matumizi mengine pia akaingia kilombero sokoni akanunua vitu vingi sana vyakula,na matunda akajaza mifuko na akapanda gari za kuelekea moshi maana hamu na furaha aliyozidi nayo haikua ya kifani na alitaka akamweleze mkewe kuhusu hayo mafanikio.
Njiani alihisi kama hiyo coaster haiendi vile maana alihisi hafiki kwani alitamani hata apae akamweleze mkewe ukweli kuhusu hizo pesa alizopata.Alivyofika Moshi alielekea moja kwa moja nyumbani ambapo alifika mida ya saa 10 jioni ambapo Anna akiwa amejikunyata hapo tu nje na wanae akiwa katika hali ya huzuni,alishangazwa kuona Tax ikiingia nyumbani kwake.
Aalaaaaa!!!mke wa Nicco alijiuliza maswali kibao kichwani mwake kwamba hiyo gari imetoka wapi na mbona imekuja hadi wanapokaa?Kufumba na kufumbua sio mwingine aliyeshuka alikua ni mumewe kipenzi Nicco.Nico alishuka na kutoa mizigo yote ndani ya Tax na kumlipa yule dereva Tax na kuondoka.
"Mume wangu umerudiiiii" alisema Anna kwa furaha sana."Ndio mke wanguuuu!!!!!!"Nico aliongea kwa furaha sana na kumnyanyua mkewe juu kwa juu na kumuingiza ndani."Nina habari njema sana tena sana mke wangu umasikini ni ndotoo sasa"."Eeeeh una maana gani mume wangu ni ndoto kivipi?"
"Mke wangu nilienda mgodini nikapata madini,kipande kimoja cha Tanzanite nimeuza nimepata milioni 45".....Anna zile habari hakuziamini kabisa alibaki akiduwaa akisema "eeeeeh" Hakuamini kabisa ndipo Nicco akatoa bunda la shilingi milioni moja na nusu minoti tu Anna ilikua kidogo azimie "Yesuuu ruwaa hela zote hizo uwiiii mume wangu jamani hivi ni kweli au unanitania tu?" ...."mke wangu zote hizo ni zetu na ngoja uone",Nico alitoa Risiti na pay in Slip za benk zinazoonyesha kiasi cha pesa kilichopo benki sio hivyo tu alimwonyesha mkewe kard ya bank akimwambia "umeamini sasa umasikini kwetu ni ndoto".Alimweleza mkewe mambo yalivyoenda hadi akapata hicho kipande kikubwa cha Tanzanite.
Anna aliruka ruka kwa furaha sana akimshukuru mungu sana na kumuimbia na kumtukuza ila hakujua mume wake nyuma ya pazia ni jinsi gani alishapita kwa mganga hadi kutafuna maiti za watoto wachanga ili tu apate utajiri.Nico aliileta furaha ambayo ilipotea ndani ya familia yake kwa muda mrefu kwasababu ya umasikini kwani vile vyakula na matunda alivyonunua viliifanya ile familia ifurahie sana siku hiyo.
Nicco alimwagiza mkewe atafute nyumba ya kupangisha pale kijijini na watoke kwenye ile nyumba waliopewa hifadhi na mama manka.Alimwaachia pesa za kodi kwa miezi 8,na pia alimpa pesa za kununua vitanda viwili na magodoro mawili kwani siku zote walikua hawana hata kitanda kizuri walikua na kitanda kibovu vile vya zamani machumachuma aka banko huku watoto wao wakilala chini
Baada ya maelekezo ilipotimia saa mbili usiku nicco alijiandaa akamwambia mkewe kwamba anaondoka arudi kazini.Mke wake alishangaa sana kwasababu Nico alifika tu nyumbani siku hiyo hiyo tena saa kumi jioni, na kwanini aondoke wakati huo huo wakati familia ilimmiss kwa siku kadhaa?."unaondoka unakwenda wapi sasa mume wangu?si uwende kesho jamani?"...."samahani mke wangu sina budi inanibidi niondoke sina namna nitafukuzwa kazi si unajua kazi yenyewe hata week sina?".Watoto nao walimlilia baba yao sana asiondoke lakini Nicco hakua na njia zaidi ya kuondoka tu kwani alikua na nia ya kufanya hivyo kama sharti la mganga kwani alijua kwamba akilala hapo nyumbani lazima yeye na mkewe ashiriki tendo la ndoa kitu ambacho ni kukiuka masharti ya mganga kwani aliambiwa kwamba asikutane na mwanamke kimwili kwa muda wa miezi 6.Na hata alivyoondoka usiku huo alikwenda kulala gest Boma mjini hadi asubuhi na kuondoka na kurudi Mererani mgodini.
Kule mgodini aliendelea na kazi kama kawaida akijifanya kama wafanyakazi wengine na hakuonyesha ishara yoyote kwamba labda kafanikiwa kupata madini la hasha alinyamaza kimya tu na ikabaki siri yake na hata mkewe alikwisha mweleza kwamba asimweleze yoyote kwamba amepata milioni 45 ibaki siri kwani hata majambazi wanaweza kuwadhuru au hata kuwavamia na kuwaua.
Alifanya kazi mgodini sio kwa mapenzi ya ile kazi no,alifanya ile kazi huku akiendelea kuchunguza kwa umakini biashara ya madini na baada ya mwezi mmoja tu aliacha kazi pale mgodini na akageukia biashara ya kununua madini na kuuza.Hapo ndo Nico alianza kunusa utajiri kwani alikua anafanya biashara anatengeneza faida kubwa sana.Alijishangaa hata baadhi ya wafanyabiashara wenzake wa madini walimshangaa maana alikua akinunua tu akitafuta soko la madini anapata wateja wengi wakimiminika kwake kutoka ndani na nje ya nchi.Ndani ya miezi 6 nicco akawa anatengeneza mamilioni.Kipindi chote hicho hakua ameenda nyumbani zaidi ya kutuma pesa tu kwa kipindi chote cha miezi 6 alikua tayari amepanga nyumba ya kisasa Arusha yenye kila kitu na ya gharama, na akaamua kununua gari yake ya kutembelea maana biashara ilikua kwa kasi ya ajabu kwani alikua akipeleka madini mpaka nchi za jirani kama Kenya na Uganda.Na ile pete ya kijini aliyopewa na mganga ilikua ni kama nuizo kwake kabla hajafanya biashara yoyote na akishanuiza basi wateja watamiminika wa kutosha.
Miezi sita ilitimia sasa alikua huru kukutana na mkewe kimwili.Ndipo akafunga safari kuelekea moshi akiwa na gari yake ya kisasa na mpya kabisa Hakua Nico yule maskini hapana,alikua Nico mwenye pesa aliyepanga mjengo wa kisasa na gari na hakumuambia mkewe kama kanunua gari aliamua aende nalo Moshi ili akamsapraizi mke wake.Na pia alitakiwa akachinje ng'ombe nzima kule Moshi. Akiwa safarini na gari yake kuelekea moshi......
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom