Nsaidieni jinsi ya kumwacha huyu

Nsaidieni jinsi ya kumwacha huyu

Allency

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
16,311
Reaction score
16,333
Habari zenu wana jf, nsiwachoshe na salaam nyingi natumai ni wazima

Ok mimi nina girlfriend ambaye kaishia form 3, mapenzi naye nilianza kama mzaa vile, lakini badae nikajikuta nimezama mazima,

yeye hana kazi na nmejaribu kumtafutia sehemu nyingi lakini hataki kwenda kwani hajiamini na anaogopa sana ki-english, nami sina sehemu nyingine ya kuntafutia zaidi ya sehu hizo mana ndo wengi nawafahamu.

Kiukweli naona napoteza na kumpotezea mda mana siwezi kumuoa kwa sababu hizi
1: kwanza hajiamini hata kidogo,

2: Alishazaa mtoto mmoja na jamaa flani huko nyuma na mimi siwezi oa mtu aliyesha zaa, ( huu ni uamuzi wangu samahani kwa wale watakaohisi nmewakosea ama siko sahihi)

3: Elimu ni changamoto nyingine mana napenda mtu wa kusaidiana maisha

Swala lenyewe sasa:

Mara nyingi tunapogombana huwa anakimbilia kijiua na alishantamkia kuwa kama ntaamwacha basi maisha yake yataisha siku hiyo, hivi hili limekaa aje kisheria? Will I be held guity?

Kwa sasa nina kaa naye na ni mwaka saa natamani haya siku moja niende kazini na nipitilizie huko huko.

Jamani niko katika hali ngumu maana sijui nini cha kufanya, wana jf nawategemea sana kwa ushauri wenu juu ya hili, thanks
 
Asa kwanza nakushangaa wewe ulijua kuwa ana mtoto na akili yako ilishajiapiza kutokuwa nae kiranga gani kilikukumba ukaishi nae..

Kama nlivyosema mwanzo nlikuwa nachukulia masihara, sasa hata sima la kufanya eti
 
mueleze ukweli kuwa hauna future naye, hawez ishi bila wewe siku ukifa ataishije?

Ok, nacho hofia nikimwambia tu atajiua nami sijajua kama ntakuwa held guity ama la, hapo ndo pagumu, ama nkatoe taarifa polis kabla ya uamuzi huu?
 
Usimuache ghafla! Anza kumpotezea taratibu taratibu baada ya muda akili itamkaa sawa na ataona ni ujinga kujiua kwa sababu ya mapenzi!
Ila mapenzi ya ajabu sana, anayetaka kuacha yuko kwenye wakati mgumu na anayeachwa naye hivo hivo!
 
Ulivyomtongoza hukujua kama una mtoto....

Unaishi nae? Kama unaidhi nae beba nguo zako acha kila kikichomo kaanze upya mahala pebgine asipopajua.

Ukishindwa mwonyeshe hii thread asome.....

Ukiona kero mpeleke elimu ya watu wazima....

Ukiona vipi mfungulie biashara awe budy. Ikichanganya sepa kimya kimya
 
Hio very simple
Mnooooo

Ila dhambi but anyway kwa vile unataka uachane naye bila shida fanya haya yafuatayo..
Jaribu ku hack systems zake... hiyo uta mwacha tu baadae lazima achomoe mwenyewe

Pili;
Mtafutie mtu bila yeye kujua au huyo mtu kujua, then fanya kama umewafumania...
Lazima atasepa

Onyo; hizi mbinu ni hatari mno inakupasa uwe na akili nyingi mno maana things can turn around you
 
Duniani kuna mambo! Umekaa na binti wa watu weeee, umemfunua funua sasa ndo unajua kaishia form 3 huwezi muoa. Mi ningekwambia ntakuua wewe

Umeona wanaume wengi ndio maana wanakuwa vichaa kwa sababu wana mambo ya ajabu sana kama wewe ulieleta uzi. Inawezekana hata Tigo umemfumua kisha unamkimbia.
 
Habari zenu wana jf, nsiwachoshe na salaam nyingi natumai ni wazima

Ok mim nina girlfriend ambaye kaishia form 3, mapenz naye nlianza kama mzaa vile, lakini badae nkajikuta nmezama mazima, yeye hana kazi na nmejaribu kumtafutia sehemi nyingi lakin hataki kwenda kwani hajiamini na anaogopa sna ki-english, nami sina sehemu nyingine ya kuntafutia zaidi ya sehu hizo mana ndo wengi nawafahamu.
Kiukweli naona napoteza na kumpotezea mda mana siwez kumuoa kwa sababu hizi
1: kwanza hajiamin hata kidgo
2: Alishazaa mtoto mmoja ja jamaa flani huko nyuma na mim siwezi oa mtu aliyesha zaa, ( huu ni uamuzi wangu samahan kwa wale watakaohis nmewakosea ama siko sahh)
3: Elimu ni changamoto nyingine mana nhependa mtu wa kusaidiana maisha

Swala lenyewe sasa
Mara nyingi tunapogombana huwa anakimbilia kijiua na alishantamkia kuwa kama ntaamwacha basi maisha yake yataisha siku hiyo, hivi hili limekaa aje kisheria? Will i be held guity?
Kwa sasa nina kaa naye na ni mwaka saa nataman haya siku moja niende kazin na nipitilizie huko huko

Jamani niko katika hali ngumu ma sijui nin cha kufanya, wana jf nawategemea sna kwa ushauri wenu juu ya hili, thanks

Mkuu masuala kama haya mara nyingi yanahitaji wewe mwenyewe ufanye uamuzi. Hali halisi - uliyosema hapa na ambayo hukusema- wewe ndio unajua. Kama vile ulimpompata bila ushauri au msaada wa mtu. Just carry your own cross!
 
Ndio ukome kucheza na hisia za watu. Hata yeye anajijua kuwa soko limeshadoda ndio maana amekuganda mkuu huyo ni mkeo huna jinsi.
Sheri ya ndoa inasema ukiishi na mwanamke kwa mda wa miezi6 huyo tayar ni mkeo hata bila ya cheti cha ndoa hata kama utamwacha utalazmika kugawana vitu vyote hata kama ulikuwa na nyumba au shamba mtauza na mtagawana.......
Ndg acha kucheza na hisia za watu ni mwiko kabisa
 
Kimsingi nyote mnatatizo na mnahitaji msaada wa ushauri

Hayo mambo ambayo umejiwekea kama sifa za mtu ambae unahitaji kumuoa yanakutesa sana

Huyo nae ni kweli ana tatizo kubwa sana la kutokujiamini,anahitaji kupewa ushauri,lakini kikubwa sana ni kuwa wote wala hamjui kupenda ni kupi

Siku hizi vijana tuna matatizo sana!
 
Usimuache ghafla! Anza kumpotezea taratibu taratibu baada ya muda akili itamkaa sawa na ataona ni ujinga kujiua kwa sababu ya mapenzi!
Ila mapenzi ya ajabu sana, anayetaka kuacha yuko kwenye wakati mgumu na anayeachwa naye hivo hivo!

Tatizo hapa ni kuwa nakaa naye, waweza nipa maujanja ya kumpotezea? Mana kila jion lazima nrudi home
 
Duuh aisee you're time waster....mwambie tu ukweli utakukomboa, hajinyongi ng'oo.

Yani kujinyonga ni lazima mana asha jitapa kwa wenzie kuwa yeye ashapata ndoa, naameshajaribu zoezi hili zaidi ya mara tatu aisee, yani waweza dhani ni masihara ili ndo ukweli huo, nshajaribu kumpa umuhimu wa maisha yake na thamani yake lakini hajielew hata kdgo
 
Kimsingi nyote mnatatizo na mnahitaji msaada wa ushauri

Hayo mambo ambayo umejiwekea kama sifa za mtu ambae unahitaji kumuoa yanakutesa sana

Huyo nae ni kweli ana tatizo kubwa sana la kutokujiamini,anahitaji kupewa ushauri,lakini kikubwa sana ni kuwa wote wala hamjui kupenda ni kupi

Siku hizi vijana tuna matatizo sana!

Kaka hapa kwa mim si kuweka sifa ila ni kuangalia maisha zaidi ya leo, kama nina familia vp itaishi pindi nsipokuwepo? I know mapenz si elimu wala kitu chochote na pia maisha si mapenz pekee ni zaidi ya hapo yakiwa na mapenzi ndani yake, maisha navyojua mim yana mpangilio na i can say structured wakati mapenzi ya kweli haya angalii wala kufungaman na lolote. Mim kwa sasa sitafuti mapenz ila naangalia maisha kwa asilimia kubwa, ushauri please kaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom